Usiwakandamize Maskini Utaumia

Usiwakandamize Maskini Utaumia

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Amo 8:4-5 SUV
[4] Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, [5] mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu;

Nabii Amos aliinuliwa na Mungu kukemea dhuluma na unyonyaji mkubwa uliokuwa unafanywa na viongozi na matajiri wa Israeli.

Ustawi wa taifa la Israeli kipindi hicho ulijengwa kiuchumi kwa kuwadhulumu na kuwanyonya maskini haki zao, jambo ambalo lilikuwa chukizo mbele za Mungu.

Andiko hili ni ujumbe wa hukumu ya Mungu dhidi ya uonevu uliokuwa unafanyika kwa jamii na ukosefu wa haki kwao.

Yesu alipokuja Duniani aliweka wazi kuwa alikuja kuwatangazia maskini habari njema, habari za ufalme wa Mungu, wamjue Yeye Mungu wa kweli.

Lk 4:18 SUV
[18] Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

Watu wanaowatendea vibaya maskini, wajue kuwa hawawatendei hao tu, wanamtendea Yesu Kristo mwenyewe, kwahiyo wanamgusa Mungu moja kwa moja kwa ubaya wanaoutenda.

Mt 25:40 SUV
[40] Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

Kumfanyia vibaya maskini unajitengenezea shida mbaya kwako, unaweza kusema hawezi kukufanya jambo lolote kutokana na hali yake duni, ila ujue hiyo kesi itakuwa ya Mungu mwenyewe.

Tujiepushe kuwaonea maskini, kuwadhulumu haki zao, kuwanyonya haki zao, kufanya hivyo tunaingia ugomvi na Mungu moja kwa moja.

Kugombana na Mungu hakuwezi kukuacha salama, huwezi kuwa na furaha ukiwa umefarakana na Mungu wako, huwezi kufurahia mafanikio yako uliyoyapata kwa kuwaumiza maskini alafu ukadumu nayo.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom