Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,934
Nchi yetu inapitia kwenye njia tatanishi japo siyo ya ajabu. Siyo ya ajabu kwa sababu kila Taifa hupata changamoto kufuatana na mazingira yake lakini mataifa hutofautiana zaidi katika weledi na werevu wa kutafuta suluhisho sahihi kwa wakati sahihi.
Rais japo siyo mtaalam wa kila kitu lakini anabeba dhamana ya kila kitu maana ukamilifu wa Taifa ni mchanganyiko wa mambo mengi yaliyofanywa kiusahihi. Changamoto kubwa tunazozipitia ambazo zinaifanya nchi yetu kutokuwepo kwenye kwenye njia sahihi na viashiria vyake ni kama vifuatavyo:
KUFUTWA/KUPUNGUZWA KWA MISAADA
Tukio la kwanza la dosari ilikuwa kusimamishwa na kufutwa kwa msaada wa fedha ya MCC kiasi cha zaidi ya TZS 1.3 trillion kilichokuwa kinatolewa kila mwaka. Huwezi kumlazimisha mtu akupe msaada lakini sababu za kuondolewa msaada ule zilikuwa zinaichafua. Msaada ule uliondolewa kwa sababu nchi haifuati misingi ya demokrasia, haki na uhuru wa watu na vyombo vya habari. Mifano iliyotolewa ni serikali kuufuta uchaguzi halali wa Zanzibar na kuendesha uchaguzi bandia kwa nia ya kupora ushindi wa Maalim Seif. Jambo lile kuna uwezekano mkubwa halikupangwa na Rais Magufuli, lakini ndiyo aliloanza nalo. Kuanza uongozi na dosari kunakupa dosari na kuangaliwa zaidi na kila Taifa kwa mtazamo hasi.
Tuna uwezo wa kuwalaumu wazungu, lakini tunawalaumu kwa sababu tuna sababu za msingi au kwa vile tu tunaweza kulaumu? Hivi sisi ni binadamu tuliokamilika au tulio nyuma ya ubinadamu halisi? Kwa nini mpaka uambiwe na watu wengine kuwa unatakiwa kuheshimu maamuzi ya wananchi? Kwa nini mpaka uambiwe na watu wengine kuwa unatakiwa kuacha uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari ufanye kazi? Tunawalaumu wazungu lakini tatizo kubwa la nchi yetu na baadhi ya nchi za Kiafrika ni kushindwa kujitawala. Kama Taifa, mnaposhindwa kufuata katiba na sheria zenu maana yake mmeshindwa kujitawala, na mnatoa haki ya watu wengine ambao wanawaona ninyi hamjaufikia ubinadamu wenu halisi, kuwaonya, kuwasema na hata kuwachukulia hatua.
Nchi kama Tanzania, mapato yake makubwa ya fedha ya kigeni hutegemea mauzo ya madini, utalii na misaada. Pesa ya misaada ni fedha ya kigeni, zaidi ya kukamilisha baadhi ya miradi lakini inaingiza fedha toka nje. Kupungua kwake kwa ghafla huathiri uchumi. Kila Taifa linapenda kujitegemea lakini kujitegemea ni process, siyo useme unajitegemea kwa sababu hata ungesema unataka kusaidiwa hakuna wa kukusaidia.
KULEGEA KWA UMOJA WA KITAIFA
Kuna mambo ambayo yamefanyika ambayo hata yangefanyika mahali pengine popote, ni lazima yaondoe umoja, ushrikiano na mshikamano. Umoja wetu haujazorota kwa sababu ya ugumu wa maisha bali kwa sababu ya matendo ya uovu, na uovu huu zaidi siyo ule wa mtu na mtu bali baadhi ya makundi ya watu na serikali au vyombo vya serikali:

- Kupotea kwa watu, kuuawa, kushambuliwa watu, kuwaweka watu ndani na kuwafungulia mashtaka bandia ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hasa wale wanaonekana kuikemea au kuikosoa serikali/viongozi wa serikali. Haya ni mambo mapya kabisa mabaya kuliko yote ambayo yaliletwa awamu hii. Na mbaya zaidi wapo wanaojivunia na kutamba hadharani kwa vile wana uwezo wa kuyatenda hayo dhidi ya wasiowapenda. Kuna Waziri mpaka aliwahi kutamka wazi kuwa mtu anaweza kukamatwa na kuwekwa ndani hata kama hajavunja sheria. Hata kama mtu huyo atakuja kutoka baadaye lakini atakuwa tayari ameteseka. Kwa nchi nyingine, Rais angekuwa alikwishamfukuza Waziri huyo au wananchi wangekuwa wamekwishamwondoa ila hapa kwetu, huyo ndiye ataonekana ni kiongozi shujaa maana ana uwezo wa kuwaonea watu kwa namna anavyotaka.
