mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Siku ya kwanza kutembea zanzibar(Kisiwani Unguja) nilijifunza mengi..
1:Watanzania wale kwa harakaharaka niliwaona kama watu waungwana sana sana.
2: nilitamani kuingia Verbal Contract ya kunizunusha mji mzima na bodaboda ili kupunguza ghalama na kuongeza flexibility ya safari za hapa na pale lakini kwanza sikumuona hata mmoja ingawa niliambiwa wapo, pili pikipiki nilizoziona sikuzielewa. Ikabidi nimkubalie dreva TAX aliyenivizia dakika kadhaa tu niliposhuka kwenye meli kwa juhudi aliyoionyesha na mialiko ya madereva wengine nikaona yeye anastahili hiyo tenda.
3:dereva TAX aliyenizungusha mjini ni miongoni mwa watu waliobadilisha taswira yangu kuhusu zanzibar na watu wake pia maana hana makuu, popote tulipotaka kwenda tulienda, ukimpigia simu anafika kwa wakati, Halalamiki nje ya makubaliano kama huku kwetu bara, ingawa alimlalamikia msanii mmoja maarufu wa comedy aliyekuwa ametoka kumpakia muda sio mrefu kwa ubahiri uliopitiliza. Alikuwa kama ndugu japo tulionana siku moja na kuna wakati niliacha vitu vya thamani kwenye Tax yake lakn vilibaki salama Sijui kama wote wako hivyo.
4:FORODHANI Market ile jioni ndio ilikuwa kilele cha Utalii wangu. Maana amani ilikuwa 100%, nilikutana na aina kama sita na hadi chapati za kuku, mishkaki kila aina, misosi na vitafunwa aina nyingi hadi unashindwa uanze na kipi. Pale tulichanganyika Wazungu,Wahindi,waarabu,Wachina,wakorea,watoto,watu wazima,wanawake kwa waume. Nilifika pale mida ya saa moja lakini hadi saa nne naondoka nilijihisi kanakwamba niko CATALUNIA Spain nasherekea Ushindi wa barca wa Sita Moja.Moyo umeshiba furaha.
5:Majengo mengi ya kizee, yamechakaa. Kuna hotel unaambiwa hiyo ni nzuri balaa lkn ukienda kuiona ukiilinganisha hata na Kunduchi beach hakuna inayofua dafu. Kilicho ni changa nyani wazungu kutoka nchi mbalimbali wake banana huko, nikabaki najiuliza mbona pa kawaida sana nikabaki bila jibu.
6:Nikapita na sokoni, wao wanapaita Darajani nikajichanganya na watanzania wenzangu wa visiwani pale, Nikachangia uchumi kwa kununua bidhaa ndogo ndogo pale. Ingawa usafi wa maeneo sikuufurahia, Kuna mgahawa mmoja karibu na mahala tulipopandia Meli nilikunywa juisi ambayo Utamu wake kwanza sijawahi kukutana nao mahala popote. Ila cha ajabu nilipotaka kunawa mikono ili nile na chapati,mchicha na maharage niliyokuwa nimeagiza nikapelekwa kwenda kunawa washroom. Yaani humohumo nasikia watu wanaoga, kuna sehemu ya haja kwa ndani nikashindwa kushangaa nikahisi labda ni utaratibu wao.
7: Sikusikia mtu yoyote anaongelea siasa, Ila barabarani japo uchaguzi ulikuwa umeisha muda mrefu bado niliona mabango ya chama tawala na picha za mgombea wao mabarabarani.
8:Niliingia duka moja la mzanzibar mwenye asili ya india ili angalau ninunue shati la culture ukumbusho. Tukapiga stori sana kabla ya biashara, Akanieleza kuwa yeye yuko huko toka enzi za mapinduzi na amekuwa na wakina karume. Baadae akakimbia kwenda kuswali akinikabidhi kwa dada ambaye sikujua kama ni mke au mtoto wake. Nikanunua Shati kwa bei tuliyokubaliana cha ajabu lisiti anataka tuandike pesa ndogo apunguze elfu kumi, nilijiuliza sana hawa jamaa vipi tena kukwepa kodi? Nikagundua kumbe ujanjaujanja ni tatizo la kitaifa.
Sikufaidi sana maana nilikuwa nafanya General Tourism nikiwa sina taarifa za kutosha nini ni nini, na wapi ni wapi, Niliapa kurudi wakati mwingine nikiwa nimeandaa vya kujifunza na safari hiyo itanibidi niende hadi pemba,.
Tuijue tanzania yetu wakuu. Naomba pia hints siku nikirudi tena vitu gani vizuri vya kujifunza.