Utakaso Wa Mfumo Uozo :Kesho Yenye Neema

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,072
Wengi tunalia leo kwa Biashara zetu kuguswa,Wengi tumeguswa kwa namna moja au nyingine {Kodi,bomoa bomoa,utumbuaji,},Wengi Tunajuta kwa namna Moja au Nyingine {Kuchagua/kutokuchagua,kuchangi/,kutokuchangia,kutekeleza/kutokutekeleza,kuwajibika/kutowajibika,kuwa waadirifu/kutokuwa waadirifu...}

Ni kweli nchi yetu ina uvundo katika maeneo mengi sana sana sababu ya uozo ktk kila sekta,ziko taarifa nyingi zinazothibitishwa na viongozi waandamizi {kitaifa/kisiasa} kabisa juu ya madudu makubwa sana yaliofanywa na wengi wa waliokuwa wananchi wa kawaida {waliosomeshwa na taifa kwa manufaa ya umma} ambao sasa waitwa vigogo/mafisadi/wastaafu/wafanyabiashara maarufu..orodha ni ndefu sana si Wakurugenzi wa halmashauri,Madiwani,Mameya,Wenyeviti wa halmashauri,waweka hazina,Maafisa manunuzi,wanasheria,wakurugenzi wa taasisi/mashirika ya umma,Wafanyabiashara,Wawekezaji,wabunge,mawaziri,manaibu waziri,n.k,n.k.

Kila mmoja alijionea fahari kufanya uharibifu,kutowajibika,kutozingatia sheria;taratibu;kanuni;katiba,kuvuruga vuruga,kutenda kwa mujibu wa matakwa ya marafiki/ndugu/wapenzi/jamaa/dini/ukanda/kabila..Uchakachuaji uliota mizizi toka kwa baadhi ya viongozi waandamizi mpaka ngazi ya familia zetu {Housegirl/Houseboy mchakachuaji,mke/mme mchakachuaji,wafanyakazi wachakachuaji,baadhi ya Wanafunzi,baadhi ya walimu,baadhi ya watumishi wa Mwenyezi Mungu,watoto kwa wakubwa....

Utendaji wenye taswira ya udini,ukabila,ukanda,u yanga,u simba,u tulisoma pamoja,u jirani ,u swahiba,u rafiki,u shikaji,u uitikadi moja,ukeleketwa,n.k ni moja ya misingi iloilifikisha taifa hapa tulipo ..taifa lenye wingi wa utajiri lukuki,wataalamu lukuki,mazingira tajiri,n.k kuwa taifa maskini sana,lenye wingi wa maskini wa fikra,roho na mwili...Matajiri wachache sana {wageni,wanufaika na fulsa za upendeleo,ufisadi,wizi,uhujumu uchumi wa taifa} ambao sababu ya umaskini wa wengi nao kuwa maskini kwa namna moja au nyingine.

Misingi thabiti ikijengwa sasa kudhibiti marudio ya uozo,uharibifu,ufisadi,wizi,...hakika tunakwenda kuwa na taifa bora sana duniani..Tunayo kila sababu ya kulifanya taifa letu kuwa kubwa kiuchumi duniani..tuna kila aina ya utajiri wa miundombinu,rasilimali,uoto wa asili,upendeleo kijiografia...Taifa lililo Nuru ya Watanzania wenye njaa,maskini,walio uchi,wenye kiu, kuonewa,kudhulumiwa,kunyanyaswa,kudhalauliwa,kubezwa....

Kazi ya kulijenga taifa sio ya CCM,CHADEMA,NCCR,ACT,Mh. Magufuri,Mh.Majaliwa,Mh. Samia,Mh.Lowassa,Mh.Mbowe,Mh.Mbatia,Mh. ZItto Pekee ni kazi ya kila mmoja wetu kusikia,kushika na kutekeleza wajibu wa msingi/majukumu ya msingi,kuwajibika kwa uzalendo,kujituma,kujitolea,Kasi...

Mwenyezi Mungu Tutakase Watanzania,Mwenyezi Mungu Tubariki Watanzania,Mwenyezi Mungu Fungua Fahamu Zetu
 
Back
Top Bottom