Rais wa nchi na viongozi waandamizi, wanapopewa mamlaka, jambo la kwanza ni kula kiapo cha kutii na kuilinda Katiba. Mantiki yake ni kuwa wajibu wa kwanza wa viongozi hawa ni kuilinda katiba na sheria zinazotokana na katiba hiyo. Kosa kubwa kabisa kuliko yote kwa Rais na viongozi waandamizi ni kukiuka Katiba maana ni kukiuka kiapo chao. Rais amepewa uwezo wa kuongozi kutokana na kuapa kuwa atafuata katiba. Haki ya mtu kuishi, kulindwa, kupewa stahiki sawa, usalama wake na mali zake, ni jukumu la kwanza la Rais, wasiaidizi wake na Serikali yake. Kuzorota kwa usalama, kutekwa na mashambulio dhidi ya watu wenye kuikosoa serikali ni doa kubwa ambalo limelegeza mshikamano miongoni mwa wananchi maana wapo wanaoona ni sahihi kwa watu wenye fikra tofauti na watawala, kupotezwa, kushambuliwa au kuwekwa mahabusu bila hatia,; na kwa upande mwingine ni wale wanaotaka haki kwa kadiri ya katiba yetu. Hali hiyo imepunguza sana mshikamno kati ya makundi ya watu, na kati ya baadhi ya makundi ya watu na serikali.
Wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, kulikuwa na makosa mengi, hasa kwenye uchumi. Kuna kipindi, watu waliishi katika maisha magumu sana kiuchumi na kihuduma, lakini kubwa kuliko yote, wakati wote, watu hawakupungukiwa umoja. Wote walisimama pamoja. Wakati wa vita vya Kagera, Amin alikuwa na vifaa vingi vya kisasa, na jeshi lake lilikuwa katika hali bora zaidi kifedha, lakini tulishinda kwa sababu ya umoja na mshikamano. Leo hii akitokea adui wa nje, kuna uwezekano wa baadhi kusimama na adui dhidi ya raia wenzake. Lakini hali hiyo haijazuka tu bila imetengenezwa.
2. UPENDELEO NA UBAGUZI
Sitalisema sana hili. Wapo watakaopuuza lakini watawala na watanzania wanaolipenda Taifa walitazame kwa umakini. Hali hii inaua Umoja na kuleta utengano. Viongozi wengi kutoka kanda moja. Miradi mingi mikubwa kuelekezwa kanda moja. Miradi mingi kujengwa eneo analotoka Rais. Haimaanishi kuwa huko ilikowekwa hiyo miradi hakustahili lakini kilicho kidogo kipelekwe kwa kuwafikiria watu wote. Ukiwa kiongozi siyo tu hustahili kufanya upendeleo bali unatakiwa kuweka mazingira ambayo hayaibui hisia kwa watu wako kuwa kuna upendeleo, hata kama haupo.
Kuna mambo mengine, inawezekana yasiwe halisi, na au yanafanywa na watu wajinga kutokana na ujinga. Kuna baadhi, tena wengi ni vijana, kuna wakati wamekuwa wakiwashawishi vijana kujiunga na CCM, na hata kuwaandikisha vijana hao kwa kuwaeleza kuwa wakijiunga na CCM watapata ajira, na kama ni wanafunzi, basi watapata mikopo ya vyuo. Kiuhalisia inawezekana wanaosema hivyo, wanafanya hadaa, lakini tusiruhusu kauli za kijinga namna hiyo hata mtu akafikiri anakosa mkopo au ajira kwa vile siyo mwana-CCM. Itajenga chuki.
KUMOMONYOKA KWA DIPLOMASIA
Diplomasia siyo ubabe. Kuna hulka imeota mizizi katika awamu hii. Viongozi wengi katika ngazi zote, hawana diplomasia. Wanadhani kila mahali ni amri na nguvu. Kati ya vitu vinavyoweza kumwangusha mwanadamu ni kutumia nguvu na kuiacha akili na hekima. Nyati mpaka leo analiwa na simba ambaye ana uzito mdogo zaidi kuliko yeye kwa sababu nyati anatumia nguvu pekee yake. Tabia hii ya kupenda kutumia nguvu kwenye mambo yetu ya ndani, kwa namna fulani imeanza kwenda mpaka nje ya mipaka ya nchi. Huko nje hatuna wa kumtisha sisi, halafu akatishika. Dunia inaogopa wanaotumia akili na siyo wenye sauti ya kulalama. Kupiga kelele sana na kulalama ni dalili ya kupungukiwa maarifa unayotaka uyazibe pengo lake kwa sauti ya mdomo badala ya akili. Kama Taifa kuna faida kubwa sana ya kutengeneza marafiki wengi wengi kuliko kuwapunguza. Na ukitaka kuwa na marafiki wengi uwe na uwezo zaidi wa kusikiliza kuliko kupayuka.
Matukio ya kuchoma vifaranga vya kuku toka Kenya, kutaifisha ng'ombe wao, matumizi ya maneno kama mabeberu dhidi ya binadamu wenzako, sisi kujifanya tuna uwezo sana wa kufanya mambo mengi wakati udhaifu wetu unajulikana sana Dunia nzima, haitusaidii chochote kama Taifa. Tujifunze zaidi kusikiliza kuliko kutoa amri. Serikali na viongozi wawasikilize zaidi wananchi kuliko kuwaamrisha. Kama nchi tuyasikilize zaidi mataifa mengine kwa mambo yanayogusa Taifa letu kuliko kuwadharau. Hakuna Taifa la kuetetemeshwa na nchi yetu.
Kuwa na kesi nyingi, matamko/barua toka mataifa mengine (mfano US), Jumuia za kimataifa (Jumuia ya wanasheria wa Uingereza, Umoja wa Ulaya), dhidi ya serikali inadhihirisha mambo makubwa mawili - kukosekana weledi wa diplomasia na kukosekana mazingira huru na taasisi huru zenye nguvu, nchini. Mambo ambayo tulistahili kuyanena Watanzania dhidi ya serikali na viongozi pale wanapopotoka, sasa yananenwa na taasisi za kimataifa au mataifa ya nje.
Wanachi walizungumzia ubaya wa sheria ya mitandao, serikali haikusikiliza. Wananchi walizungumzia ubaya wa sheria ya vyama vya siasa, serikali haikusikiliza. Wananchi walizungumzia ubaya wa sheria ya Takwimu, serikali haikusikiliza. Wananchi wanazungumzia umuhimu wa Katiba mpya, serikali haitaki kusikiliza. Wananchi wanazungumzia umuhimu wa Tume huru ya uchaguzi, serikali haitaki kusikiliza. Na mengine mengi. Sisi sote tunahusika lakini kwa namna ya pekee Rais Magufuli anahusika zaidi. Rais alifikirie sana hili - sheria hizi nyingi mbaya zimeundwa wakati wa utawala wake. Akiwa nje ya madaraka atajisikiaje, watawala wengine wakaja wakazifuta hizi sheria zote mbaya?
