Habari wanajamii wenzangu,
Baada ya salamu niwapeleke moja kwa moja kwenye hoja
Kuna hili swala ya kuthibitisha vyeti kwa kutiwa muhuri wa mwanasheria, vyeti hivyo ni kama;
(cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu katika ngazi mbalimbali utakazo kuwa umepitia kama astashahada, stashahada, sekondari n.k)
utaratibu huu nimeshindwa kuuelewa na sioni umuhimu wake kwa sababu zifuatazo
#Kwanini visibitishe wakati vyeti hivyo tayari vina muhuri na saini za viongozi wa taasisi inayokutunuku cheti/vyeti hivyo.
Je taasisi hizo zimeshindwa kuaminika?
#Nguvu ya muhuri na saini za wasimamizi wa izo taasisi ni ipi kama vyeti bado vitahitaji kuthibitishwa
#Kama muhuri wa mwanasheria ni muhimu kwanini lisiusishwe moja kwa moja na mwanasheria wa taasisi inayokutunuku chetii
Karibuni tuelimishane kwa hoja katika hii dunia ya sayansi na teknolojia