GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,318
unaiweka roho yangu juu juu kama mtu nayeoga nje, mpenzi yako kwako yamekuwa ya dhati kama mheshimiwa anavyompenda makonda. sijajali watu wanasema nii juu yako. kuwa hujatulia na kuwa una mambo mengi ya hovyo hovyo na hata jina lako uligushi kumbe unaitwa ashakum. nimekuwa nikiwajibu wasikubughudhi wakuache. kumbuka tumetoka mbali kama nape na ccm mwishoni unakuja kunitenda hivi?hukumbuki nlivyolala nje kwa ajili yako huku nikinyeshewa na mvua?
kila siku imekuwa kwetu ugomvi kama tundu lissu na ccm? kwa nini mama? uliniacha kwenye mateso kama lipumba alivyoondoka cuf umerudi kwangu lakini huna heri asha... unanitesa nakosa kujiamin najipendekeza na kuishi kwa matumain ukinirusha rusha kama mwakyembe anavyorushwa rushwa na serikali ya ccm ingawa najaribu kujipendekeza kwako niwezavyo.ni bora basi baada ya kuwa umemlia yule bwege pesa zake ungenyamaza tu kama dr slaa ukala maisha yako. lakin ulirudi kwangu na kunambia umejirekebisha ingawa sioni kama umejirekebisha. mamaa ulisahau nini kwangu? naulaumu moyo wangu umekuganda kama kucha kwenye kidole pamoja na maumivu yote nakomaa kama nape nnauye nikilalamika tu kwa watu.
napokuwa nawe nakuwa sina amani utadhan mtu mwenye tumbo la kuhara ukweni. nlihitaji kutulia kama mtu anayejisaidia mamaa... sina amani wakati wote. uliuvamia moyo wangu kama alivyofanya makonda clouds ukachukua mapenzi yangu na kutokomea huko. ingawa kuna mabaya uliyonitendea nashindwa kukuchamba kama gwajima. nakumezea mate tu ya huzuni ,uchungu na hasira kama membe kwa magufuli.
usiutese moyo wangu asha. unataka nijinyamazie kama alivyofanya mwigulu?nisiseme kitu hata unaponinyanyasa?mapenzi gani haya kama ccm na wabunge wake? unafiki siwez. tutulie tu mama tujilie vyetu kama marais wastaafu.
usinitese asha inatosha unataka niishi kama makonda mjini? kila wakati waswas na kupoteza amani? au unataka niwe tu boya kwako kama mawaziri flan flan?