Utamaduni wa Kujiuzulu Uongozi kwa Tuhuma Barani Afrika

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Katika duania ya kidemokrasia na ya watu wanaofuata nyao zake, tuhuma yoyote ile itakayothibitika au kutothibitika inafanya kiongozi aachie nafasi yake.

Hizi hutokea zaidi katika nafasi za uteuzi kuliko kuchaguliwa, ingawa demokrasia husimamiwa na wanaochaguliwa.

Kwa mfano, huko Marekani Mshauri wa Usalama wa Taifa, Michael Flynn amejihudhuri kushika nafasi yake baada ya kukaa ofisini kwa siku 24 tu. Hii imetokana na kutuhumiwa kufanya mawasiliano na balozi wa Urusi nchini humo.

Aidha imetokea kwa Rias wa Korea Kusini, Park Geun-hye, ametolewa ofisini kwa kashfa kumpa dili.

Inapokuja Afrika, tunaona mambo ya tofauti sana.

Watu wanaamini bila wao hakuna demokrasia na demokrasia haipo bila wao.

Nini shida ya utawala wa Afrika.
 
Mwinyi aliwahi kujiuzulu uwaziri kama sikosei, kitu adimu sana kwa bara la Afrika, kwa wale tunaoamini vitabu vya imani, vinasema uovu usitajwe kabisa kwa waaminio, lakini sasa hivi hata watu wakikamtwa na ushahidi bado wanaona ni sawa na hakuna tatizo.

Kwanini utajwe au uhusishwe na uovu, japo sio mara zote kwamba kuna ukweli lakini inaashiria kwamba kuna tatizo.

"Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu"
(Waefeso 5:3)
 
Shida ya Africa kuna umbeya mwingi sana, vinginevyo watu watakuwa wanajihuzulu kila siku bila kuwa na makosa(Lowasa, Chenge, Karamagi n.k).
 
Back
Top Bottom