Utajiri wa Magofu ya Rapta

Kila mara nilikuwa namwambia mtunzi asikae muda mrefu bila kutuma naona hakunielewa j[emoji848][emoji848].
Japo unabana huku ili upate watu wengi kwenye group la WhatsApp ambalo watu wanalipia 3000 mwisho wa siku ladha na hamu inapotea kabisa na unaruhusu watu waone weakness kwenye hii simulizi. Na mwisho kabisa itakosa mvuto kama mwanzo
 
Imefikia wakati sasa jamii forum iangalie namna ya kudeal na watu ambao wanatumia lugha za kuumiza hisia(psychological torture) kwa wengine. Sio kwasababu hatujui identity yako basi una uhuru sana wa kucomment chochote unachojisikia. Ifikie mahali lugha zisizo za staha ziwekewe hata button ya ku report ili ziwe deleted.
 
Mnaoona ni ya uongo acheni kusoma.
Kuna vitabu vingi sana vya ujasusi hspa bongo walikopi kwa James Chase, ila watu walivinunua na kuvisoma
Bongo movie ni kopy za Nigeria,China Hollywood Bollywood, na sasa tamthilia maarufu za korea uturuki na Italy.
Hamna Mbongo mwenye uvumbuzi wake labda ngoma za jadi na uganga vingine vyote ni copy.
Hivyo basi mtutolee upuuuuuuzi!!
 
Kwa maelezo ya fatemeh ni kwamba kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake alikua ana experience vitu vipya kwenye maungo yake. Ni kwa mara ya kwanza alihisi anahitaji mwanaume, lakini kiukweli mi sikua nimemuelewa kabisa kwanza nilitamani tuendelee na stories zilizohusu maisha yake.

Nilitamani kujua ni kwa namna gani alifanikiwa kujifunza mafunzo ya kininja, lakini pia alisoma chuo gani na course zipi zilizomfanya kuwa mtundu kiasi kile kwenye computer.

Kuna muda nilitamani sana na mimi nijue baadhi ya mambo aliyoyafanya hususani yale yaliyohusu computer. Kwani apa kibongo bongo ukiwa na kaujuzi kidogo tu ka computer basi pesa nje nje sasa ukiwa hacker si ndio balaa kabisa.

Kwa maelezo yale machache tu nilijua kuwa namchanganya sana huyu binti ninapo m hug au kum kiss, na niligundua hilo mapema kwani mara zote nilizomkiss (romance) au ata nilipo m hug alionekana kuwa mwenye hisia nyingi sana.

Yaani kuna muda alikua mpaka ana tetemeka kabisa, tukiwa bado tupo sitting room namlisha lakini na mimi pia nikiendelea kula. Nilimuomba tena aendelee kunisimulia mambo machache yaliyohusu maisha yake.

Lakini ilishindikana kuendelea na masimulizi hayo kwani aliniomba asiendelee kuongelea habari hizo akidai wakati ukifika nitajua mengi tu yanayomuhusu yeye.

Tuliendelea kupata msosi na muda huu mimi ndio niliyekuwa namlisha, asee mwanamke ni mwanamke tu haijalishi ana nguvu kiasi gani cheo au pesa kiasi gani kuna muda ata hitaji kupata treatment kama
mwanamke tu.

Wakati tunaendelea na msosi, fatemeh hakua tena mkaidi kwangu yaani nilikua nafanya chochote nachojisikia kuna muda nilimvuta vuta mashavu na alitulia tulii.

Kuna muda nilimkiss kwenye sehemu zote za usoni kuanzia kwenye paji la uso na kisha kwenye lips ila aliniangalia tu na hakusema Chochote.

Tulipomaliza msosi aliniomba akalale kwani alidai amechoka sana na viongozi wake walimpa muda mwingi wa kupumzika hivyo alitaka aitumie fursa hiyo kupumzika vyema.

Alinyanyuka na kisha Alielekea kwenye chumba chake japo alisimama kinyonge sana, ni kama mtu ambae alikua akijiuliza maswali mengi kichwani mwake.
Na mimi pia nilieelekea kwenye room yangu kwenda kuuchapa usingizi ambao nilitarajia uwe usingizi wa maana kwelikweli kutokana na uchovu wa safari yetu hiyo.

