THE BROKER
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 765
- 950
Duh, pole kwa kuja Dar jana na kutapeliwa hapohapo. IT zinapita Magufuli Stand na unatoa pesa hujaona wala kuingia kwenye gari!!!Wadau napenda kuwajulisha kuwa mnapofika katika stand hii na kama unataka kusafiri usiku kuwa kutumia magari maarufu kama IT na hasa ukishukia stand ya daladala unakutana na wapiga debe wanaotangaza kuwa kuna magari ya IT wakati si kweli.
Wanachofanya wanakuchukua hadi ndani ya kituo cha Magufuli kwenye ofisi za kukatia tiketi mabasi na kukuhakikishia kuwa kuna basi linaloondoka usiku huo huo wakati si kweli.
Stand ya Magufuli hakuna basi lolote linaloruhusiwa kuondoka usiku yote yanaondoka asubuhi kuanzia saa 12.
Mi yamenikuta nikaenda hadi kituo cha polisi lakini hakuna msaada wowote wa maana na inaonekana mapolisi wanajua mchezo huu na hawaonyeshi kuukomesha wma wameshindwa au wanalambishwa asali na wahusika.Hali hii wadau inasababisha usumbufu mkubwa usio wa lazima.Serikali ipige marufuku kabisa wapiga debe ambao wanaendelea kuwa kero sana kwa abiria.
Pia inaonekana hata tiketi za mtandaoni bado ni issue isiyo ya lazima kwa hawa jamaa.Kwa kifupi kunahitajika kampuni ya kusimamia logistics zote za stand ili kuleta tija na hadhi ya stand hii ya kimataifa.
Wewe ni mshamba hapo hauna hoja kabisa walikuona zoba ukaingizwa kingi na kama mjanja huwezi kutoa pesa bila kuona basi na hasa likiwa na abiri
Pole sana NDUGU. Na Asante Kwa kutoa angalizo. Hapo kuna watu hawatimizi wajibu wao. Pengine wanasubiri yule Mr. President afufuke awaambie Cha kufanya maana alitoa angalizo kuhusu jina lake kutumika kama jina la kituo hicho! Naona sasa wanaanza kuchafua jina lake.Wadau napenda kuwajulisha kuwa mnapofika katika stand hii na kama unataka kusafiri usiku kuwa kutumia magari maarufu kama IT na hasa ukishukia stand ya daladala unakutana na wapiga debe wanaotangaza kuwa kuna magari ya IT wakati si kweli.
Wanachofanya wanakuchukua hadi ndani ya kituo cha Magufuli kwenye ofisi za kukatia tiketi mabasi na kukuhakikishia kuwa kuna basi linaloondoka usiku huo huo wakati si kweli.
Stand ya Magufuli hakuna basi lolote linaloruhusiwa kuondoka usiku yote yanaondoka asubuhi kuanzia saa 12.
Mi yamenikuta nikaenda hadi kituo cha polisi lakini hakuna msaada wowote wa maana na inaonekana mapolisi wanajua mchezo huu na hawaonyeshi kuukomesha wma wameshindwa au wanalambishwa asali na wahusika.Hali hii wadau inasababisha usumbufu mkubwa usio wa lazima.Serikali ipige marufuku kabisa wapiga debe ambao wanaendelea kuwa kero sana kwa abiria.
Pia inaonekana hata tiketi za mtandaoni bado ni issue isiyo ya lazima kwa hawa jamaa.Kwa kifupi kunahitajika kampuni ya kusimamia logistics zote za stand ili kuleta tija na hadhi ya stand hii ya kimataifa.
IT haziruhusiwi kubeba abiria. Ni madereva wao tu wanajiongeza kimjini mjini.Hivi pia ni kwa nini hizo IT zinaachiwa na mamlaka husika kubeba abiria?
Hata hizo haziruhusiwi kubeba abiria na sidhani kama zipo sahivi maana ukikutwa faini yake utasema kwanini musiba ajapata msiba.Ungeenda zako kibo ungekua special Hire za kutosha za uhakika.
Dar ipi iyo?Mimi nafahamu. IT stands for in transit
Ila nimeishawasikia watu wa Dar waki-refer gari yoyote ya binafsi kama IT. Otherwise, unaendaje ndani ya stendi ya Magufuli kutafuta gari ya IT?
Nyingine ziko Camel karibu na Malawi Cargo.It zote huwa wanaanzia pale pemben ya VETA pale sheli ya mafuta kwenye fly over
Wewe ndiyo umemsaidia maana wengine wanamzodoa tuIT ziko bandarini, chang’ombe, Buguruni, kibo, mbezi stand nje uelekeo wa moro, kibamba shule, maili moja, misugusugu, kongowe na kuendelea, na huwezi kutoa nauli hujaingia kwenye gari hapo kuna costa za hakuna kulala za uyole to dar, au dar to mbeya, au arusha na moshi to Dar au dar to arusha na moshi na zote hua zina parking zake zinazoeleweka anzia kidongo chekundu,
Hapo sasa, nami ndio nashangaa gari ya IT ikafanye nini stand ndani mule? Mashamba ni mshamba tu🤣Gari ya IT ndani ya stendi!
asanteHayo ni magari yaliyosajiliwa rasmi kwa ajili ya kusafirisha abiria wenye shughuli zao binafsi.
Yaani kama unataka kusafirisha msiba, au kusafirisha kundi la watu fulani kutoka sehemu moja kwenda nyingine, mnakodi kwa makubaliano maalum.
KabisaaUngeenda zako kibo ungekua special Hire za kutosha za uhakika.