Ustaarabu wa kukojolea kuta

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
548
Reaction score
62
Heshima na murua wa mtu hujulikana kutokana na tabia yake na wakati mwingine hata mavazi na namna ya uzungumzaji wake. Moja ya mazoea mabaya ni kukojolea kuta za nyumba. Kuna watu tena hata sio walevi, kwani wangekuwa walevi tunesema pombe ndio inayowaongoza. Lakini wao sio walevi wamevaa vizuri na wanaonekana watanashati lakini utakmkuta kasimama anakojolea ukuta wa nyumba. Huu ni uungwana kweli jamani? Ndio maana leo moja ya matangazo ambayo pengine huwezi kuyakuta katika nchi za wenzetu ni "TAFADHALI USOKOE HAPA, "USIKOJOLEE UKUTA" na kadhalika. Katika nchi nyingine huwezi kukuta haya kwa sababu haina haja ya kumuwekea mtu tangazo la usikojoe hapa ilhali yu mwenye kufahamu kwamba, hapaswi kukojoa hapo. Tustaarabike kidogo Watanzania. mambo mengine hayahitaji uwe na digirii hata uweze kuyapambanua, bali wapaswa kutumia akili yako kidogo tu.
 
Ninakubaliana na wewe kwa asili mia. Lakini tujiulize kwa nini watu hufanya hivyo???
Jee ni kwa kukosa ustarabu tuu au kuna sababu nyingine zinazowafanya wafanye hivyo? ninadhani kuna sababu pengine za msingi tuu zinazofanya watu wafanye hivyo kwani kutafanya hivyo inabidi wajikojolee nguoni. pengine uhaba wa vyoo vya jamii au sababu nyingine tu.
 

Mkuu Abunwasi, nadhani hata kama kuna upungufu wa vyoo vya umma katika maeneo mengi nchini, Si ustaarabu KABISA kuhalalisha kukojoa katika SEHEMU/MALI YA MTU simply kwa sababu hiyo..natambua kama binadamu tunazo haja, lakini haja zingine kwa kiasi fulani zinavumilika mf. ndiyo hizo za kukojoa ovyo, kutema mate ovyo,n.k.
 
Last edited by a moderator:
Ninakubaliana kabisa na hoja yako lakini kwa nini juu ya kwamba kuna matangazo ya kukataza kukojolea ukuta lakini bado watu wenye akili timamu bado hijisaidia haja ndogo ukutani. ningependa tutafiti kidogo ili kufahamu kwa kina kwa nini hali hii inaendelea.[hiyo ndiyo pointi yangu] WHY???????
 
akaa....sio sisi....ni wanaume hao....ndio washenzi wa tabia......
 
Hii ndiyo bongo bwana maisha hayana formular kabisa umetoka home ushapiga chai vikombe vya kutosha unatoka tu home grocery ya jirani unakuta marafiki zako wanapiga ze lager mara unaitwa na wewe unajumuika hapo unapiga kama 2,3 za chap chap.....ndo unakumbuka una safari yako ukiwa njiani sababu ya zile bia za bure ulizofakamia unabanwa na haja na hakuna vyoo karibu uadhani nini kitafuata hapo?

Ila ulaya ukishapiga chai yako na ukakojoa kwako no more free whatever......so unaweza jibalance mpaka muda utakaporudi home ndo ujisaidie tena. Nadhani yatupasa kuwa na formular ya maisha.
 
Acha porojo bana. Mbona bar nyingi tukiingia vyooni tunakojolea ukuta kama kawa. Wameshatuzoesha, tukifika kitaa kama kawa.
 
akaa....sio sisi....ni wanaume hao....ndio washenzi wa tabia......
Acha kuchonga bibie. Na nyie mkizoeshwa mwendo huo hapo chini, ukifika mtaani kitu kimebana na huduma hakuna unafikiri kinachofuata ni nini?

 
Ni tabia mtu hakufundishwa kujisitiri tangu utotoni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…