Asiyekubali hili hajui soka kwamba mchezo sio dakika 90 tu huwa unachezwa kabla ya hapo. Imekuwa tabia ya CECAFA nchi inayoandaa bonanza lake kuwa bingwa na hivi sasa Kenya atachukua ndoo hiyo. Kwa utaratibu huu ndio maana Zambia, Malawi na nadhani Zimbabwe iliyokuwa inataka kujiunga zilijitoa kwenye shirikisho hili. Sijui kama wana malengo mema kwa kukuza soka kwa ukanda huu kama sio tu kutafuta pesa za kujikimu.