Usingizi wa siku hiyo ulikua mwingi na mzito watoto wa mjini wanasema nilikua na kama kilo tatu ya usingizi yaani usingizi wa siku tatu. Licha ya kuwa usingizini bado niliendelea kushuhudia impacts za magome yale ya mmea na matunda yale ya Camu Camu.

Niligundua impacts hizo kwani wakati nimelala nahisi kutokana na zile situation au moments nilizokua napitia na mrembo fatemeh hivyo hali ilikua mbaya sana.

Baada ya kupitiwa na usingizi nilikuja kustuka asubuhi na nje kukiwa kweupe kabisaaa nadhani kwa haraka haraka ilikua ni kama saa mbili au tatu kasoro asubuhi.

Fatemeh alikua amesha amka na muda huo alishaandaa kifungua kinywa mapema sana. Nilipotoka ndani ya chumba ambacho nililala sikua nimemuona fatemeh maeneo yale ya sitting room.

Nilichokiona ilikua ni breakfast iliyokuwa tayari imewekwa mezani na hapo ndipo niligundua kuwa fatemeh alikua amekwisha amka mapema zaidi.

( Kitu kibaya zaidi nyakati zike sikuwa na ndevu za kutosha yaani ndiyo maotea yalikua yaanaanza ila kama ningekuwa tayari na uchebe ukichanganya na kanzu nilizokua navaa toka nifike kwa fatemeh.

Mtu Yoyote angejua mi ni bonge la shekhe au mufti kabisa kwani muonekano wangu ulimshawishi yoyote kuamini nilikua Muslim.)



MIMI: miss beautiful
( Mrembooooooo)

Niliita kwa mbwembwe zote yani kama kungekua na mtu ambaye angesikia jinsi nilivyomuita ni wazi angejua mule ndani tulikua mtu na mpenzi wake.

FATEMEH: stop the noise
( Acha kelele)

Kwa sauti moja kavu sana fatemeh aliniomba niache kelele kwani hakuzoea na kama angetaka kusikia kelele. hivyo basi angeenda kutafuta apartment karibu na stendi za mabasi, Na kama sio viwanja vya mabasi au ata kwenye viwanja vya michezo.

Baada ya kusikia sauti yake nilijua alikua kwenye chumba chake na kwa upande wangu niliridhika kusikia sauti yake na kujua kama yupo nyumbani.
Nilijisogeza mpaka kwenye room yake na kuingia moja kwa moja mpaka ndani, sikutaka kuomba kuingia ndani au kubisha hodi kwani tayari niliona namudu vyema ni vile tu alikua anachelewesha kunitunuku tunda.

Nilimkuta akiwa bado kwenye night dress ambayo haikua ndefu kiivyo kitu kilichopelekea niweze kuona sehemu kubwa ya mwili wake especially na mapaja. Lakini kichwa pekee ndicho kilikua kimefunikwa kwa ustadi wa hali ya juu kwa kutumia taulo nyeupe.

Alikua ameketi kwenye mezo kubwa iliyokuwa chumbani kwake huku macho akiwa ameyaelekeza kwenye computer kubwa iliyokua kwenye chumba hicho.

Nilipoingia ndani tu cha Kwanza ilikua ni kumkumbati kwa nyuma pale alipokua amekaa na mikono nikaipeleka kifuani jambo lilionekana kumtoa kwenye reli kabisa.
FATEMEH: stop that shit...!!!! don't you see I'm busy
( Acha ujinga basi hauoni kama nipo bize)

Alilalamika kwa sauti nzuri ya kirembo, na mimi bila hiyana nikaacha nilichokua nakifanya nikaenda kukaa karibu yake kwenye kitanda.

Lakini aliniomba nikapate breakfast kwani uwepo wangu pale hawezi kufanya lolote kama nitakua hapo. Niliona ni kweli niende kupata kifungua kinywa kwani alionekana kuwa bize na alichofanya kilionekana cha msingi sana.

Lakini kwa kuwa ameshakuwa kibonde wangu sikuona kama ni sahihi kumuacha hivihivi nilimsogelea na kumdondoshea mvua za kisses. huku mkono ukiwa karibu kabisa na mapaja yake ambayo yalikuwa wazi kutokana na ile night dress kuwa fupi.

Kilichokua kina nifurahisha kwa fatemeh wakati huo yaani ukimfanyia chochote kile kwenye mwili wake alikua anaacha kila kitu na kutulia as if kuna kitu anakisikilizia kwenye mwili wake na mimi nikishakigundua hilo.

Wakati naondoka kwenye screen ya computer yake niliona sura ya mtu kama javier akiwa kwenye vazi moja matata la suti.

MIMI: is this Javier?
( Huyu sio javier kweli)

FATEMEH: yes he is
( Ndio mwenyewe)

MIMI: has he run away from haullaga?
( Ameshatoka haullag?)

Alijibu kwamba alishatoka haullaga, lakini hiyo picha ilipigwa kabla hajaenda haullaga. Kuhusu kukimbia haullaga alisema siku ileile alitoka haullaga usiku uleule ni baada ya kugundua mimi na Manuela ( fatemeh) tumeondoka na vitu vyake.

Hapa fatemeh aliniambia alichokibeba kwenye ile nylon ilikua ni ushahidi ulionyesha kuhusika kwa Javier kwenye shambulio la kigaidi la mwaka 2008. Hivyo basi ushahidi huo ulishapelekwa tayari kwenye vyombo husika tayari kwa ajili ya kuufanyia kazi.

Hapa fatemeh alidai Javier na wenzie ni miongoni mwa watu wanaojaribu ku hujumu jamuhuri hiyo ya kiislamu ya Iran. Wakishinikiza kwa namna tofauti tofauti kuondolewa kwa utawala huo na kurudishwa kwa utawala uliokuwepo enzi hizo kabla ya mpinduzi ya nchi hiyo miongo kadhaa iliyopita.


Sikutaka kusikia story nyingi kuhusu jambo hilo kwani hazikua na faida yoyote kwa upande wangu.

Niliondoka nikamuacha yeye mwenyewe lakini Wakati naondoka nilimsisitiza amtafute yule bwana aliyeitwa Shahzad ili tufanikishe lengo letu la mimi kuwepo pale.

Kwa mujibu wa fatemeh alisema ameshafanya mawasiliano tayari na huyo shahzad na tayari amempata kilichotakiwa ni mimi na yeye kuongozana mpaka eneo alilopanga kukutana na mtu huyo.

Alisisitiza nipate kifungua kinywa mapema kwani miadi ya kukutana na bwana huyo yaani shahzad ilikua ni mapema sana siku hiyo.



Baada ya kusikia taarifa hiyo nilifurahi mno nikiamini naenda kusikia habari za mji ule kutoka kwa mtu ambaye familia yake ndio Ilikua ameshikiria jambo lenyewe.

Wakati natoka ndani ya chumba kile nilitoka kwa shingo upande sana yaani nilitoka kinyonge na fatemeh alishalijua hilo. Sababu ya kutoka kinyonge ni namna ambavyo fatemeh alikuaa amekaa ndani pale.

Hakuna mwanaume angekubali kumuacha kirahisi hivyo nilikua na roho ngumu sana kuamua kuondoka ndani pale.

Wakati naondoka ata yeye alijistukia na kwenda kutafuta mavazi ambayo at least yangefunika maungo yake vizuri kama ilivyokua akifanya siku zote na hapo kabla.

Appointment yetu na Shahzad ilikua ni ndani ya maktaba ya taifa, na kwa Wakati huo huyu bwana Shahzad alikua ni miongoni au mmoja kati yaa watumishi ndani ya maktaba ile.

Hivyo basi mimi na fatemeh tulitakiwa kuelekea kwenye maktaba hiyo ili kukutana na bwana huyo aliyejulikana kwa jina la Shahzad.

MPAKA SASA TAYARI NIMESHAJIBU MASWALI KADHAA AMBAYO TULIJIULIZA HAPO AWALI KWENYE PROLOGUE.

Maswali yaliyojibiwa ni pamoja na:-

Niliwezaje kufika Colombia Peru kisha Iran na miji mingine mikubwa duniani mfano Dubai?



Swali lingine la msingi, wageni wa kwanza wa pwani ya Africa mashariki walikua ni warumi na wachina kabla ya waarabu na waajemi,

sasa imekuaje details za rapta zilizoandaliwa na warumi zikafika Iran(Persiangulf)zilifikaje huko?

Je wanafahamu kua details hizo zinazohusu rapta kabla ya kuwafikia wengi tunajua kama zilishatumiwa na waajemi wa kale Na kuna uwezekano taarifa hizo zilichakachuliwa!?

Simulizi yetu inaenda kwa namna ya kujibu maswali yale yote yaliyopo mwanzoni kabisa kwenye dibaji ya simulizi.


NILIAHIDI SIMULIZI ITAISHA HAPA, HUU UKIMYA UNATOKANA NA SAFARI NILIKUA NJIANI NAELEKEA BUJUMBURA NIMEFIKA LEO.







Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
TUNAENDELEA JAMANI TUSIWAKATISHE TAMAA WENYE MOYO WA KUSOMA

Nilichangamkia ile breakfast sikutaka kupoteza muda tena baada ya kujua kwamba nikitoka hapo natakiwa kwenda kuonana na Shahzad. Wakati naendelea alikuja pia fatemeh akajiunga na mimi kwenye ile breakfast.

Baada ya story za hapa na pale Nilikua wa kwanza kunyanyuka kwenye ile dinning table na kiukweli nilimshukuru pamoja na kumsifia sana mpishi kwa kile alichokifanya. Kuna vitu nilikula na sikujua ni vitu gani ila kikubwa nilichokijua kwenye ule mchanganyo ni unga wa ngano pekee.

Nilipo nyanyuka kwenye ile meza ya chakula nilikimbilia kwenye room yangu kwenda kubadili nguo. lakini kabla sijabadili niliona ngoja nimzingue kibonde wangu fatemeh kwakua mpaka wakati huo nilisha amini ya kuwa nammudu tena sana.


MIMI: fet
( Nilimuita jina lake lakini kwa kifupi, na ilionekana kwake sio jina geni au haikua mara ya kwanza kuitwa kwa ufupisho kama hivyo)

Nilimuita kwa saut ya wastani sana lakini ilisikika vyema sana kutokea chumbani mpaka pale dinning alipokuwepo.

FATEMEH: what the matter?
( Kuna nini?)

Kiuhalisia ni kweli nilikua na makelele sana toka nifike kwenye nyumba hiyo, lakini kelele zangu zilikua ni sehemu ya faraja kwa fatemeh kwani alijiona kabisa kama tayari ana familia.

MIMI: may you please come this way
( Unaweza kuja huku mara moja)

FATEMEH: what the hell you want me to do there ?
( Unataka nije kufanya nini huko)

MIMI: I want you to choose clothes for me
( Nataka unichagulie nguo za kuvaa)

FATEMEH: worry out, you will come out naked since no one knows you.
( Usijali utatoka ata uchi kwanza anakujua nani huku)

Baada ya kauli ile ya fatemeh nilijua tu hakua tayari hivyo nilijipigilia t-shirt na jeans kama ilivyokua wakati natokea cero de Pasco kuelekea Lima.

Nilipotokeza tena mbele ya fatemeh ambaye yeye alikua tayari ameshajiandaa kwa safari aliuliza swali moja tu.

FATEMEH: why don't you wear a............

( Kwanini usivae .......)
Kabla hajamalizia sentensi yake nilimuwahi kwa kumziba mdogo asimalizie alichotaka kuongea kwani nilijua alitaka kuuliza kwanini nisivae kanzu.

Pale pale nilirudisha tena swali kwake,
MIMI: i told you to ..........
( Nilikwambia u......)

Na yeye aliniziba mdomo kwa haraka kwani alijua nataka kumwambia nini, na ni kweli nilichotaka kumwambia ni kuwa nilimuita aje kunichagulia nguo lakini aka leta pozi.


Unajua unapotaka kutoka na mwanamke kwa mara ya kwanza yaani apa na maanisha kama mnahitaji kuongozana, mpe yeye uhuru wa kukuchagulia nguo

Hii itamfanya awe huru na Amani sana kwenye matembezi yenu kwani hawa wenzetu wanajali sana muonekano especially wa mavazi pindi wanapokua wametoka na wenzao.

