Utafiti Mdogo wa kwanini serikali hii iwe ya vijana zaidi kuliko wazee

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Wana JF,

Tukiwa kwenye furaha kuuubwa kwa teua teua za vijana zinazoendele za serikali makini, tumefanya utafiti ndogo na kuona kasoro kubwa za wazee zilizolifanya Taifa hili kuingia mdororo wa kiuchumi , kuanzia kibiashara, kilimo, uchimbaji na ufugaji.

Utafiti wa awali unaonyesha kwamba wazee wengi walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea , hawana mafunzo mapya na ikitokea akajua kitu hataki kabisa kumfundisha mwingine kwa kuofia kuchukuliwa nafasi yake.

Wazee wengi wamezoea kutukuzwa, hawapendi kabisa kujifunza vitu vipya kufuatana na mabadiliko ya technology, hivyo akitokea tender ya kubadilisha mifumo mipya huwa wanaichelewesha makusudi, hili isifanikiwe.

Ni watu waliojibebesha majukumu mazito sana hasa za familia zao zilizopotelewa na mzazi mmoja au wote hivyo inabidi kutumia njia zozote zile kufyoji vitu ili wapate pesa za kuhudumia family kubwa.

Mazoea ya kupewa kila kitu wakazi wa enzi za mwalimu kumewafanya wadumae kimaendeleo hivyo wengi walijikuta bado wako kwenye nyumba za serikali wakiwa wamejisahau, ikitokea wakapata chance uoga wao uwafanya wakwapue mali haraka haraka ili wakistaafu wasipate shida.

Wengi wao hawajui bajeti kwani walikuwa wanategemezi wengi kwenye mabaa, nyumba ndogo jambo ambalo limewafanya wawe wabadhilifu ili kukidhi haja hizi.

Walijaza sana watumishi ambao hawana viwango kwa kuwa wengi ukurugenzi waliupata kwa kuonga.

Wanaigharimu sana serikali kwa kusoma wakiwa kazini wakati muda wao wa kuitumikia kwa cheo hicho ni mfupi

Kwa nini vijana:
Hawaigharimu sana serikali kwani wanasoma kwa mkopo ambao wataurejesha

Serikali inachukua watu walikamilika ki-idara, hakuna mafunzo mapya wakiwa kazini (kujiendeleza kielimu wakiwa kazini)

Vijana wa sasa hawapendi mizigo (familia zisizo zao) hivyo upenda kuhudumia famia yake tu jambo ambalo huwafanya walizike na walichokipata.

Wengi wamesoma kwa malengo na wafanya kazi kwa malengo hivyo akipata kijumba kidogo na ka-gari (usafiri) utulia tu kufanya kazi

Kila kijana aliyepita chuo amejifunza kompyuta hivyo kazi nyingi ujifanyia kuepuka kusambaa kwa nyaraka kupitia sekretary.

Upenda kujifunza vitu vipya ili kuleta ufanisi kazini (Mfano Makonda, Mchechu)

Hivyo basi vijana kwa pamoja tunamshukru Mh. Rais kwa kuyaona haya mapema kwani naye anajua kuwa wazee ndio waliotufikisha kwenye tabu hizi , sasa ameagiza kuondoa kero za ukritimba, yaani walijifanya miungu watu wapotezwe kabisa.
 
Alafu ilikuwa akija.kijana mwenye digrii kwenye halmashauri hasa mikoani akajifanya anafata sheria na maadili ya kazi,hao wazee wakikuhurumia wanakuweka benchi tu vinginevyo wanakupiga kipapai hakuna rangi utaacha ona..
 
Alafu ile principle ya kuwa u cant teach an old dog new tricks inatumika hapa pia..
 
Back
Top Bottom