Utapeli hatari.

New Nytemare

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
3,400
Reaction score
2,572
Kuna utapeli wasikuizi ni hatari.. Kama wiki mbili zilizopita katika gazeti la Mwananchi la tarehe 2 novemba niliona tangazo la chuo cha afya cha Eckernforde Tanga University kwa wito kwa wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya Diploma na cheti wakatoa na maelekezo jinsi ya kupata form katika internet na jinsi ya kuituma ila kabla uwe umeingiza pesa katika account yao ya CRDB...Kumbe wakati huo wametoa tangazo tayari chuo kilishakuwa kimepokea form na kimesha fanya selection na mwezi huu wa novemba waliochaguliwa ndo wanaripoti na mwisho na tarehe 15 novemba kuripoti,mie nina mdogo wangu ambaye baada ya kuona tangazo na vigezo wanavotaka anavo nikaona bora tu apply sasa majuzi katika kutaka kutuma form kwanjia ya fax nikaona ni vema kuwajulisha uongozi kwa njia ya simu kwamba natuma form kwa fax maana namba zao zilikuwepo kwenye tangazo ktk gazeti nikakutana na majibu haya "usijisumbue kutuma form kwani selection zilishatolewa kabla ya Novemba na kuripoti mwisho ni tarehe 15 yani kesho kutwa"
sasa najiuliza walitoa tangazo hili novemba 2 ili watulie pesa zetu 20,000/= na je wangapi wameliwa kama mimi..
tahadhari kwa wote
 
pole mkuu..kama risiti na ushahidi wa selection unao waburuze kwa pilato
 
Pole sana ila tabia hii kwa sasa imeenea sana hapa nchini.
Kuna watu na taasisi ambao wanapata hela nyingi sasa hivi kwa kutumia utaratibu wa ada ya fomu za maombi na mwisho wa siku utaambiwa nafasi zimejaa.
 

ndugu , hiko chuo hakitambuliki na baraza la wafamasia nchini. Usimpotezee muda mdogo wako na wala usipoteze pesa zako bue. Soma gazseti la mwananchi la leo tarehe 14 november 2012
 
Tatizo sio chuo au utapeli. Tatizo ni tangazo lao limechelewa kutoka
. Either aliyepewa kupeleka tangazo alilichelewesha au waliopewa tangazo walichelewa kulitoa
 
ndugu , hiko chuo hakitambuliki na baraza la wafamasia nchini. Usimpotezee muda mdogo wako na wala usipoteze pesa zako bue. Soma gazseti la mwananchi la leo tarehe 14 november 2012
Mkuu soma vizuri uzi wa jamaa! Nikwamba ameshaliwa!
 
mjini shule,hiyo ni njia ya kuongeza pato la chuo,huo mtindo ni wazaman,ata kama muda umeisha awatoi tangazo ili waendelee kula pesa,karibu vyuo vyote africa ufanya hivo
 
Duh kweli utapeli una category nyingi huwez jua utatapeliwa kwa style ipi.....
 
Inauma sana! Kwa utapeli au uzembe huu hatufiki....
 
msipotoa sadaka mungu atainua hata wanavyuo kutoa sadaka
 
Mbona hilo ni desde amuinto tempo watu wana piga massa oje india nao pode comfiar ninge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…