GE2025 Utaratibu uliotumiwa na CCM Kumpitisha Samia Kugombea Urais 2025 Umetengeneza Dangerous Precedent Kwa Chama!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Pulchra Animo

Platinum Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
6,767
Reaction score
10,312
Inaonekana CCM iko mikononi mwa watu ambao uwezo wao wa kuona mbele ni mwisho wa pua zao. Sijui kama wamewahi kufikiria uwezekano wa historia kujirudia!

Hatuombei iwe hivyo, lakini ikitokea (for any reason) Samia ameshindwa kumaliza term anayopigana kuichukua na hivyo Nchimbi (VP wake mtarajiwa) automatically akarithi kiti cha Rais kwa mujibu wa Katiba,

CCM itakuwa na ujanja gani au sababu zipi za kumzuia Nchimbi kupindisha mchakato wa kupata mgombea Urais kwa ticket ya CCM 2030 na kujiteua yeye kuwa mgombea, kama alivyofanya Samia? Obviously, itakuwa almost haiwezekani kumzuia.

Je, hiki ndicho CCM mlikusudia mliporuhusu uhuni uliofanyika January 2025? Kama ndivyo hivyo, ni lini wanachama wa CCM watapata fursa ya kuweka mgombea Urais kwa ticket ya CCM wanayemtaka wao wenyewe, kama historia inajirudia?
 
Mtu yeyote akishika usukani atabuni utaratibu wake kumfanya anayetaka akamate usukani.

Huu utaratibu umekuwepo tangu vyama vingi vianze mbona kama Mwaka huu kelele ndio zinakuwa nyingi. Kuna story KUWA hata JK aliwahi kushinda mwalimu Nyerere akapindua matokeo nyuma ya pazia eti Bado kijana.
 
Huu utaratibu umekuwepo yangu vyama vingi vianze mbona kama Mwaka huu kelele ndio zinakuwa nyingi. Kuna story KUWA hata JK aliwahi kushinda mwalimu Nyerere akapondua matokeo.
Assuming Nyerere kweli alifanya hivyo, hicho bado ni kitu tofauti kabisa. Aliyeshika usukani hakupindua matokeo!
 
Hata JPM pia inasemekana hakushinda kwenye mchujo KWA mujibu wa malalamiko ya waliokuwepo na wagombea wenzake kwenye tatu Bora. Huoni hii ndio trend na hata huko mbele hakutakuwa na cha tofauti kama hizo story huwa ni za kweli.
 
Inaonekana CCM iko mikononi mwa watu ambao uwezo wao wa kuona mbele ni mwisho wa pua zao. Sijui kama wamewahi kufikiria uwezekano wa historia kujirudia!

Hatuombei iwe hivyo, lakini ikitokea (for any reason) Samia ameshindwa kumaliza term anayopigana kuichukua na hivyo Nchimbi (VP wake mtarajiwa) automatically akarithi kiti cha Rais kwa mujibu wa Katiba,

CCM itakuwa na ujanja gani au sababu zipi za kumzuia Nchimbi kupindisha mchakato wa kupata mgombea Urais kwa ticket ya CCM 2030 na kujiteua yeye kuwa mgombea, kama alivyofanya Samia? Obviously, itakuwa almost haiwezekani kumzuia.

Je, hiki ndicho CCM mlikusudia mliporuhusu uhuni uliofanyika January 2025? Kama ndivyo hivyo, ni lini wanachama wa CCM watapata fursa ya kuweka mgombea Urais kwa ticket ya CCM wanayemtaka wao wenyewe, kama historia inajirudia?
Mkuu, mwaka 1962 mwezi Mei Mwalimu J.K Nyerere akiwa raisi wa TANU alikuwa na andiko lake lenye kusema "Tujisahihishe".

Hilo ndilo linaweza kutumika mkuu...
 
Hizo sasa ni conspiracy theories!
 
Ndio maana Polepolepolepole anasema mchakato urudiwe.✍️
 
Nakumbuka vijana wetu wa bongo fleva wana wimbo wanasemaga "huu mwaka eeh! Ni mwaka wa kufosi" ...wacha tule mtori nyama ziko chini!
 
Mkuu, mwaka 1962 mwezi Mei Mwalimu J.K Nyerere akiwa raisi wa TANU alikuwa na andiko lake lenye kusema "Tujisahihishe".

Hilo ndilo linaweza kutumika mkuu...
Hata sasa hivi kuna fursa nyingi za kulitumia, lakini limegeuziwa mgongo! Nini kitalifanya lisigeuziwe mgongo huko tuendako?
 
Assuming Nyerere kweli alifanya hivyo, hicho bado ni kitu tofauti kabisa. Aliyeshika usukani hakupindua matokeo!
Mzee Kikwete alipata kura nyingi lakini zikiwa chini ya asilimia 50 ya wajumbe waliopiga kura kwenye mkutano Mkuu wa mwaka 1995. Mzee Mkapa akawa wa pili na mzee Msuya wa tatu.

Mwalimu Nyerere alitoa hoja kwamba ili mgombea awe na nguvu ni muhimu angalao 50+1 ya wajumbe wamkubali. Hoja yake ilikubaliwa na ikabidi upigaji kura urudiwe kwa wagombea wawili wa kwanza. Jina la Mzee Msuya likaondolewa na kubakia mzee Kikwete na Mkapa. Wajumbe walimpitisha Mkapa. Kwa kifupi Nyerere hakufanya mauzauza ya kumwengua mzee Kikwete. Uchaguzi huo ulipewa live coverage.
 
Mtu yeyote akishika usukani atabuni utaratibu wake kumfanya anayetaka akamate usukani.

Huu utaratibu umekuwepo tangu vyama vingi vianze mbona kama Mwaka huu kelele ndio zinakuwa nyingi. Kuna story KUWA hata JK aliwahi kushinda mwalimu Nyerere akapindua matokeo nyuma ya pazia eti Bado kijana.
Kikwete analipa kisasi. Si akina Warioba walikuwepo na wakabariki Nyerere kupindua meza? Alikuwa anawazoom
 
Mzee Kikwete alipata kura nyingi lakini zikiwa chini ya asilimia 50 ya wajumbe waliopiga kura kwenye mkutano Mkuu wa mwaka 1995. Mzee Mkapa akawa wa pili na mzee Msuya wa tatu.

Mwalimu Nyerere alitoa hoja kwamba ili mgombea awe na nguvu ni muhimu angalao 50+1 ya wajumbe wamkubali. Hoja yake ilikubaliwa na ikabidi upigaji kura urudiwe kwa wagombea wawili wa kwanza. Jina la Mzee Msuya likaondolewa na kubakia mzee Kikwete na Mkapa. Wajumbe walimpitisha Mkapa. Kwa kifupi Nyerere hakufanya mauzauza ya kumwengua mzee Kikwete. Uchaguzi huo ulipewa live coverage.
Una kumbukumbu nzuri sana. Wasiokumbuka vizuri wanachapia tu kwamba Kikwete aliondolewa kinyemela na Nyerere!
 
Back
Top Bottom