Utapeli wa ardhi plan ltd-tabora

Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,858
748
Habari zenu wana jamvi,

Hivi karibuni kumekuwa na mgogoro wa ardhi katika maeneo ya Uledi hapa mjini Tabora, ambapo Manispaa ya Tabora ilitaka kuwafukuza wakazi wa mtaa wa Uledi kwa madai kuwa ni wavamizi wa eneo hilo.

Wakazi wa uledi wakachukua jukumu la kuishtaki Manispaa ya Tabora mjini,na katika shauri hilo wakazi wa Uledi walishinda huku ikiamriwa kuwa wao wapewe kipaumbele na kupimiwa maeneo yao kwa mujibu wa taratibu za mipango miji...na mahakama ikaionya Manispaa kuwaita wakazi hao kuwa ni wavamizi.

Ikawa wakati Manispaa ikifanya taratibu ya kuwapimia wakazi hao,imeibuaka kampuni ijulikanayo kama Ardhi plan Ltd na kutaka(bado inang'ang'ania) kuwatapeli na kuwadhurumu wakazi wa uledi kwa makubaliano yafuatayo ambayo wakazi hao wamekataa na sasa kampuni ya Ardhi Plan Ltd inatumia migongo ya Viongozi wa manispaa(akiwepo Mkurugenzi wa Manispaa) kufanikisha utapeli huo;



  1. Kila ekari moja itapimwa kwa mita za mraba 4,047.
  2. Kila ekari moja itapunguzwa mita za mraba 1,047 kwaajili ya barabara za mitaa.
  3. Mita za mraba 3,000 zilizobaki zitapimwa ili kupata viwanja vitano(5).
  4. katika kila viwanja vitano wao (Ardhi Plan Ltd) watawagawia wakazi wa uledi viwanja vitatu na wao(Ardhi Plan Ltd) watachukua viwili kama malipo ya gharama za upimaji.
  5. Hawatafidia mti au nyumba yoyote itakayopitia/kuvunjwa wakati wa zoezi la upimaji.
  6. Kwamba baada ya zoezi zima, wakazi wa uledi watapaswa kwenda Manispaa kwaajili ya kulipia gharama nyingine ili kipata leseni au hati za makazi

Na kwa taarifa za uhakika ni kuwa maeneo hayo ya Uledi tayari ilishachorwa Plan na Manispaa ambayo iliwahi kuoneshwawa mahakamani wakati Manispaa iliposhitakiwa na wakazi hao.

Wakazi wa Uledi walichukua jukumu la kuwasiliana na Mkurugenzi wa Ardhi Plan kuhusiana na tuhuma hizi za utapeli, akadai kuwa maswali yote aulizwe diwani na Mkurugenzi kwani wao ndio wabarikio zoezi zima la kampuni yake.

Diwani wa kata hiyo akadai kuwa yeye anajua zaidi ya wakazi wote wa Uledi na kuwa hivyo ndivyo itakavyowasaidia na yeye ndiye aleyeipigia chapuo kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora amekanusha kuhusika pia kujua uwepo wa kampuni hiyo kwenye mamlaka yake.

Wakazi wa Uledi wameapa kutokukubali utapeli huo, wako tayari kupigania ardhi yao hata kwa kutoa maisha yao.

Maswali nijiulizayo ni kwamba;

Je Serikali ya Tanzania na mamlaka zake zinazidiwa nguvu na akili na makampuni haya ya kitapeli?

Je uko wapi uzalendo wa Kampuni hii ya Tanzania ya Ardhi Plan LTD kwani haihitaji degree au Ph.D kutambua utapeli wao?

Je ni kweli Mkurugenzi huyu hana taarifa hizi au na yeye ni mmoja wa wafaidikaji katika utapeli huo?
kwa msingi huu huyu waweza kumuingilia mkurugenzi nyumbani kwake na kuanza kucheza na mkewe usiku kucha huku naye akiwa pembeni na asubhi akajibu kuwa hana taarifa ya purukushani nzima.
 
Back
Top Bottom