Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Nikiwa mwanachama hai wa ACT, nimeona nichukue nafasi kumtahadharisha Kiongozi wa ACT Zitto. Jambo la kwanza analopaswa kulijua ni kuwa anasimamia sera za ACT popote awapo, chama ambacho kimejipambanua na kujitofautisha kisera na vyama vingine vya upinzani.
Kwa mujibu wa maelezo ya kamati ya maadili, kosa la Zitto ni utovu wa nidhamu kwa kukiuka kanuni na taratibu za bunge ikiwamo kufanya "fujo", ninamkumbusha Zitto kuwa, sera za kuanzisha vurugu, kupiga kelele si sera za ACT, ningefurahi sana Zitto kufukuzwa bungeni kwa kuleta hoja au kujenga hoja sio kukosa nidhamu kwa kiti. Ni aibu kuona Zitto anajumuishwa kwenye makosa na wabunge wanaofahamika kwa utovu wa nidhamu hata katika jamii wanayoishi.
Kuna taarifa zinasambaa kuwa zitto na wabunge wengine waliofukuzwa wanaopanga kuzunguka nchi nzima, katika hili, nimeshituka kwa kweli, ushwahiba huu wa Zitto na Lema na wengine ni katika yepi? je kuna kikao chochote cha chama ACT rasmi kilichopitisha na kujadili suala la Zitto kutimuliwa bungeni?
Nikuhakikishie tu Zitto, ACT bado changa mno na tupo katika kipindi muhimu cha kukijenga chama, uwe makini mno. Kumbuka kuwa, hao watu muda wowote wanaweza kubadili gia angani na kukuacha usijue la kufanya.
Ushauri wangu kwako ni kuchukua hatua za kisheria na kikanuni kupinga adhabu uliyopewa, weka pingamizi hilo kwa maandishi ukiainisha makosa uliyopewa na utetezi wake hii ni kama unahisi umeonewa, na ikithibitika ulikiuka sharia au kanuni kubali adhabu au omba msamaha. Ni kwa njia hizi tu utarudisha imani kwa wafuasi wako na wa chama kwa ujumla.
Wenu
Tume ya katiba
Mcheza Pool Table Maarufu