sitaki hayo mambo ya kwenda kwa mganga kuna jamaa yuko uku mwanza ana ela ila mguu mmoja ni mnene alafu una madonda makubwa yani dah inasikitisha...na ukiona mtu anaenda kwa mganga ujue kwaishiwa maarifa kichwani...
Inawahusu hasa wale wenzetu wa kutoka wilaya ya Makete. Yaani Wakinga. Full mazingaombwe
Umekariri ... Siri ya utajiri ni ubahili. !Inawahusu hasa wale wenzetu wa kutoka wilaya ya Makete. Yaani Wakinga. Full mazingaombwe
Bonge moja la topic. Me mtaan kwe2 kuna jamaa mmoja mmeru bac ameua ndugu zake wote (sacrifice) na juzi juzi mwezi wa pili kammalizia maza ake, at the first ckuelewa coz umri ulikuwa haujachanganua mambo wakat napewa hizi story! Miaka minne iliyopita na sasa hivi ndo nikaelewa kinachoongelewa, yaan kila akiuwa anaandika jina mali ( mfano akinunua fuso anaandika jina la ndugu yake aliyekufa) maza ake kafa juzi amenunua mjengo wenye ghorofa mbili kauandika jina la mama ake! Masharti nuksi!
Utajiri una madaraja na kila daraja lina kafara lake mfano
Milioni 20-50 ni tofauti na milioni 100-200 na kila daraja huhitaji kitu kikubwa zaidi au damu nyingi zaidi
Inawahusu hasa wale wenzetu wa kutoka wilaya ya Makete. Yaani Wakinga. Full mazingaombwe
hao mbona tayari ni matajiri?Hata hili wimbi la kupotea kwa watoto lina uhusiano mkubwa na hawa watafuta madaraka hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu
acha kulisha watu ujinga wewe!!
Hata hili wimbi la kupotea kwa watoto lina uhusiano mkubwa na hawa watafuta madaraka hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu
Ukisikia paa ujue kuna mtu limempata. nina hakika hii post ya Mshana imekushika pabayaboss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.
mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.