Mwingine anaweza asikwambie Lakini kama hajafurahishwa na code zako za siku hiyo unaweza kushangaa mwenzio kanuna barabara nzima na hamna sababu ya msingi.

Hiyo yote ni kwakua wanaume tunajali kuvaa lakini hatujali tumevaa nini, ndio maana asilimia karibia 85 % ya wanaume huwa hatabadili boxa bila kuinusa kwanza hahahahaha haha jokes.

Once you find that the shit is smell nice hiyo niaje itavaliwa week nzima.

Turudi zetu kwenye simulizi hao walikua ni wadhamini lakini natumaini tumejifunza kitu hapo.

Yaan mkiwa mnatoka na mwanamke lazima atakuwa serious kuangalia unavaaje kabla hata yeye hajavaa hii ikimaanisha wao hawakosei kwenye mavazi ila sisi ndio huwa hatuchelewi kuchana mikeka.

Kile kitendo cha kuzibana midomo kilitufanya wote kwa pamoja tucheke kwani kila mtu alikua ana jaribu kujilinda au kujitetea kutokana na alipokua amekosea.

Leo kwa mara ya kwanza nilishuhudia tabasamu zuri la bidada fatemeh, hakika alikua mrembo sana kwani sikuwahi kumuona akicheka kicheko cha kutoa sauti na kilichotokea moyoni.

Siku hiyo ndio ilikua mara ya kwanza kumuona akiwa kwenye tabasamu zito namna hiyo na alipendeza kiukweli.

MIMI: fet
( Nilimuita kwa upole sana)

FATEMEH: what's up boy
( Niambie mshkaji wangu)

Tena this time aliitikia kirafiki sana uku uso ukiwa umejaa tabasamu la nguvu

MIMI: you are gifted with beauty
( Umejaaliwa uzuri)

Kama ilivyoada mwanamke akisifiwa hufurahi zaidi, hivyo basi alishukuru kwa kumsifia lakini pia alitanguliza shukran zake kwangu. Alishukuru kwa kampani ambayo nimekua nikimpa kwa siku hizo mbili tatu kwani amejihisi wa tofauti na amekua na amani sana alitumia neno peace of mind.

Baada ya maneno mawili matatu nilimsogelea na yeye alijua kinachofuata, na akanipiga chenga ya mwili kwani alijua tu kinachofata ni romances na fujo nyingine hivyo alinikimbia kwa staili hiyo.

Yaani mpaka hapo mimi na yeye hatukuelewa tulikua wapenzi au vipi, lakini pia fatemeh bado alikua ana nikwepa sana na ilionekana wazi hakua tayari mimi nimu undress.

Ila alichonifurahisha hakua mkali hivyo ikitokea nimemuotea alikua hana ujanja alikua anatulia anasikilizia radha ya romance au touches zangu.


Kwenye akili yangu niliamini ipo siku nitamtaiti na atatoa tunda kimasihala tu wala sitatumia nguvu kwani hatua tuliyofikia ilikua inaleta matumaini.

Jambo la kuchekesha ambalo lilinifurahisha, ni kwamba fatemeh baada ya kunipiga chenga ya mwili na kunikimbia alienda kusimama mlangoni kwa mbaali na kunisisitiza kuwa tunatakiwa tuwahi Kwani Shahzad alikua anatusubiri sisi.

Binafsi nilifurahi pia kumuona binti huyo yupo kwenye nyakati za furaha kama ambavyo nilimuona Wakati huo. Kwani alionekana hapo awali hauwahi kuwa mwenye furaha na amani kama anayoipata wakati huo baada ya kukutana na chalii ya kaskazini.

Nilimuomba anipe dakika moja tu kuna jambo nikalifanye lakini hakukua na lolote zaidi nilienda kula kanzu tena nilitupia na kilemba juu kama mujahideen ( mujahidina).

Zote hizo zilikua ni mbinu na namna za kuhakikisha mrembo anakua na amani lakini pia na confidence zaidi kwenye matembezi yetu.

