Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,560
- 3,955
Visiwa vya Zanzibar, ambavyo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vimekumbwa na mdororo mkubwa wa watalii takribani mwezi mmoja baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu uliogubikwa na matukio mbalimbali, ikiwemo maandamano na mauaji ya waandamanaji yaliyofanywa na Polisi.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, anaonekana kijana mmoja ambaye ni mwongozaji watalii (tour guide) akionyesha eneo maarufu la Zanzibar la Forodhani. Tofauti na miaka mingine ambapo kipindi hiki cha mwishoni mwa Novemba kuelekea Desemba huwa kimefurika watalii na eneo hilo kujaa, safari hii eneo hilo linaonekana kuwa tupu kabisa bila wageni.
Kijana huyo anaonekana akisema: “Leo Novemba 26 hakuna wageni. Maisha yamekuwa tafrani, pesa hakuna na wageni wamekimbia. Hatujui hata tufanye nini; kupata 10,000 sasa hivi ni ngumu. Yale mliyofanya ndiyo yamesababisha kutokea haya. Maisha ni tafrani, utalii umeharibika. Tusikubali utalii upotee, maana vijana wengi watakosa kipato kwa kuwa wengi wamejiajiri kwenye utalii.
Wakati wa maandamano, nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, Canada na Uingereza ziliwaonya raia wake kwamba Tanzania si salama kutembelea na kuwataka waliopo nchini kuchukua tahadhari zaidi za kiusalama.
Oktoba 29, 2025, siku ya Uchaguzi, wananchi, hasa vijana wanaojulikana kama Gen Z, waliandamana kupinga kile kilichoelezwa kuwa uchaguzi usio wa haki, kufuatia Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani, Tundu Lissu, kushikiliwa rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini. Malalamiko mengine yaliyosababisha maandamano kulikuwa na lawama za utekaji na upoteaji wa watu vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Polisi, ukandamizaji wa haki, ugumu wa maisha, pamoja na hali ya watoto wa viongozi kuonekana kuishi maisha ya anasa.
Katika kuwatawanya waandamanaji, Polisi walitumia mabomu ya machozi na baadaye wakatumia silaha za moto na kuanza kuua raia. Mashuhuda mbalimbali wamedai kuwa Polisi walienda hadi katika nyumba za watu ambao hawakuhusika na maandamano na kuwaua, kisha kuchukua miili na kuondoka nayo kusikojulikana, hali iliyowafanya wengi kushindwa kujua mahali walipo wapendwa wao hadi sasa.
Hakuna taarifa rasmi kuhusu idadi ya vifo, ingawa namba mbalimbali zinatajwa na wananchi wanakadiria kuwa maelfu ya watu wameuawa. Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, alipoulizwa Novemba 25, 2025 kwa nini hakuna taarifa rasmi, alisema kuwa hawawezi kuitoa ili “kulinda utu wa marehemu,” akisisitiza kwamba kilichopotea ni maisha ya watu.