Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,914
- 3,437
Rafiki yangu mpendwa,
Japo huwa siamini kwenye utabiri na ubashiri, nimegundua njia ya uhakika kabisa ya kuweza kutabiri kipato chako kwa usahihi mkubwa.
Na leo, kwa kutumia njia hiyo, naenda kukutabiria kipato utakachoingiza kwenye mwaka huu mpya 2023 ili uache kujidanganya na kujiumiza.
Najua huu mwanzo wa mwaka una moto wa kuweka malengo ya mwaka. Na moja ya malengo unayojiwekea ni kuongeaa kipato.
Kwenye ujumbe wa leo nataka nikusaidie ili usijisumbue na malengo ambayo umekuwa unayaweka kila mwaka kwa kujidanganya.
Kuna taarifa tano ninazohitaji ili nikutabirie kipato chako cha 2023 kwa uhakika.
1. Kipato chako cha 2022.
2. Watu 5 unaotumia nao muda wako mwingi.
3. Vitabu ulivyosoma mwaka 2022.
4. Muda ambao huwa unaamka, unalala na masaa unayoweka kwenye kazi.
5. Mtazamo wako kuhusu fedha na utajiri.
Baada ya kupata taarifa hizo tano, hiki ndiyo kipato utakachoingiza 2023.
Rafiki,
1. Kama utaendelea kuzungukwa na watu wale wale ambao wamekuwa wanakuzunguka.
2. Kama hutasoma vitabu vipya.
3. Kama utaendelea kufanya kwa mazoea kama unavyofanya sasa.
4. Kama utaendelea na mtazamo ulionao sasa kuhusu fedha na utajiri.
Kipato chako cha mwaka 2023 kitakuwa kinafanana au chini ya kile cha 2022.
Hilo nakuhakikishia bila ya shaka yoyote.
Huwa siamini kwenye 'kubet' lakini kwenye hili naweza kubet kiasi chochote kile na nina uhakika wa kushinda.
Kwa kumalizia, kama kweli unamaanisha hayo malengo ya kifedha unayojiwekea kwenye mwaka huu mpya 2023, fanya mambo haya matano mara moja;
1. Weka lengo la kiasi cha kipato unachotaka kuingiza. Andika namba kabisa na siyo kusema fedha nyingi.
2. Badilisha watu wanaokuzunguka, hasa wale watano unaotumia nao muda wako mwingi.
3. Soma angalau kitabu kimoja kila mwezi.
4. Ongeza muda unaofanya kazi/biashara. Anza saa moja mapema kabla ya wengine na maliza saa moja zaidi ya wengine. Tumia muda wote kwa tija.
5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu fedha, utajiri na matajiri. Amini fedha ni kitu kizuri, utajiri ni haki yako na matajiri ni watu wazuri.
Fanya hayo na mwaka huu 2023 utakwenda kuwa wa kipekee sana kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Mkuu wa CHUO CHA MAUZO