Utandawazi usikutawale ukakosa maadili

Utandawazi usikutawale ukakosa maadili

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Hiyo ni kazi ya kizazi kisicho na maadili. Akiona mtu anaumwa sana, au akiona nyumbani kwa kikiongwe kuna watu wengi, yeye anakimbilia kwenye mtandao kutoa taarifa za kifo ili aonekane wa kwanza kutoa taarifa. Ikitokea yupo wakati mgonjwa anazidiwa au kukata roho atapiga picha na kuzisambaza fastaaaa kabla hata ya kumsitiri marehemu, akili yake ili tu awe wa kwanza kutoa taarifa na uthibitisho wa picha hata kama ni baba yake atampiga picha domo wazi ili mradi amekuwa wa kwanza kuwajuza watu.

Sasa kwa bahati mbaya ambayo ni nzuri kwake akute kuna ajali.... ataikimbilia ili awahi kupiga picha za kutuma Whatsap ... Looo salaleeeee kuna mmoja alikoswa koswa kugongwa na gari akikimbilia kupiga picha maiti wa ajali. Jamani hili janga.

Jizuieni kutoa taarifa zisizo rasmi kama hivi leo kuna mmoja alikurupuka eti Mama wa Taifa kafa. Jamani! imekuwa kero sasa. Toa taarifa rasmi, tuma picha zenye staha ambapo si lazima sana picha usitume. Ukisema fulani kafa na ukaelezea vizuri tukio zima utaeleweka.

Kuna mmoja aliambulia vibao alipotaka kupiga picha ya marehemu aliyegongwa na gari pale Mlandizi. Alikuta watu
wamemstili Marehemu kwa kumfunika na kanga yeye kwa kiherere akamfunua na kuanza kupiga picha. Nilifurahi sana walimdunda na kumsukumia huko akatahayari. Umefika muda wa kuwafunza adabu watu wa namna hii. Tumieni vizuri utandawazi.
 
Ni ulimbukeni ndo unawasumbua wabongo mkuu.
Ila kila lenye mwanzo lina mwisho,so itafika mwisho wataacha
 
Nakubaliana na ujumbe wako. ifike wakata utandawazi utumike kwa kuzingtia muongozo wa maadili.
 
Back
Top Bottom