Utamu wa Mgao wa Umeme live bila chenga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamu wa Mgao wa Umeme live bila chenga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjenda Chilo, Jul 21, 2011.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu naweka mezani experince ndogo tu ya matatizo ya mgao. suala kati ya giza na mwanga kipi bora nakiweka pembeni kwani hicho tunaelekea kukizoea.
  Kuna ka ujenzi kanafanyika, na ninatoa mfano kwa ki item kamoja tu, yaani chuma, bidhaa za chuma ni kama nondo, flat bars etc ambazo hutengenezwa viwandani. some months ago kabla ya huu mgao nondo moja ya 12mm ilikuwa haizidi TZS 12,000/=, baada ya mgao kuanza ikashoot mpaka TZS 16,000/=, jana jioni nikapita nikaambiwa imepanda yaani jana hiyohiyo inauzwa Sh. 17,500/= nikasema no sweat ngoja nikomae hivyo hivyo nikazinunue kwani inaonyesha huu mgao hauwezi kuisha leo na kahela kenyewe ka mkopo kasije kakayeyuka. Niko hapa hardware nimewasha laptop natuma msg hii baada ya kukuta si TZS 17,500/= tena ila ni TZS 18,500/=. Maana yake I cant make it. Hivi hawa jamaa hawaoni haya madhara ya wazi ambayo kila mtu anapitia??????!!!!!!!!, au kwa kuwa wao wanajengewa????!!!!! Sijasikia kauli yeyote ya maana zaidi ya kumsikia Pinda akisisitiza kumfukuza mtendaji wake ni jambo kubwa sana ambalo Mh ndo lazima alitekeleze. Kwa maneno yake hata Makamu wa Rais hana uwezo huo, ina maana hata katiba inayowapa madaraka wasimamie nchi Rais asipokuwepo nayo bado ni ngumu kuitekeleza? Tunachukulia poa ila tutapigwa makonzi na watoto wetu siku moja.
   
 2. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  mi nawasikitikia wauza samaki wabichi na wafugaji wa kuku wa kisasa ambao saa zote wanataka joto.... achilia mbali saloon...Sawmill mashine za kusaga... yaani ni umasikini full.....
   
 3. k

  kajunju JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Ni kweli vitu vimepanda bei,apa nilipo nondo mm 16 ilikuwa mwaka jana august ilikuwa sh 16 elfu, wk jana nimenunua nondo hiyo elfu 21. Kopo la rangi coral ilikuwa elfu 7 mwaka 2006 machi. Leo hii nimenunua elfu 17 kopo
   
 4. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu bado serikali haijaona na inawezekana wao wanaona short term problem ila in the long run kuna uwezekano uwaziri ukawa wa moto kwani wananchi watakuwa wana hasira na maisha yatakuwa juu na hakuna mwananchi atakubali kwenda kumpongea waziri au kiongozi yeyote wa serikali
   
 5. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa nimejua Maisha bora si Kwa kila mtanzania ni wao na wana wao tu.vumilieni wananchi,mnatak kujenga nyumba za nini wakati nitazibomoa kupisha wawekezaji hapo endeleni kupanga,nilikuwa sijailewa Siasa ya Uongozi wa Tanzania kumbe Rais ni kila kitu kumbe Pinda Pale Bungeni ni kama sanamu la kufukuza ndege shambani mwenyewe akiwa hayupo maana hat haliwezi kuwakata wala kuwapiga ndege waharibifu Kweli JK Ringa upendavyo Maana unaongoza Taifa la Wajinga watupu.
   
 6. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  viitu vinapanda bei kila siku, pakikucha unatamani ya jana.
   
 7. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Country is dying
   
 8. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Nijitoka sauz namsitaafisha JAIRO nione mnapata faida gani, wa tz kwa wivu mmezidi
   
 9. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli ina umiza sana sana hata mimi kuna kaujenzi walianza cement,juzi nikaenda nondo 13000,jana asubuhi 13500 leo 14500 duka hilo hilo,mimi inaniuma sana,nimechoka haya maisha bora kwa kila mtanzania,ngoja nkanunue zote zinazohtajika maana ikifika bei yako ntaumwa,
   
Loading...