USTAARABU WA KWELI

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
2,910
Reaction score
3,024
Chiefs
Assalaam Alaykum

Bila kupoteza muda,naomba niingie moja kwa moja katika mada,iliyo chukua sura timilifu
Ustaarabu,ni mtu kuwa mwenye maendeleo chanya huku akipambwa na mila,tamaduni sahihi
Jamii zetu,tumekuwa na system ya kuchukua Ustaarabu wa watu fulani au namna fulani ya maisha yao,bila ya kuchuja,tumekuwa ni sawa na msanya kuni usiku,tunazoa mpaka nyoka,ilihali hatujitambui.
Ustaarabu kamili,ni ule uliokuwa ndani ya mipaka ya kisheria,utu na tamaduni sahihi
Kadhalika,Moja ya dira kuu kwa jamii endelevu au iliyostaarabika,ni kuangalia vijana wa jamii hiyo,Ukiwaona vijana wanajitambua na kuwa na ustaarabu uliobora,Basi jamii hiyo,itakuwa jamii nzuri/njema na yenye kuleta ufanisi sahihi
Kadhalika na kinyume chake.
Katika moja ya mambo ya ajabu katika jamii hii iliyotuzunguuka,ni kama yafuatayo
ZINAA:zinaa imekuwa ipo nje nje,bila ya aibu,imekuwa ndio fasion ya mjini,kijana kujinasibu kwa kuwa na wanawake wengi!!!
Ndio maana mmoja wa wasemaji wa kweli aliwahi sema
Ikifika zama,zinaa itatangazwa waziwazi,Basi zama hizo,hakuna balaa,isipokuwa litawashukiwa wana jamii hiyo mbovu
POMBE😛ombe nayo ni sawa na chai,mtu kununua ukichaa na mkojo wa firaun,kwake ndio pambo!!!tena mbaya zaidi,kila siku wanatokea watu,na kuipa majina mazuri mazuri
WATU KUKATAA UZEE:Uzee ni neema,itokayo kwa Mola,na ndio kimbilio la busara na hekima,lkn cha ajabu,ukifika jiji la Gharama,utawasikia watu wakinena,"Wazee mwisho Chalinze"
Utawaona nao,wakipaa mvi zao dawa,ili wafanane na nyele za vijana,na Vijana nao,wanapakaa rangi tofauti tofauti,kwa lengo la urembo
KUKOSEKANA HAYA/AIBU:Jamii imekaa mbali mno na kuwa na aibu,Hakuna mkubwa wala mdogo,kila mmoja hana haya wala aibu,afanya atakalo,maisha haya,hayana tofauti na mnyama
Tupu zimekuwa wazi mno,Midomo imechanua kwa kusema lolote bila ya kujali!!!

NI WAPI JAMII HII INAELEKEA?!!!
Nawatakia usiku mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…