Pastor Silla
Senior Member
- Sep 22, 2020
- 162
- 166
Mmmh kumbe!Utajiri ni jinsi akili yako inavokutuma kuwajibika.
Askofu wa madini Arusha na kanumbaHakuna utajiri wa namna hiyo.
Kwa Mungu Hakuna matesoNi udhibitisho gani unautoa kwamba huko unapotaka au kulazmisha watu waingie ndiko hakuna mateso...
Dini ni imani.Matendo ni mtu binafsiDini ndio zinafuga wachawi wanaoharibu maisha ya watu na mtu anapoharibiwa maisha ndo anajikuta anafanya mambo ya aina hiyo.
Kimsingi ukienda kwenye nyumba yeyote ya ibada kuna wachawi wengi kuliko mtaani hao walio na utajiri wa majini, nashangaa hata viongozi wa Dini wanatimba kwa waganga wa kienyeji.
Chanzo cha hayo uloleta humu ni Dini...
Kama Imani inashindwa kuondoa uchafu (uchawi) na inazidi kuulea na kuukuza huo uchafu, unafikiri inamsaada gani?Dini ni imani.Matendo ni mtu binafsi
Kwa Mungu Jehovah ni utajiri wa raha unainjoi na ndugu zako utajiri wako Pasipokuteseka wala masharti mfano mfanye msukule kisha mlawiti mama,baba, mtoto wako Ili kumfurahisha shetani Ili akupe mali,akikinai ukutoa kafara anywe damu yako.Kwa mungu ni wapi?!
Kuna imani mbili ya Mungu na ya shetani ya Mungu haishindwi.Kama Imani inashindwa kuondoa uchafu (uchawi) na inazidi kuulea na kuukuza huo uchafu, unafikiri inamsaada gani?
Sijakataa Mungu hashindwi, ila nioneshe hata Kanisa moja ambalo vipofu wanaona, viwete wanatembea, nk maana hizo ndo kazi zinatakiwa kuonekana katika nyumba za Mungu wa kweli...Kuna imani mbili ya Mungu na ya shetani ya Mungu haishindwi.
Waliopata ulemavu na upofu,magonjwa kwa kulogwa wanapona.Waliozaliwa kwa mapenzi ya Mungu Mungu kaweka kusudi.Sijakataa Mungu hashindwi, ila nioneshe hata Kanisa moja ambalo vipofu wanaona, viwete wanatembea, nk maana hizo ndo kazi zinatakiwa kuonekana katika nyumba za Mungu wa kweli...
Ndio sababu nimesema Imani kwa nyakati hizi, zinalea uovu...
Ni imani potofu na mawazo ya kimaskini yaliyokubuhu. Juhudi na maarifa ndiyo njia pekee ya kufikia malengo yako ya utajiri.Nyakati za Sasa dunia pamoja na nchi yetu ya Tanzania imekumbwa na roho chafu ya kutafuta au kupenda mali au utajiri wa kichawi na kishirikina.
Watu waliowengi wapo tayari kuua au kumiliki majini na kutia kafara mbalimbali za damu kwa Shetani ilimradi wapate pesa ,mali na utajiri.
Wapo ambao wanashirikina tendo na Mama zao wazazi,wapo waliowafanya watoto wao mazombi na wapo wengine wanaingiliwa kinyume na maumbile na wapo ambao hawazai au jogoo hapandi mtungi na hana mtoto;wengine wamefunga mizukule kwenye vyumba maalum kwenye nyumba zao.
Ukifanya tafiti utakuta mara nyingi utajiri wowote unaopatikana kutoka kwa Shetani uwa una majuto mengi Sana na uwa haudumu kama utajiri utokao kwa Mungu;pia matajiri hao wakifilisika ushia kuwa masikini wa kutupa .
Neno la Mungu linasema utajiri na heshima upo kwa Bwana.Pia kwenye Mithali inasema "Baraka za Mungu hazina huzuni ndani yake" tofauti na za Shetani zimejaa huzuni nyingi ndani yake ikiwemo kuteseka kwa kafara,kutokwa vidonda ndugu,kujamiana na Mama mzazi ,kutolala usiku na kuua mke au mtoto wako umpendae.
Zingatia;Kataa kuvutwa na utajiri wa kipepo au kishetani utakutesa Sana.Yupo Yesu kwa ajili yako ukimwamini atakusaidia mqamini na fanya kazi kwa bidii utafanikiwa.Hacha tamaa maana tamaa ilisababisha fisi kukosa vyote maana utajiri wa kishetani ukukosesha furaha na amani pia utaishia Jehanamu.
Mithali 3:5-6 inasema vyema Sana kwamba"Mtumaini Bwana kwa kila Jambo Wala usitegemee akili yako peke yako na katika njia zako mkiri yeye naye atanyoosha mapito yako.Kumbuka utajiri na heshima vipo kwa Bwana na si kwa Shetani.
KATAA UTAJIRI WA KICHAWI NA KISHIRIKINA.JENGA MAHUSIANO NA MUNGU NA FANYA KAZI KWA BIDII.
Pastor Silla.
Akitafuta atapataAmesema umuoneshe kanisa ambalo vipofu wanaona, viwete wanatembea, maskin wanakua matajiri