Utaratibu wa kuoa na kuolewa

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,415
119,417
Habari zenu wapendwa,
Kila jamii ina utaratibu wake linapokuja suala la ndoa..utaratibu wa kabila langu siujui kiundani ila naomba niwashirikishe utaratibu huu niliowahi kukutana nao.
Ni hivi niliwahi kuishi katika mkoa mmoja huko kwetu nyanda za juu kusini, utaratibu wa ndoa ulinishangaza kama sio kuniogopesha. Na utaratibu huu umefanyika mpaka miaka ya tisini mwishoni hadi elfu mbili kabisa...sina hakika kama siku hizi wameacha. iko hivi kijana akimpenda binti anamvizia nyakati za jioni akiwa anatoka labda shambani, kuchota maji n.k hata kama ametumwa na wazazi safari itaishia hapo, anabebwa jujuu hadi nyumbani kwa kijana analala nae then asubuhi wanaenda kusema kwa wazazi wake. Kwa hiyo wazazi wasipomuona binti jioni wanasubiria ugeni asubuhi
Wapo waliokuwa wanabebwa na watu ambao ni wapenzi wao ila wengine walikuwa wanabebwa tu as long as kijana wa kiume amependa binti unajikuta umeolewa kwa staili hiyo.
Kwa maana hiyo ukisema yes kwa mtu inatakiwa uwe umemaanisha kweli na uko tayari kuishi nae maana siku isiyo na jina utajikuta uko ndani tayari.
Hali ilikuwa mbaya siku ambazo wanafunzi walikuwa wanafanya mitihani ya mwisho ( darasa la saba) , mabinti wengi walikuwa 'wanatekwa' na ikumbukwe miaka hiyo hasa maeneo ya vijijini watu walikuwa wanamaliza shule na miaka 17, 18 au 19.
Mimi binafsi niliposikia hiyo kitu niliogopa si kidogo, tena waliokuwa wananisimulia wananitisha kabisa kwamba hivi na wewe jiandae siku ukionekana umenona nona utabebwa tu kwani we nani? Nashukuru Mungu niliondoka nikiwa bado mdogo maana nahisi kikombe hicho kisingeniepuka na sasa hivi ningekuwa naongea habari nyingine kabisa.
 
Back
Top Bottom