JENDALUJEJE
Member
- Nov 18, 2012
- 43
- 22
Ulikuwa na mke wa ndoa,mlipendana sana.....mliishi kwa miaka 4,2kabla ya ndoa na baada ya ndoa 2.
Katika muda huo,mkeo alishabeba mimba mara2 zikaharibika kwa tatizo la homorne........mkiwa katika kutafuta ufumbuzi wa kitabibu................ukawa unachepuka kwa mdada fulani..................ikasababisha mkatengana na mkeo.
Ulipoulizwa na wazazi ukadai hujawahi hata kutongoza tangu uoe.....wk mbili baada ya mkeo kuondoka yule bi mdada akaanza kukutembelea hme,mara anapika,mara anafua...ilimradi mbwembwe nyingi,baada ya miezi 2,mdada akadai "NINA MIMBA YAKO",akahamia kabisa!
Wazazi wakakusihi,mrudishe mkeo,ukadai "HUYU MTOTO ATAKAYEZALIWA ATAHITAJI MAPENZI YA WAZAZI WAWILI"..........ukamtwanga talaka mkeo,ukatuma posa kwa mdada na mahari juu.Ukauza kiwanja ulichonunua na mkeo na kuanza ujenzi fasta kwenye kiwanja ulichumnunulia mdada kwa madai unamwandalia mtoto.
Siku za nyuma ulishapata wasiwasi kuhusu mtoto huyo,ukazuka ugomvi mkubwa,mama mkwe wako akaja fasta toka kijijini kuamua kesi,ukaendelea kuishi na binti yake.
Tangu alipozaliwa huyu mtoto, mdada aliweka vijiti vya uzazi wa mpango,akidai mpaka mfunge ndoa ya kanisani na vigelegele kama uliyofunga na mkeo wa kwanza,ndio atazaa mtoto wa pili!
Mkeo alishakubembeleza myamalize ukagoma,nduguze wamemshauri atafute mwanaume mwingine azae naye,amegoma.....anasema anataka aone mwisho wako!
Mtoto alipofikisha miaka 4,anajitokeza njemba,tena ya mtaani mlipohamia(nyumba alitafuta huyo mdada,hapakuwa na dalali) na kudai mtoto ni wake na anamtaka.Mbaya zaidi sura ya mtoto ni copy right na huyo jamaa.Siku za nyuma,shemejio(binamu na mkeo mpya,ambaye ndie anayemlea mtoto huyo)aliwahi kukuuliza, "HIVI SHEMEJI UNAMWONAJE "JINA LA MTOTO"?.....kafanana na nani?akamalizia na kauli....MJINI HAPA!Mwanamke akiulizwa,anajibu..."Fanya maamuzi yoyote kama unahisi si mtoto wako"
Ndugu wote walishakususa,na hakuna anayekutembelea,wanakuja ndugu wa mke tu,yaani uko bize upande wa ukweni.......mke mpya alipigwa stop na wifi zake,asikanyage kijijini kwenu,nawe ukajibu kwa mbwembwe......ulishaamua hurudi nyuma!
Nimejitahidi kufupisha..............
Hebu wadau toeni msaada,wapi pa kuanzia jamani........yamemtokea ndugu yangu kabisa,sasa kawa kama amechanganyikiwa.