Utapeli wa baadhi ya Recruitment Companies

Utapeli wa baadhi ya Recruitment Companies

denis fourplux

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2017
Posts
1,050
Reaction score
1,395
Habari za Jioni ndugu zangu.

Natumain wote mu wazima wa Afya, naomba nijikite katika Mada moja kwa moja kama nlivyo ambatanisha apo juu.

UTANGULIZI
Kwa miaka takribani 10 sasa tumekua na changamoto za Ajira katika nchi yetu ambapo kila mwaka kulingana na idadi ya vyuo kuongezeka wahitimu pia wanamwagwa kwa wingi katika kada tofauti tofauti na kwakua wahitimu ni wengi ivyo Job Market haiwezi kukidhi mahitaji ya wahitimu wote.

Tumekua na mifano mingi,
mfano pale TRA waliwai kuita interview nafasi kama 12 ila walio apply na kuhudhulia walikua ni zaidi ya 4000, kwa muonekano wa macho ya kawaida ni kiashiria kua watu wengi hawana ajira

ila pia mfano wa pili Mwaka huu mwezi wa 10 tume ya uchaguzi ilihitaji watu kwa ajili ya zoezi la kupiga kura na si ajabu watu waliudhulia pale Taifa hususani wilaya ya Temeke maana kulikua na nyomi la watu wanaozidi ata 10,000 wakitaka kujaza nafasi izo za muda.

Sasa kutokana na Changamoto izo za ajira na kua ni tatizo now kuna kampuni za kuajiri ambazo zinakaa katikati ya Job seeker na Employer yaani wao wameliona tatizo na kulifanya fursa mara nyingi hawa ni watu waliosoma HRM , Public relation na Mambo ya Labour Law watu hawa wanaungana na kufungua kampuni kwa lengo la kusaidia vijana wapate kuconnectiwa na waajili.
Mfano wa Kampuni izi ni Empowered, Brightmonday,Zoomtanzania, Vipaji inc nk.

Sasa naomba niwatoe tongotongo kidogo izi kampuni sasa zimekua ni nyingi na ili uweze kupata angalau kuitwa katika interview yakupasa ujaze fomu yao ambayo utalipia gharama mfano elfu 20, 30,40 nk kulingana na kampuni.

Kampuni nyingi ni kweli zinasaidia vijana wenzangu kupata ajira na wao wanacho kusaidi nikukupa au kukuconnect na muajili upate interview na kama ukifanikiwa katika interview basi unakua umepata kazi.

UTAPELI UNAANZA WAPI
Kwakua watafuta kazi ni wengi kampuni izi zimeunda mfumo wa kutangaza kazi kupitia njia mbali mbali mfano unaweza kutana na tangazo anahitajika Data clerk officer wanaweka na sifa baada ya apo wanaweka detail za email au namba za simu kwa muongozo zaidi.

Na kwakua watafuta kazi ni wengi wanapita katika site tofauti tofauti watakutana na tangazo wataamua ku apply kwa kutuma CV au kupiga simu kuomba waelekezwe ofisi ziko wapi kupeleka Taarifa zao.

Ukiisha kamilisha Taratibu wao watapitia CV watachukua namba zako na za marefaree na watakupigia simu ufike ofisini siku fulani, baada ya kufika ofisini mtawekwa katika kundi la watu wengi mtaanza pewa detail za kuhusu iyo kampuni na baada ya apo mtaambiwa kujiunga ukikubali utatoa pesa utajaza fomu na lisiti utapewa labda ya EFD au ya kawaida.

Baaada ya kujaza fomu zao utatumiwa msg inayoonesha siku, mahala, saa na kampuni unayotakiwa kwenda kufanya interview.

Kama ukipata kazi mkataba unakuja katika makato ambayo kampuni utakukata asilimia flani mfano 30% katika mshahara wako kwa muda labda wa mwezi 1 au 3.

Mara nyingi interview unazotafutiwa na izi Recruitment Company ni ndogo ndogo ndugu zangu ni kwa wachina yaani wao wanakutafutia kazi kwa wachina ukauze mabegi, saa, vyombo, foodsuppliments, au uzunguke mitaa ya k koo ukipita kila mitaa kuandika taarifa za maduka yana deal na nini na ujira wako ni sh 5000-7000.

Na kama si kwa wachina watakutafutia interview katika vijiwanda vidogo vya masofa, magodoro,au supermarket na sheli.

Sasa kwa mantiki hii jaribu kufikilia unapata kazi mshahara 150,000 toa 30% miezi mitatu na apo ulijaza fomu yao ya 40,000 inamaana watakua wanakukata 45,000 kila mwezi kwa miezi 3 ambapo wewe utabaki na 105,000.

Sasa kwa kiasi hiki cha pesa sawa hauna Ajira ila kwanini uteseke, umesoma kwa shida na gharama kubwa ila ujira wa kazi ni wakinyonyaji sana yani kama unakaa eneo la mbali na kazi hii pesa itakua inaishia kwenye nauli tu.

Ubaya zaidi najua watu wanawajua wachina na wahindi walivyo wanyonyaji na wenye roho mbaya utafanya kazi kama punda na mda mwingine utafanya ata zisizo katika mkataba wako.

