Utakuwa ni mwisho ama kupunguza speed!

Utakuwa ni mwisho ama kupunguza speed!

fikikungetaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
331
Reaction score
79
Baada ya kuapishwa Rais wa awamu ya tano au baada ya Jumatano 28 October 2015 inawezekana kakupungua au kuisha kabisa kwa mambo kama vile:-

1. Chuki binafsi na Baadhi ya matusi yaliyotokana na siasa
2. Kupungua au kuacha kuingia mitandaoni kusoma habari (kwa baadhi ya watu)
3. Kupungua kununua ama kusoma magazeti mbalimbali (kwa baadhi ya watu)
4. Ndoa nyingi zitaimarika kutokana na kupunguza ubize na utofauti wa kiitikadi
5. Tabia za watu zitajirudia, kuzungumzia mapenzi masaa 24, mahali popote watakapokuwa, watu wa kila rika. Hii tabia imeota mizizi maana wengine hata wakitoka ibadani wakitawanyika wanaanza kutizama maumbile ya nyuma ya mwanamke japo wanakuwa wametoka Kumtukuza Mungu soon.
6. Rushwa inatarajiwa kuongezeka kwa kasi kubwa
7. Watu tutapendana kama zamani na kusahau kama tulikuwa tunatukanana hadharani na majukwaani kwa mbwembwe
8. Inawezekana ukali wa maisha utapungua kwa sisi tulio wengi kama tutaongeza utendaji kazi na ubunifu mara dufu
9. Tutarajie kuzungumzia mambo mengi mengine mapya ya kimaendeleo ambayo yatajitokeza siku za mbeleni
10. Natarajia kufunga ndoa mwakani, hii ni mabadiliko ya maisha yangu binafsi
11. ....

Nawasalimu wote!, huu ni mtazamo wangu tu.
 
....ndo mabadiliko kimtindo...


Natarajia kubadilika positively, zaidi ya hapo. Kwanza hii kesho kutwa itakuwa mara yangu ya kwanza kupiga kura na ni muhimu sana kwangu. Bora nikashinde kwenye foleni siku nzima
 
Back
Top Bottom