Utafiti wangu kuhusu Ukuaji wa Mtoto (Child Development)

Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,474
1,079
Napenda kusalimia GT wote ndani ya jukwaa hili, ambapo tunapata fursa kujadili masuala mbalimbali. Katika kipindi cha Miezi 6 iliyopita, kuanzia July-December 2016. Nimekuwa nikifanya uchunguzi wa makuzi ya mtoto wangu ili niweze kugundua hatua za ukuaji wake na mabadiliko ya tabia.

Nitaeleza kwa ujumla mpaka sasa nimegundua nini;

i. Mtoto wa miezi 5/6 anakuwa ameanza kujenga hisia, mfano furaha, huzuni, Ukali. Mfano. Katika uchunguzi wa hisia ya huzuni/huruma nilimchukua mtoto video clip ya Dk. 1.30 akiwa analia akiwa na miezi 4, baada ya miezi 2 baadaye nilimuonyesha video ile wakati akiwa katika hali ya furaha lakini baada ya kumuonyesha video ile kwa wakati ule zaidi ya Mara tatu alianza kutoa machozi, na baadaye akaanza kulia kwa hisia ndipo nilipotambua kwamba watoto katika umri huo wanaweza kukabiliana na hisia zote tatu alizonazo binadamu aliyekamilika.

Kucheka na kukasirika ni hisia rahisi kwa mtoto kwa sababu endapo akifurahishwa ni rahisi kucheka na endapo atakasirishwa au kukosa hitaji lake basi ni rahisi pia kukasirika tofauti na hisia ya huruma/hatari ambayo inahitaji kuchunguzwa.

ii. Katika kipindi cha miezi 5/6 mtoto huwa na uwezo wa kutambua watu wa karibu kwa sauti na sura, mfano: katika uchunguzi wa mtoto huyu mama yake alipokuwa akiingia chumbani akiwa anaongea mtoto alianza kulia akimaanisha kumsikia au kumhitaji mama hata kama alikuwa ametulia. Kwa upande wa sura mtoto aliweza kufurahi sana pale alipoenda kushikwa na mama yake.

Nitaendelea wakati mwingine, mnakaribishwa kwa maoni na ushauri!!

NB: Makuzi ya watoto yanatofautiana baina ya mtoto na mtoto.
 
Mkuu wa kwangu ana miez 5 sasa hivi ntamchunguza then ntarudi kwa mrejesho.ila naamini humu kuna waatalamu wa pyschology waje kutupa somo kwa undani zaidi
 
Mkuu wa kwangu ana miez 5 sasa hivi ntamchunguza then ntarudi kwa mrejesho.ila naamini humu kuna waatalamu wa pyschology waje kutupa somo kwa undani zaidi
Fanya kama nilivyofanya mkuu then tupeane mrejesho
 
Back
Top Bottom