Naomba msaada juu ya mtuhumiwa anayetakiwa kuwekewea mdhamana mahakamani ukoje kesi ya jinai. Na lingine ni halali kutoa pesa kwa ajili ya kumdhamini mtuhumiwa anapokuwa kituo cha polisi?
Dhamana ni haki ya msingi mtuhumiwa alienyimwa uhuru wake wa kwenda atakako kwa tuhuma zinazo mkabili kwenye kituo cha polisi au mahakamani.
Lengo la dhamana ni kumfanya mtuhumiwa huyo aliechini ya vyombo hivyo kupata uhuru wa kutembea huku ukivihakikishia kuwa mtuhumiwa atakuwa tayari kufika kwenye vyombo hivyo muda wowote atakapohitajika kwenye kesi
Isipokuwa tu kwenye kesi chache za jinai kama mauwaji ya kukusudiwa ujambazi wa kutumia silaha ; uhaini sheria inaruhusu dhamana kama haki ya mtuhumiwa.
Kutoa pesa polisi kama malipo ya dhamana sio halali ila kama pesa hiyo imetolewa kama bond au uhakikisho kuwa mtuhumiwa utamleta siku akihitajika na hiyo pesa unarudishiwa ikiwa utatimiza masharti ya kumpeleka mtuhumiwa na unatakiwa kuandikishana na wewe ubaki na nakala ya pesa yako uliyoacha.
Ila si hitaji la lazima kumdhamini mtu polis kwa pesa waweza kumdhamini kwa kuacha kitambulisho chako chochote kama pasport barua ya serikali za mtaa hata bila kitambulisho chochote kama utaonekana mwaminifu kumrudisha mtuhumiwa siku atakayohitajika.
Kwa upande wa mahakama hautofautiani sana na polisi ili mradi kosa la mtuhumiwa lisiwe kwenye kesi tajwa hapo juu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.