Utapeli kwenye kilimo/ufugaji

Utapeli kwenye kilimo/ufugaji

bkas

Member
Joined
May 20, 2018
Posts
34
Reaction score
17
Kumekuwa na wimbi wa vikampuni vinavyojihusisha n kilimo vikidai wanakulimia/kufuga huku ww ukitoa gharama zote za shughuli alafu kwenye mavumo mnakatana kwa percent mara nyiingi hufanya 25% kwao alafu 75% za kwako baada ya kutoa mtaji uliowekeza..hili ni wazo nzur sna ila huwa havifanyi hivyo huishia kuwatapeli watu n watu wengi huingia kwenye huo mtego wakiambiwa utapata faida ndani ya miez mitatu eg (kilimo cha tikiti etc)..wafanyakazi wengi huingia huku mana wao hawana muda wa kusimamia shamba anaona bora aweke hela izunguke n aje apate pesa nyingi sna baada ya miez mitatu

Naomba nitoe mifano zahili ya vikampuni hivyo naaza n VJ AGRIMARKET SOLUTION hiki ni kikampuni kilichoanzisha n mwanadada mmoja hivi alikuwa anajitangaza hadi kwenye magazeti n tv (channel ten) akidai anapata hadi mil 100 kwenye kilimo ilihali maisha yake yenyewe kwa uhalisia sio hivyo kabisa n alipoanzisha kampuni hiyo alijitangaza sna kwenye chanel ten huku akiongelea kuwa ukijiunga unajiunga kwa ada ya tzs 1,000,000 kma mwanachama alafu anakulimia shamba la ekari 1 la matikiti kwa mwaka utakuwa na 10milion daaah hamna cha pesa yyte ile iliyotolewa kwa wanachama hao kuanzia alipoanza mwaka jana hadi sasa n bado anaendelea kupokea wanachama ana jumla takriban ya wanachama 300....alipofikishwa polis alijibu jeur kuwa wawekezaji hao waende mahakamani mana anajua fika mahakamani itakuwa kesi ya madai na atalipa atakapopata....niliumia sna nilipoona mmama wa nyumbani analia akidai kuwa alichukua hela ya ada ya watoto akitegemea ndani ya miez mitatu atakuwa anapata pesa zaid n sasa watoto wanatakiwa ada n mumewe anahitaj pesa n huku alipowekeza hamna pesa yoyote ile...mmiliki wa kampuni hiyo ameenda mbali zaid baada ya kuwafanya wananchi mazezeta wachukue mkopo kwenye bank kwa kuweka dhamana ya nyumba/viwanja vyao alafu huo mkopo unaingia kwa account yake n kuenda kuwalimia mapapai wakat hamna chchte kinachofanyika mashambani mana hana hata ekari zinazozid 7 ambazo hutumia kuwaoneshea watu mwisho wa siku bank itaenda kuuza nyumba/viwanja vya wananchi...please wananchi tuamke kuepukana n utapeli huu ukiona unataka kilimo ni bora uingie mwenyewe lkn sio kutumia vikampuni hivi


Pili kuna kampuni inaitwa MAISHA BORA hawa watu wanadeal n asali ofisi zao zipo bahar beach...wao ukienda ofisini kwao watakuambia wanawateja wa asali wengi n wapo nje ya inchi n wao wanamizinga ya asali mingi ipo maeneo ya dodoma wakati hamna hata mizinga ukienda unaoneshwa mizinga ya watu wa kule n ukijiunga unanunua mizinga ya asali kuanzia laki 5 (unapata mizinga 5) n kuendelea....hawa waliwalipa watu wa mwanzo walipoanza project ili kuwavuta watu wengi zaid n walifanikiwa mana watu waliingia wengi zaid kilichotokea hamna cha malipo wala nin wametokomea hawajulikani walipo hata simu zao hazipatikani n zikipatikana hawapokei kabisa....wawekezaji walitakiwa kulipwa mwez wa sita lkn hadi sasa hawajalipwa hata cent...hawa MAISHA BORA walianzisha project nyingi sna mfano project ya mlonge,bodaboda na vicoba lkn hamna hata mradi waliowalipa wawekezaji walioingia kwenye hiyo miradi...wizara ya kilimo n ufugaji inabid iangaliye jwa jicho la tatu hivi vikampuni mana vinafilisi wananchi mno na pia tunaomba wananchi wajiepushe n hizi project zinazoonekana ni nzur n zenye pesa nyingi mara nying huwa ni matapeli

Imetolewa,
Bkas
Mgeni wa jamii forum
 
Sawa,, ujumbe umewafikia wapenda pesa za shortcall. Na nasisitiza kuwa pesa inakuja kwa kujituma na kufanya kazi. Asiyefanya kazi na asile.

Ukiona watu wanakuitia fursa za aina tajwa hapo juu,, fahamu wazi "WEWE NDO FURSA YAO"
 
Ni kweli mkuu hivi vikampuni ni shida ongeza na kingine kinaitwa MKIKITA hiki wakulima wa mhogo na papai wameliwa sana
 
Ni kweli mkuu hivi vikampuni ni shida ongeza na kingine kinaitwa MKIKITA hiki wakulima wa mhogo na papai wameliwa sana
Nimekickia hicho chief naskia hatar sna watu wameliwa mno hapo
 
Back
Top Bottom