Kunautofauti gani wa muhitimu wa chuo na mdada wa kazi za ndani ambae yeye anapata unafuhu kwa kukaa kwa boss, chakula, maladhi na vingine boss anatimiza au muhitimu uyu anatofauti gani na wabeba mizigo au barmaid?

Na izi kampuni ndogo ndogo za kutafuta ajira ndio zinazo haribu taswira ya kampuni kubwa na mda huu wameenda mbali kwakua unatoa CV yako wanachukua namba za marefaree wako wanapigiwa na wanajieleza kana kwamba wanakufahamu sana kwakua detail za CV Wanazo kumconvice mtu ni rahisi sana hivyo kutapeliwa kwa njia hii.

HITIMISHO:
Ukitaka kujiunga na Recruitment agency au Company tafuta zile kubwa kubwa kama Eurolink, Vipaji, Brightermonday especially tafuta zile zinazo operate zaidi ya nchi moja ila nyingi za kwetu wazawa hazina Connection yoyote zaidi ya kuibia wahitimu waliochoka zaidi

Mfano pale Makumbusho stendi kuna kampuni ya Muhindi na mbongo wanajiita JOB JUNCTION hawa jamaa n kampuni ndogo sana hawana website,kijiofisi ni kiframe kimoja, taarifa zao ukitaka wanakwambia njoo ofisini kwetu na ukisearch google hupati taarifa zao kiufupi niwapigaji ndugu yangu aliwai kwenda pale akakuta vijana kama 40 ivi ambao walifanya registration sku iyo yeye akashindwa kwakua alikua hana pesa sasa unapata ona kwa siku moja iyo.

40,000x ada ya kujiunga(20,000) ni sawa na 800,000 per single day kesho yake amerudi tena kakuta wengine inamaana hawa jamaa wanatengeneza pesa ata zaidi ya 10M per months kwakua wahitaji wa huduma ni wengi na kazi watakazo kuunga amini ata wewe unaweza zitafuta kazi za sales zipo nyingi sana.

Lakini pia unapotafuta kazi usipende kutuma CV au taarifa zako katika email ambazo sio za kampuni mfano unapata ujumbe mwalimu wa Chemistry anahitajika Dodoma, Mshahara ni 800,000 tuma detail kwenye email hii.

hatunamajanga@gmail.com unapokutana na tangazo kama ili achana nalo ni matapeli hawa utatuma CV watatumia detail zako kuibia watu kama Refarees wako

Kiashiria cha kampuni kama inatambulika ni
1. Anuani halisi mfano
info@ kazinikwetu.go.tz inamaanisha hii kampuni ina website official ila sio kutuma nyaraka zako katika email ya mtu binafsi inayo kua na gmail, hotmail, yahoo

2. Lazima kampuni iwe na taarifa sahihi mfano unapoingia google lazima utapata location, historia ya kampuni, Mission, vision nk ila kama ukikuta hivi avipo badala yake ni namba za simu anza kushtuka kwanini uitwe ofisini kupata maelezo wanaficha nini awa ndo matapeli wenyewe

Chukua taadhali kua makini achakua fursa au daraja la kunenepesha wengine

Asante.
Denis4+
 
Neno kuwa makini, chukua tahadhari, etc hayajawa na msaada sana kwa watu wenye uhitaji usiopimika.

Mtu anapokuwa hata mlo wake wa tabu akiambiwa atoe 20,000 apate kazi ya laki2 anampigia mjomba wake anatumiwa hiyo 20,000 mengine anapotezea.

Bahati mbaya sana shida haina adabu. Cha muhimu ni vijana kupeana maarifa ya kujikwamua kama biashara ndogo ndogo na jinsi ya kuzianza kwa mtaji zero. Hapo ndio tutasaidia wengi.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Aisee mkuu,

Kwanza pole sana kwa ndugu yako huyo "kupigwa". Na kwa niaba ya wengine, tunashukuru kwa kushea jambo hili ili watu wapate kujua Mambo yalivyo!!

Mi ushauri wangu wa ujumla tu kwa wahitimu, jaribuni kufanya na jambo lingine kama kuajiriwa kumeonekana hakuna dalili. Acha kupoteza pesa zaidi ili uajiriwe, siku hizi hakuna ajira jamani!!

Kwa wale ambao bado wapo masomoni, ni bora wakajiandaa kisaikolojia na kuwa na plan A na B, kwamba ikishindikana kuajiriwa moja kwa moja ana translate kwenye plan B

Asante!
 
Hivi kuna aliwahi pata kazi kupitia hizi recruitment agencies?

Maana, pamoja na kukidhi vigezo vya maombi, toka nianze kuapply sijawahi itwa interview zaidi ya kukutana na mataperi tu
 
Tz soko la ajira limezidi haribiwa na kuzitreat sekta binafsi na wawekezaji kama wezi.

Jana nikiwa Makambako kuna tangazo lilikua linasema waendesha maguta na bajaji wanatakiwa waanze kulipa kodi na kutoa risiti za efd.

Lete tena stori ya kujiajiri.
 
Back
Top Bottom