Utabiri kuhusu kampuni ya ACACIA na makinika

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
319
500
Kuna taarifa kupitia vyombo vya habari leo Juni 3/2017, kuwa Rais wa Kampuni ya madini ya Barrick Gold na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Acacia, Kelvin Dushnisky, amekuwa hapa nchini kwa wiki hii yote, akiwa pamoja ya Bwana Brad Gordon, Mtendaji Mkuu wa Kampuni tanzu ya Barrick, Acacia.

Ujio wa Bwana Kelvin Dushnisky unafuatia serikali ya Tanzania mwezi Marchi 2017 kusitisha kampuni ya Acacia kuendelea na biashara ya kuuza mchanga wa madini nje ya nchi. Mchanga wa madini uliositishwa huchimbwa katika migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu iliyopo katika mkoa wa Shinyanga.
Kutokana na sitisho hilo, wiki iliyopita hisa za Acacia katika soko la London zilishuka kwa asilimia 46.

Utabiri wa kinachoweza kutokea

Kwa kuzingatia mwenendo, vitendo na tabia za Acacia, baada ya ujio wa kiongozi wake mkuu akiambatana na mtendaji mkuu, tunaweza kutabiri, pengine kwa uhakika zaidi kuwa kampuni ya Acacia itakiri makosa yake (kukosa uaminifu katika biashara za madini/michanga ya dhahabu), kisha kupigia magoti serikali, kuruhusiwa kulipa nakisi ambazo kampuni hiyo ilikuwa imekiuka (imekwepa -evade) kulipa, ikiwa ni kodi, mirabaha na tozo nyingine.

Serikali kwa upande wake inaweza kuridhia maombi ya kampuni ya Acacia kwamba ilipe nakisi hizo kwa muda wote utakaodhihirika malipo husika kutolipwa kwa sharti kuwa mikataba (MDAs) baina ya serikali na Acacia idurusiwe mara moja (with immediate effect), Board ya Acacia imfukuze kazi (fired with immediate effect) Brad Gordon (CEO) na kisha kampuni ifanye mabadiliko makubwa (significant changes) kweye management za migodi na kampuni kabla ya kuruhusiwa kuendelea na uzalishaji wa dhahabu tena.

Baada ya hapo Tanzania itakuwa ime-set precedent ya kudurusu mikataba yote (makampuni yote) ya uwekezaji katika madini, na pengine hata mikataba ya gesi asilia pia hapa nchini. Tunachoweza kufanya kwa sasa ni kusubiri kushuhudia mabadiliko (sweeping reforms) hayo tunayoyatabiri.

Mgodo wa Bulyanhulu ulianza kuzalisha dhahabu mwaka 2001 wakati Buzwagi ulinza uzalishaji mwaka 2008. Migodi hii miwili, pamoja na mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime (eneo la Nyamongo) inamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Acacia mining. Kati ya migodi hiyo yote, hakuna mgodi uliowahi kulipa kodi ya makampuni (30% ya faida). Mgodi wa Buzwagi unatarajia kufungwa Septemba 2018 wakati Bulyanhulu utafungwa mwaka 2025, mara baada ya dhahabu kuisha katika migodi hiyo.

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 

war sniper

Member
Dec 10, 2016
88
125
Hili lawezekana kwa kuwa kuna taarifa za acacia kuwa na matumaini ya kuzungumza na serikali na kuelewana
 

kankiza

Senior Member
Apr 15, 2016
160
225
Mungu Atusaidie haki itendeke.JPM ABARIKIWE KWA KUHAMUA KUIJITO MUHANGA KWA UZARENDO ALIOUONESHA KTK NCHI HII.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom