Mimba ya nne kujifungua kwa njia ya kisu, nini madhara au athari kwa mama?

walikuyu

JF-Expert Member
Jul 27, 2018
753
1,504
Wakuu habari za jioni, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kuna mama ni mjamzito kwa sasa ana watoto watatu lakini ametoka kujifungua mwaka umepita mtoto wa mwisho na uzao wote ni kisu. Sasa swali langu uyu mama alitoka kujifungua mwaka jana na sasa ni mwaka tu umepita sasa sijui niseme bahati mbaya amepata mimba nyingine.

Swali langu kwenu vipi kama akihamua kujifungua je kuna madhara ya kiafya atapata ambayo yatagharimu uhai wake? Au atoe tu huu ujauzito?

Naomba ushauri wenu najua hapa kuna madaktari mbalimbali wenge kujua mambo ya afya.

Karibuni kwa mchango.
 
Unaomba ushauri lakini unaigopa kusema mke wangu, unajaficha ficha eti huyu mama loh.
 
Wakuu habari za jioni, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kuna mama ni mjamzito kwa sasa ana watoto watatu lakini ametoka kujifungua mwaka umepita mtoto wa mwisho na uzao wote ni kisu. Sasa swali langu uyu mama alitoka kujifungua mwaka jana na sasa ni mwaka tu umepita sasa sijui niseme bahati mbaya amepata mimba nyingine.

Swali langu kwenu vipi kama akihamua kujifungua je kuna madhara ya kiafya atapata ambayo yatagharimu uhai wake? Au atoe tu huu ujauzito?

Naomba ushauri wenu najua hapa kuna madaktari mbalimbali wenge kujua mambo ya afya.

Karibuni kwa mchango.
Hakuna madhara
 
sam

samahani na mi naomba kuuliza. je kama nilijifungua uzao wa kwanza op kwa ajili ya complication flani je ni lazima uzao unofuata nimpate Dr yule yule anihudumie.
Siyo lazima lakini inakuwa vizuri mimi mke wangu alipata scenario kama yako. Mimba ya kwanza hakuwa na shida ila mtoto hakugeuka wakati wa kujifungua ikabidi afanyawe upasuaji. Sasa alipopata mimba ya pili akaenda kwa daktari mwingine kwa vile alikuwa mkoa mwingine. Daktari akamwambia hana shida ila angekuwa yeye ndiye amemfanyia upasuaji wa kwanza angemwacha ajifungue kawaida. Ila kwa vile siyo yeye hawezi kushauri kwa kuwa hajui yule aliyemfanyia alimshona kwa namna gani. Kwa sababu kama hakumshona vizuri kuna risk ya mshono kuachia wakati wa kusukuma mtoto na hiyo inakuwa risk kwa mama na mtoto. Hivyo dokta akatuacha tuamue kama ajifunge kawaida au kwa upasuaji. Sisi baada ya kufanya tathmini tukachagua upasuaji. Na mimba mbili zilizofuata tulienda kwa daktari yuleyule yuko mhimbili na hatujawahi kupata changamoto yoyote. Ahsante
 
Mimba zingine alipitisha mda gani?
 
zipo hatari nyingi tu za Upasuaji wa Mara kwa Mara (Cesarean Sections) ni vyema kujiandaa nalolote.
  1. Kushikamana kwa Tishu (Adhesions): Upasuaji wa mara kwa mara unaweza kusababisha tishu kushikamana, hali ambayo inaweza kufanya upasuaji wa baadaye kuwa mgumu zaidi na kuongeza hatari za kiafya.
  2. Uwekaji wa Plasenta Mbaya (Placenta Previa, Placenta Accreta): Hatari ya matatizo haya inaongezeka baada ya upasuaji wa mara kwa mara. Hii inaweza kuathiri sana ujauzito na kujifungua.
  3. Uvimbe wa Kovu (Uterine Scar): Kovu la upasuaji linaweza kuwa na hatari ya kupasuka (uterine rupture) katika ujauzito unaofuata kabla au mda wa kujifungua, hali ambayo ni hatari sana kwa mama na mtoto.
 
Muhimu apate uangalizi makini wakati wa ujauzito, at least twice per month ahudhurie clinic, then ataweza kujifungua salama kabisa. Muhm mkubali gharama za uangalizi
Sawaa mkuu ilo litafanyiwa kazi kwa asilimia mia kabisa, ubarikiwe sana kwa msaada wa mawazo yako
 
Back
Top Bottom