KUYUMBISHA UCHUMI
Adui mkubwa wa ukuuaji wa uchumi katika nchi yoyote ni kodi adui. Kodi adui huua na kudumaza mitaji. Kodi adui huzifanya biashara zikonde na uwekezaji kusinyaa. Hakuna nchi Duniani iliyokuwa maskini ambayo ilipiga hatua haraka ya maendeleo kwa kuongeza ukubwa au uwingi wa kodi. Kuna kodi zimepunguzwa. Hilo ni jambo jema. Lakini bado kodi Tanzania ni nyingi sana na kubwa sana. Tanzania haitaendelea kwa kugawana umaskini, ni lazima kuwepo na sera na mazingira yanayovuta mitaji/utajiri wa nje kuja nchini mwetu. Kivutio kikubwa kimojawapo ni kodi rafiki, kodi zinazosababisha mitaji kukua haraka ili iendelee kuwekeza maeneo mengine au zinazoruhusu kupanuka kwa uwekezaji.
Kosa kubwa lililofanyika awamu hii ni kujenga uwoga kwenye uwekezaji na biashara. Harassment imekuwa kubwa sana japo imepungua kiasi siku za karibuni. Biashara ni independent entity, na kisheria ni mtu. Kumnyanyasa mtu kwa sababu ya biashara/kitega uchumi chake ni kuua uwekezaji. Hata kama kukiwa na makosa, isichukuliwe kuwa ni kosa la mtu binafsi. Mathalani kiwanda kimetirirsha maji ya sumu kwenye ardhi, mkuu wa Wilaya/Mkoa anasema Mkurugenzi awekwe ndani! Ni jambo la ajabu sana. Viongozi, na hasa Wakuu wa Wilaya na Mikoa, wafundishwe jinsi wanavyotakiwa kushughulikia matatizo ya miradi au vitega uchumi yanapojitokeza.
Nimepita mataifa mengi yanayotuzunguka. Watanzania wengi wawekezaji wapo huko. Wanafanya uwekezaji huko wakati hapa kwetu bado tunawahitaji sana. Wengi wao hawajaenda huko kwa sababu ya kutaka kupanua bishara bali ni kwa sababu ya mazingira yasiyoridhisha nchini ya uwekezaji. Watu wanakamatwa kwa makosa ya kodi lakini wanashtakiwa kwa uhujumu uchumi. Ni vema sheria hii ya Uhujumu Uchumi, na ya Utakatishaji Fedha, ikafanyiwa marekebisho ili hawa maadui wa Taifa wasizitumie sheria hizi vibaya dhidi ya wananchi. Polisi, DPP, wanasheria wa serikali, TISS au hata viongozi, wanaozitumia sheria hizi vibaya, hawa ni maadui wa Taifa.
RAIS KUTOKUWA NA MASIKIO MAKUBWA
Wajibu mkubwa wa kiongozi ni kuwa msikivu na mchambuzi. Ukiwa kiongozi ni lazima, na wala siyo hiari, kuwasikiliza unaowaongoza. Utasikia, utaambiwa na kushauriwa mengi, na mengine yatakuwa yanakinzana. Ndipo unapohitaji uchambuzi ili kujua ushauri upi unatakiwa kuuchukua. Na katika kufanya hayo, ana wasaidizi. Wasaidizi hawa wanaweza kuwa watu sahihi au siyo sahihi.
Ushauri wangu kwa Rais, ni vema kuhakikisha wakati wote una watu sahihi kwa majukumu sahihi. Siyo kila mtu anakuwa mtu sahihi wakati wote na maeneo yote. Una watu wengi ambao ni watu sahihi lakini hawapo maeneo sahihi. Prof; kwa asili yake, hayupo eneo sahihi. RC kwa vile wenzake wenye vyeti fake waliondolewa, yeye kutoondolewa kunamfanya Rais aonekane ni mtu wa upendeleo na asiyeongozwa na principles. Kugushi cheti au kutumia jina lisilo lako, ni kosa la udanganyifu, na ni jinai. Kiongozi anatakiwa kuwa kioo ambacho wengine hujiangalia ili kuweza kuona kama wapo sawasawa.
Hakuna mtu au taasisi isiyofanya makosa. Serikali yetu imefanya makosa mengi, na itaendelea kufanya makosa lakini jambo la muhimu, ni je, ina mfumo gani wa kugundua makosa yake, kujisahihisha, kutoa taarifa na kuwapa imani mpya walioathrika na makosa yaliyofanywa na serikali?