Mimi niliingiziwa pesa kwenye account ya nmb, kiasi cha shilingi millioni3.
Wakati sina habari, maana hata sms haiku-display,.
Wakatokea jamaa wawili smart sana nyumbani kwangu, wakidai wao ni wauzaji wa kiwanja, sasa wametokea kwa jamaa yangu, ni rafiki yangu ambaye walisema yuko bize na mishe zake, wameelewana naye millioni 5, kapungukiwa mill2. Hivyo kutokana na tunavyoaminiana naye,
katupia kwenye akaunti yangu mill3 ili nimkopeshe izo2 kwa sababu kiwanja hicho kilikuwa na ushindani mkubwa,watu wengi wanakitaka, lakini hawajafikia bei!
Hao jamaa nadhani walikuwa ni wataalamu wa mawasiliano, sababu nilivyoingia chumbani ili nichat na jamaa yangu kuhusu mipango yake hiyo, simu zake zote zikawa hazipatikani.
Nikaona isiwe shida, nikakomandi pesa yote iliyokuwa kwenye account ya nmb iingie crdb.
Zoezi hilo lilishindikana kwa sababu pesa waliyokuwa wameitupia tayari walikuwa wameiblock.
Hivyo ukiangalia salio, kweli kiwango hicho kipo, lakini ukitaka kukifagia, kinakataa kwamba salio halitoahelezi!
Nilichokifanya baada ya kugundua kwamba "nimetembelewa", kwanza nilikasirika na ukichukia, kuficha hasira yataka akili kuigiza furaha na bashasha usoni, nilifanya hivyo, lakini walinisoma, nadhani kwa muda niliotumia chumbani kwa tryal mbalimbali.
Kwa upole wa kuigiza huku nikifikiria haraka haraka cha kuwafanya, niliomba twende kwa jamaa yangu kwa kuwa hapatikani kwenye simu.
Hao jamaa wakasema wao hawafanyi biashara za usumbufu.
Kama sitoi hiyo pesa, basi hiyo fursa ya kupata kiwanja cha chee, jamaa yangu kakosa.
Majibu hayo yanatolewa huku wakitoka nje ya compound kwa speed.
Dah! Nifanyeje sasa?
Nilipata majibu mengi kichwani hadi ya kuua, wakati huo jamaa wameishatokomea zao.
Nilichotaka kueleza kwamba, utapeli wa kwenye mtandao ni mkubwa sana kuliko tunavyodhania, usiamini maandishi kabla ya kujiridhisha.