Utapeli huu umekuwa hatari nchini

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,160
3,266
Habari zenu

Sasa hivi kumekuwa na matapeli ambao wanakupigia simu na kuomba kufanya kazi na wewe.

Hawa jamaa ni wasomi, wataalamu na pia wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kukushawishi ili ukubali kufanya nao kazi na pia kuwapa pesa.

Imegundulika kuwa mtandao wa matapeli ndani yake wapo wasomi wakubwa wa vyuo vikuu, madaktari, walimu na watu wenye nyadhifa mbali mbali katika ofisini binafsi na hata za serikali.

Pia ukumbuke kwamba kama watakuwa wameamua kukupiga pesa ndefu na kutokana na aina ya kazi waliokusomesha kufanya nao basi wajanja hawa huwatumia matapeli wenzao walioko nchi za nje kukupigia simu na namba za USA, Canada, India au nchi yeyote ili kukutengenezea mazingira mazuri ya wewe kutoa pesa.

Mara nyingi matapeli hawa hushuhulika na kazi zifuatazo.

1. Kutafutia watu kazi jeshini

2. Kujifanyana wao ni kampuni kubwa Marekani inataka kufungia branch yake Tanzania na hapa utapigiwa simu na mzungu wao alioko Marekani

3. Wanaweza kukupa dili ya kupokea watalii na kukupa dili ya kutengeneza vivutio vya watalii kama Masai Shuka, bangili.

4. Wanaweza kukupa dili ya kupokea tenda za
serikali kuhusu kilimo na hapa utapigiwa simu na anaependa kujitambulisha yeye ni Afisa Kilimo wa Rufiji

5. Watu hawa hununua vitu mbali mbali katika maduka na hapa watakueleza kuwa twende bank tukakulipe na wakati huo mshapakiza mzigo katika gari inawasubiri nje ya bank lakini wanatabia ya kupaki bank sehemu isioruhusiwa, yani wrong parking, na wanapenda sana bank za CRDB au NMB kwenye foleni kubwa, sasa akiwa kwenye foleni kubwa utaona askari anaingia na bunduki na kitangaza gari aina fulani imepaki ktk mlango wa bank tafadhali mwenye gari kasogeze, basi tapeli huyu atakuomba wewe ukae katika foleni ili yeye akasogeze gari na hapo utakaa hadi bank ifungwe yeye hutamuona tena..

6. Kwa wale kwenye kutafuta viza matapeli hawa wako huko.

7. Ukiwa umelazwa katika Hospital za rufaa na ukapewa barua ya kupelekwa nje, utashangaa utapigiwa simu na namba kutoka India na hapo wataanza kuongea Kihindi msipoelewana utaona badae anapiga mtu wa hapa anakueleza kuwa ulipigiwa simu yeyote kutoka India? Ukijibu ndio anasema yeye ni wakala wa Hospital unaotakiwa kwenda kutibiwa hivyo unaweza kufanya malipo hapa hapa, ukizubaa tu unatapeliwa na hawana hata huruma we ni mgonjwa.

8. Matapeli hawa wana mtandao wao katika internet wa vikoba ambapo wanakopesha hela kwa kutumia jina la mheshimiwa Zitto Kabwe, ukishajaza form yao utapigiwa simu ili kufanya malipo ya awali na pia watakuunganisha katika group lao LA WhatsApp ambao huko utakutana na watu wengi sana wakishukuru msaada wanaopewa na Zitto Kabwe ili kukushawishi wewe kutuma pesa za awali, ukituma tu umepigwa.

Tuwe makini sana Watanzania tusiibiwe hovyo na sambaza ujumbe huu kwani kila dakika kuna mtu anatapeliwa sehemu fulani msaidie haraka sana asitapeliwe.

Hizi ni baadhi ya namba wanazotumia kwa hapa Tanzania

0768 020 273

0788 177 313

0758 268 896

Kumbuka kwamba wakishaamua kukutapeli wana taarifa zako zote na wanakujua vizuri sana hilo lisikupe shida ukaingia mkenge.

Kwa wale ambao washatapeliwa ama wanataka kutapeliwa tafadhali toa taarifa police haraka sana.
 
toka nilivyotapeliwa kwa mara ya kwanza na ya mwisho pale ubungo mataa sitakuja kutapeliwa tena...
 
Sasa hawa matapeli wameingia mpaka misikitini,juzi tu walitaka kutapeli 200,000 tsh.za msikiti kwa kisingizio kwamba hiyo 200,000 wafungulie akaunti ya benki kwa ajili ya msikiti ili baadae wao waingize tsh.25,000,000 alafu kuna mmoja wao anaongea lafudhi ya kihindi kabisa
 
Ili usitapeliwe, kuwa makini na kila neno watakalokwambia au sentensi watakayokwambia.

Huwa tunasahau kuunganisha dots
 
Back
Top Bottom