Utamaduni, falsafa, elimu na maendeleo

Tanganyika jeki

JF-Expert Member
Jun 12, 2011
243
87
Utamaduni huwa chanzo cha falsafa. Mfano, falsafa ya ujamaa na kujitegemea ya tanzania ilitokana na tamaduni za kibantu za usawa, haki, ushirikiano, undugu, na upendo. Na kwa uchache ikachukua mawazo ya kitamaduni za mashariki ya mbali. Falsafa hutoa mwigo wa fikra za kila jambo la kimaendelea. Elimu yetu ilifuata misingi hiyo ya ujamaa na kujitegemea. Baadhi tulilima kwenye shule za kilimo. Jkt nako ilikuwa ni sehemu kwa kujifunza ukakamavu, uzalendo na kujitegmea. Unakumbuka wazo na fikra za uwepo wa vijiji vya ujamaa, elimu na afya kwa wote. Matunda ya maendeleo yaligawanywa kwa msingi wa haki, usawa na 'equitably'. Viongozi wengi walitenda - au walilazimishwa kutenda kwa kumuogopa mwalimu J.K. Nyerere - kwa ufanisi, uzalendo na uadilifu. Chama (tanu na na ccm ya mpaka awamu ya kwanza ya mwinyi) kilitengeneza katiba inayofuata misingi ya azimio la arusha - ambalo lilikuwa mwongozo wa utekelezaji wa falsafa (mliita itikadi) ya nchi. Miiko ya viongozi wa umma (chama na selikari) ilipatikana humo. Falsafa (ambao ni mwigo mwafaka wa kufikiri) kwa wakati huo ulilenga katika: taifa kwanza, then wananchi kwa ujumla wao, halafu chama. Mitandao ya kiuongozi wakati huo haikupewa nafasi. Fikiri - na sio kuwaza - kuhusu haya. Ni upi utamaduni wetu? Ni sahihi? Nani anafluence ujenzi wa utamaduni na kwa faida ya nani? Ni ipi falsafa ya nchi? Elimu yetu ni sahihi? Nani anatengeneza mitaala yetu? Au elimu yetu ni "copy and paste" toka magharibi? Ni nini itikadi inayoendana na falsafa ya nchi? Maendeleo - kidogo tuliyonayo - yana faida kwa mtanzania? Ni endelevu? Nini msingi wa kifalsafa wa maendeleo yetu?TAIFA KWANZA
 
Back
Top Bottom