Kwani niligundua ndani ya jiji hilo karibia asilimia 98 ya wanaume wanakua wamevaa kanzu au mavazi yale ya tamaduni za kiarabu. Kukuta mjuba aliyevaa tshirts na jeans ni nadra sana ndani ya mji huo, na ni kweli baada ya kutokelezea na zile pigo za kijahidina nilimuona fatemeh kama furaha iliongezeka.

Tukiwa ndani ya lifti tunaelekea floor ya chini, huyu mwana mama alianza kunipanga sasa namna ya kuishi tunapotoka ndani ya apartment ile.

" Najua umenizoea sana, na mimi pia sitaki kuwa muongo nimekuzoea ila nakuomba huku nje tunapoenda jaribu kuweka umbali na mimi"
Watu wanavyo ni treat mimi nikiwa huku nje ni tofauti sana na wewe unavyo ni treat.

Hivyo basi naomba uniheshimu sana tena sana", na wakati anaongea maneno haya alikua serious sana

Alimalizia kwa kusema:-
FATEMEH: we are in Islamic state where shari'a rules applied in each and every corner of the state.
( Tupo kwenye nchi ya kiislamu ambapo shari'a zinafanya kazi kila sehemu)

FATEMEH: We don't have to show if we are lovers
( Hatutakiwi kuonyesha kama sisi ni wapenzi)

MIMI: i didn't know if we were lovers, and I'm not going to sleep alone tonight
( Sikua najua kama sisi mi wapenzi sasa kwa taarifa yako leo silali peke yangu)

Kabla hajajibu chochote lift ilisimama tukiwa floor ya chini yaani ground floor ile tunatoka tu tulikutana na mashekhe wawili, ambao Salam yao ya kwanza ilikua ni asalaam aleykum.

Nilijibu lakini jamaa hawakuridhika na namna nilivyojibu waliniangalia tu nadhani kimoyomoyo walisema hapa hamna shekhe au ndio wale mashekhe ubwabwa au mashekhe wa mchongo.

Tulipotoka nje tulikuta gari ile ile ambayo ilikuja kutuchukua airport, ilikua Toyota hiace nyeusi hivyo ata kabla sijaambiwa ndiyo gari tunayoenda kupanda mimi mwenyewe niliongoza kuelekea ilipo kuwa imepark gari ile.


Tukiwa ndani nilijaribu kuwa mpole na kufuata taratibu zote kama nilivyoelekezwa na fatemeh kuhusu ni namna gani natakiwa ku behave.
MIMI: do you know the driver of this car?
( Unamjua dereva wa hili gari)

Niliuliza hivyo kwakua toka siku ya kwanza Tunapanda gari hiyo sikubahatika kumuona wala kusikia sauti yake sasa nilitamani kujua ni utaratibu gani huo wanautumiaga.

Lakini kutokana na ukimya wa fatemeh nilijua tu kuwa hayupo tayari kujibu swali lile either lilikua la kijinga kwake au liligusa maadili ya kazi yake.

Kwani mpaka hapo niligundua hakua tayari kujibu maswali yote yaliyohusu taaluma au maadili ya kazi yake hiyo.

Kwa speed ya kuridhisha sana tulikamata highway moja ambayo niliambiwa iliitwa Haghani Expressway na kwa umbali uliotuchukua dakika chache tu tukisimama mbele ya jengo lililojulikana kama, National Library And archives of Iran (NLAI) na pembeni pia kulikua na jengo lingine kubwa lililosomeka kama Central Bank of Iran.

Kwa waliosoma history wakisikia neno ARCHIVES linaweza lisiwe geni kwao kabisa, kwani wamekutana nalo mara kadhaa kwenye scenario tofauti tofauti.

lakini niseme tu archive kwa wasiojua ni jengo au sehemu ambapo zinahifadhiwa documents zote za kihistoria inaweza kuwa history ya sehemu, watu au jamii nzima kwa ujumla.

Sasa basi kwa mujibu fatemeh ni kwamba tulikua tunaenda kukutana na shahzad ndani ya jengo hilo ambalo lilikua ni maktaba kuu ya nchi hiyo lakini pia archive ilikua ndani yake.


