MstahikiMeya
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 1,633
- 561
Wapendwa kuna utapeli imeingia mjini wa kupigiwa cm na mtu anakwambia nenda ofisi za tigo (yumkini akasema voda, airtel, etc) anakutaja majina yako yote na anasema namba yako imechaguliwa kupata promotion na hivyo nenda ofisi za watoa huduma ukapate hizo hela. Anakupatia Namba za kuingiza ili uretrive (upate) namba ya utambulisho wako huko tigo, voda,....na anaanza na coding *148*......#. Maana yake ni kwamba ukibonyeza reli utakuwa unaruhusi kumtumia ama hela ama password yako ili kumwezesha yeye kutoa hela. Kwa wanaopenda hela za bure yumkini wameishalizwa wengi lkn bado zoezi hilo la utapeli linaendelea. number yenyewe inayotumika (yumkini anazo nyingi) ni 0658104199, nimeona niwataarifu muwe makini. Pls share taarifa hii na mengine ili kuvunja mtandao huu. Najua watu wakipata kuelewa itawagharimu muda kubuni mbinu nyingine.