Utajiri wa Diamond Platinumz wafikia Billion 8.6 za Kitanzania

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
 
Hard work pay.......
94d493d80f908625d249a5d94c33d3ca.jpg
 
ukisikia maneno ya mkosaji ndo haya sasa,na ukisikia mtu ana roho ya korosho ndo kama hii,na ukisikia mtu anaumia kumoyo ndokama hivi.........mi nakuomba muulize kwanza mengi na bakhresa hilo swali afu diamond atakujibu vizuri tu..

Halafu we bwana post zako ni za kitoto sana
Mwenzako ameuliza pato la taifa limeongezekaje hapo??
We unasema awaulize mengi na bakhresa
Ninyi ndo mnaofanya wakenya wazidi kuja kuwatawala hapo hapo kwenu
 
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
It's a good start, ingependeza tukapata kiwango ajira zinazoweza kupatikana kutokana na utajiri wake, asiishie kununua mashamba na meno ya dhahabu.
 
Huo utajiri una manufaa gani kwenye nchi iliyo top five ya nchi maskini duniani????
nawew kumbe liongo nchi maskini kumi hizi apa

Gross domestic product (GDP) based on purchasing-power-parity (PPP) per capita.
Values are expressed in current international dollars, reflecting a single year's (the current year) currency exchange rates and PPP adjustments.
Ranking Country
2015 International Dollars
1 Central African Republic 639.937
2 Congo, Dem. Rep. 753.907
3 Malawi 819.688
4 Liberia 934.095
5 Burundi 951.098
6 Niger 1,069.59
7 Mozambique 1,208.61
8 Eritrea 1,210.15
9 Guinea 1,388.74
10 Madagascar 1,477.78
 
Back
Top Bottom