Utafiti Mpya: Magufuli asilimia 89, Jakaya wa Pili, Lowassa umaarufu washuka

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Lubuva-Ripoti.JPG

Katika ripoti ya utafiti uliotolewa leo na gazeti la Habari Leo na Majira, inaonyesha Rais Magufuli kwa sasa anakubalika kwa asilimia 89, Jakaya Kikwete umaarufu umepanda na Lowassa kashuka zaidi...

Hii ni kiashiria kwamba uchaguzi ukifanyika leo Dr. Magufuli atashinda kwa zaidi ya asilimia 89.

Mytake: Hali ikiwa hivi, na kule upande mwingine Dr. Tulia akizidi kukaza nakiona rasmi kifo cha upinzani by 2020

======

Utafiti uliofanywa na Taasisi Huru ya Kijamii ya CZI katika mikoa 15 nchini kuhusu utendaji kazi wa Rais John Magufuli, umebaini kuwa rais anakubalika kwa wananchi kwa asilimia 89 tangu aingie madarakani.

Hayo yamo kwenye taarifa ya matokeo ya utafiti uliofanywa Tanzania Bara na Visiwani, kuangalia utendaji kazi wa rais kwa miezi minane tangu aingie madarakani; anaripoti Ikunda Eric.

Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, jopo la watafiti hao likiongozwa na mwanadiplomasia kijana Dotto Nyirenda, walisema walihoji makundi matatu ya watu.

Nyirenda alisema kwa ujumla rais anakubalika kwenye jamii kwa asilimia 89 na hiyo inatokana na majibu ya utafiti huo kutoka makundi matatu yaliyohojiwa. Kundi la kwanza lililohojiwa ni vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 18 ambalo lilisema wanaamini Rais Magufuli ataleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kurejesha nidhamu ya masomo shuleni.

Nyirenda alisema kundi hilo linaamini kwa asilimia 78 utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba ataleta mageuzi kwenye elimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la madawati, mitaala na kurudisha nidhamu ya walimu.

Hata hivyo, katika kundi hilo asilimia 22 wanaona huenda rais asifanikiwe kwenye sekta ya elimu na pia kuondolewa kwa michezo shuleni kutadidimiza maendeleo ya michezo nchini.

Kundi la pili lililohojiwa ni vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 30 wanaoamini utendaji kazi wa rais kwa asilimia 82, na kwamba ataleta mabadiliko kwenye sekta ya ajira na elimu kwa sababu amelivalia njuga tatizo la watumishi hewa na ajira za kwa wahitimu zitapatikana kwa kiasi fulani tofauti na ilivyokuwepo tatizo la watumishi hewa.

Kundi la tatu ni wananchi wenye umri wa miaka 30 hadi 60 ambao asilimia 89 walisema upo uwezekano wa watumishi wa umma kurejesha imani kwa serikali kutokana na juhudi za rais alivyopambana na ufisadi na rushwa.

Pia kundi hilo linaamini kwa rais atamaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa mwezi lakini pia wanaamini nidhamu ya watumishi wa umma itaongezeka. Mikoa iliyofanyiwa utafiti ni Tanga, Dodoma, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Tabora, Kigoma, Simiyu, Morogoro, Pwani, Arusha, Manyara, Geita, Mara na Ruvuma.

Chanzo:Habari leo
 

Attachments

  • 1466738006437.jpg
    1466738006437.jpg
    69.1 KB · Views: 99
  • 1466738015349.jpg
    1466738015349.jpg
    57.4 KB · Views: 105
Huu utafiti umemuonea Magufuli. Sidhani kama kukubaliwa kwake kunapungua chini ya 98 au 99% hivi. Subutu wee. Rais huyu shoka eti. Tena uchaguzi ukifanyika leo na kura wakawapa chadema wakahesabu wenyewe bado Magufuli atashinda kwa asilimia nyingi. Nchi imekaa sawa aisee.
 
Katika ripoti ya utafiti uliotolewa leo na gazeti la Habari Leo na Majira, inaonyesha Rais Magufuli kwa sasa anakubalika kwa asilimia 89, Jakaya Kikwete umaarufu umepanda na Lowassa kashuka zaidi...

Hii ni kiashiria kwamba uchaguzi ukifanyika leo Dr. Magufuli atashinda kwa zaidi ya asilimia 89.

Mytake:.. Hali ikiwa hivi, na kule upande mwingine Dr. Tulia akizidi kukaza nakiona rasmi kifo cha upinzani by 2020
Magazeti yenyewe ya Habari Leo na majira. Wameshituka nini? Kumbe wameshangamua kuwa hali siyo nzuri kwa Mheshimiwa the only option out is PROPAGANDA!
 
Habari Leo inamilikiwa na nani? Halafu wewe unaewaita wapinzani nyumba na kwamba wamebanwa eti hawana pakutokea......hujitambui na hujui maisha Hama kwanza kwa wazazi unakokula Bure ndo utaweza kuandika point
 
Habari Leo inamilikiwa na nani? Halafu wewe unaewaita wapinzani nyumba na kwamba wamebanwa eti hawana pakutokea......hujitambui na hujui maisha Hama kwanza kwa wazazi unakokula Bure ndo utaweza kuandika point

Tulia dawa ukuingie...!
 
Tulia dawa ukuingie...!

Dawa umejidunda mwenyew. Cjawahi kuamini tafiti za tz hata siku moja. Kwanza wabongo mm siwaamini. Huyo mnaemsifia ni kwamba kuna watu wansikia kichefuchwfu wakimuona.. Watoto wa maskini wamefukuzwa dodoma alafu wakupende? Unafikiria kuitia.........
 
Back
Top Bottom