Tulishuka ndani ya ile gari yetu ambayo sijawahi kumuona dereva wetu kabisa toka nianze kuipanda ile siku ya kwanza na leo ni siku ya pili.

Tukiwa tunaingia ndani ya jengo hilo ambalo lilikua ndio maktaba yenyewe fatemeh aliniambia amemiss sana shule na aliongea hivyo baada ya kukatisha eneo moja na kuona watu waliokuwa na utulivu mkubwa na ni wazi walikua wanafunzi wale.

Lakini Wakati anaongea vile aliamini na mimi nitajibu kama nimemiss shule lakini haikua hivyo nilipiga kimya yaani kwa dalili zile alijua kabisa kama nachukia shule.


Kwa maelezo ya fatemeh ni kwamba shule au college ya mwisho kuhudhuria ilikua inapatikana nchini Russia. Na alitamani kuendelea kujifunza mambo mengi lakini serikali ya nchi yake yaani Iran chini ya idara yao nyeti ya MOIS walimuhitaji ili kuendelea na majukumu.

Hakutaka kusema jina la college iliyo attend akiwa nchini humo lakini alienda huko akiwa tayari ni graduate wa mambo ya information technology yaani IT.

Kwa haraka haraka kwenye maelezo yale machache ni kwamba fatemeh alihudumu pia kama Ethical hacker au jina lingine wanaitwa white-hat hackers.

Baadae tutaelezana nani ni white- hat hacker nani ni black-hat hucker na nani ni grey- hat hucker kwa mujibu wa fatemeh ambae alionekana kuwa tegemeo kwenye nyanja hiyo ya udukuaji wa mifumo ya kikompyuta.

Bila kusahau kuna hawa wengine ambao wapo sana kwenye nchi zetu especially Nigeria na South Africa ambao jina lao maarufu huitwa script kiddie na wenyewe tutawachambua kidogo.

KULE WHATSAPP HIZI SIKU MBILI TATU PIA NIMETUMA VIPANDE VIFUPI NA KWA KUCHELEWA SANA MTANISAMEHE SANA.

(0623329512 Whatsapp only) kwa kupata muendelezo,je!! Ni kweli leo inaenda kuwa siku ya mwisho kukutana na shahzad kisha nitimkie rapta? Tukutane baadae

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hawa watu hawakosekani,

mi kawaida nazisoma tu alafu naachana nazo, Cha ajabu mtu ameikataa simulizi toka siku ya kwanza lakini kila siku yupo nikiweka kipande anasoma anaendelea na comments za kuipinga.

Apo awali nilishasema sababu ya kuchukua ef 3 ni kujiweka committed na kuandika maana nitakuwa kama nina deni la uandishi. Bila hivyo ningekua natuma kwa week ata mara moja tu lakini kwa sasa nalazimika kuandika kila siku kwa maana nimechukua pesa ya watu zaidi 300's.

Tuendelee kusoma simulizi inamengi sana ya kuyajua, lakini ukiona ina utoto mwingi nashauri Usipoteze muda wako achana nayo tu.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Jf kuna watu wana mpunga wa maana mzew wacha kabsa. Ingekuta hizi Ids zinaongea watu wangeogopana sana hapa.
 
Jf kuna watu wana mpunga wa maana mzew wacha kabsa. Ingekuta hizi Ids zinaongea watu wangeogopana sana hapa.
Alaf kuna akina sie ambao ugonjwa wa 50k tu inabid ukoo mzima ukae kikao ili kujadili namna ya kusaidia


Kiukwel upo sahih hiz id's zingekuwa zinaongea ingekua balaaaa
 
Hizi picha kapiga msimuzili hadi aseme zisisambazwe 😆😆😆
 
Hizi pichq kapiga msimuzili hadi aseme zisisambazwe [emoji38][emoji38][emoji38]
Chief apa nilikua namaanisha picha za mashambani na baadhi ya picha za mabaki ya mji ( chini ya bahari). Picha hizo zitawekwa kwenye kitabu baada ya kupitiwa na wataalamu,

Asante kwa kunikumbusha

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Kama umepita KZ Camp na SunLG zilikuwepo we ni kinda hata Dumba pengine humkuta, au Warioba pale Kizuka Sec
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…