Utajiri na umasikini vinaanzia rohoni

Utajiri na umasikini vinaanzia rohoni

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Utajiri na umasikini vyote vinaanzia kwenye mawazo. Matajiri huamini kwenye wingi. Na masikini huamini kwenye uhaba.

Kuna madaraja matatu hadi manne ya viwango vya pesa na mali.

Kuna daraja la kwanza ambalo lina watu wengi. Hawa huamka asubuhi kwenda kazini, kwenye ajira, kujiajiri nk.

Kundi wakipata pesa ambayo ni mbegu ya kupanda wao huitafuna yote.

Kundi la pili ni wale ambao wanapopata pesa yao huweka akiba kama njia ya kukusanya mtaji biashara au kuwekeza.

Kundi hili ni gumu ukilinganisha na hilo la kwanza . Kwa sababu tunaona kazi siyo kutengeneza pesa bali kwa wengi tatizo liko kwenye kuitunza kile ambacho tayari wanacho.

Kundi la tatu ni kundi gumu kuliko hayo yaliyotangilia. Kwa sababu kundi hili linakuwa limeshavuka kwenye kutengeneza, kuweka akiba. Sasa inatakiwa Ile pesa aliyoitunza au kuikuza kupitia biashara aitumie kwenye uwekezaji.

Hapa tunazungumzia Hisa, hatifungani , Mali Isiyohamishika nk.

Huku kunahitaji mtu mwenye ujuzi na maarifa. Mtu mwenye maono makubwa na mwenye uwezo wa kujenga mifumo ambayo itafanya pesa aliyonayo imfanyie kazi.

Kundi la nne ndiyo hilo la ukwasi. Hawa ndiyo ambao tunaambiwa hawatengenezi tena pesa wao wanazivita pesa.

Pesa inawatafuta wao. Wanaweza kununu biashara za wengine na kuweka mifumo Yao. Hawa wanaotumia pesa za wengine kuelendela zaidi.

Watu wanawaamini wanawekeza kwake. Na hivyo wanakuwa na ukwasi mkubwa.

Masikini waliokuwa wengi hubakia kwenye mbio za panya. Wanatafuta, wanakula wanaendelea tena kutafuta.

Hawa hawapandi daraja. Kwa hiyo hata ukiwagawia pesa Bado watarudia mchezo wao WA kula na kutafuta tena

MATAJIRI WOTE WAKIPOKONYWA UTAJIRI WAO WAPEWE MASIKINI BAADA YA MDA MASIKINI WATAKUWA MASIKINI NA MATAJIRI WATAKUWA MATAJIRI

Huo usemi ni sawa na kusema Waafrika kuhamia Ulaya Wazungu wakahamia Afrika , bado Waafrika watakuwa maskini.
Utajiri uko NDANI ya mtu Mwenyewe hautoki nje. Kinachomuongoza mtu kinaanzia NDANI yake Kwa jinsi anavyojitambua. Utajiri ni : ni Maarija na ujuzi, utajiri ni Roho , wakolon walipoondoka waliacha viwanda vingi tu vikiendeleea na uzarishaji, havikuchukua time vyote vilifungwa. Hata familia ambazo Baba ndo Mwenye maarifa ya utaftaji peke ake akifa na Mali zote hufa
 
Mada kama hizi huwa hazina wachangiaji maana zinaumiza kwa ukweli na wabongo hatupendi kuambiwa ukweli.
 
Back
Top Bottom