Usivunjike moyo, inuka endelea

Prince Naahjum_

Senior Member
Jun 13, 2016
139
125
Amekukumbuka lakini hatakutafuta tena. Kwa kipindi kirefu sasa amejaribu kuwa mwema kwako na kufanya jitihada zote kukufurahisha. Kwa muda mrefu amefanya kila kitu ili kukuonesha kwamba anastahili kuwa na wewe.

Ila mwishowe amejiona hawezi kuonyesha jitihada za kukupenda tena. Mwisho amejiona hawezi kujali tena, mwishowe ameona hawezi kabisa kukupigania. Amekumbuka Kila kosa ulilolifanya. Maumivu unayompa yamemshawishi kwamba wewe ni mtu mbaya kwake.

Dharau, usaliti, maumivu na kutomjali kumemsukumia mbali na kamwe hatarudi tena katika maisha yako.

Hivyo usitegemee atarudi tu kwa vile anakupenda. Usifikirie kwamba atakuwa na hisia kama za mwanzo juu yako. Usifikirie atakuja kuumia tena kwa yale uliomfanyia. Moyo wake ushakuwa sugu.

Usifikiri saa hii atatulia na kurudi tena! Inachukua maana kubwa kusema 'imetosha' inachukua muda mrefu kesema 'Sidhani kama nitarudiana na wewe', na inachukua maana kubwa kusema 'it's over' ila sasa ameshamaliza, anamaanisha anachosema.

Ni kweli, itakuwa ngumu sana kuwa mwenyewe maana alishakuzoea, ila ni vema awe mwenyewe kuliko kuwa na mtu ambae anamfanya ajisikie mpweke zaidi.

Ni kweli itamuumiza sana kuendelea na maisha yake, ila ni bora aumie kwa kuendelea na maisha yake kuliko kuumia kila siku katika mahusiano na wewe.

Ni kweli, itakua changamoto kubwa sana kumpenda mtu mwingine, ila ni bora akaja kumpenda mwingine atakapokua tayari kuliko kumpenda mtu ambae anamchukulia poa.

Nzi alimuuliza nyuki, mbona kila ukitengeneza asali binadamu wanakuja kuichukua kinguvu huku wakikupulizia moshi, lakini wewe bado unang'ang'ana kutengeneza hiyo asali.?

Nyuki akamjibu nzi, "waache waniibie asali, ila kamwe hawataweza kuniibia maarifa yanayotumika kutengenezea asali"

Hivyo basi hii ni maana njema kwako kwamba, thamani yako isivurugwe na binadamu wabaya, bado una mambo mazuri nafsini mwako ya ku share na yule atakae kuja kukupenda.

Usivunjike moyo, Inuka na endelea....Better days are ahead!

Rudisha mpira kwa golikipa, halafu anza mashambulizi upya, mechi itakuwa rahisi kwako kama Ujerumani walivyowalaza Brazili goli 7 kwa moja ule usiku wa tarehe 8 July 2014 Estadio Meniero, Brazil.

"A heartbreak is a blessing frm God, it's just his way of letting u realize that he saved you from wrong one"

Share




PRINCE NAAHJUM ALSINA
 
Back
Top Bottom