Usiumie kama hakupendi! Songa mbele

Usiumie kama hakupendi! Songa mbele

painboy

Senior Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
110
Reaction score
51
USIUMIE KAMA HAKUPENDI.... Usiumie kama hakupendi.ngoja niweke hili jambo vizuri kidogo.yaani ni bora uone kabisa huyo umpendae hakupendi kuliko ajifanye anakupenda kumbe hakupendi.maumivu yake ni makali huwezi amini.

Kuna watu wakiachwa huwa sijui kwanini wanalia?naelewa ni maumivu lakini ngoja nikuambie kitu.kabla hujaachwa kuna vitu fulani au viashiria kuwa umeanzwa kuchokwa.sikiliza ukiona mtu kaaanza kukuchoka anza kujitoa mapema kabla hajakuambia.iko hivi ukiona mawingu unajua kabisa kuna mvua.

Usitake mpaka mtu akuambie hakutaki.jiachie.siku hizi hauambiwi umechokwa yaani utaona kuna vitu vinapungua kidogo kidogo.utaona mawasiliano yanapungua,utaona hakujali,utaona hana muda na wewe.usisubirie akuambie kabisa hakutaki.na ili usiumie sana jifunze kumuacha aende.ukiachwa jifunze kusema japo nimeanguka ntasimama tena.ila jifunze kumsoma mtu ambaye anadai anakupenda wakati hakupendi.

Iko hivi maumivu ya mapenzi ni magumu lakini niamini mimi.kabla hatujaweza kutembea lazima tuanguke mara moja au mara mbili na saa zingine utasimamia meza.sasa mdau wetu mzuri naamini kabisa kuwa kakuacha lakini ndo unajifunza kutembea.ipo siku utapata mtu sahihi.unachohitaji usikate tamaa....
.. Nani kanielewa zaidi hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo mdogo tunasonga
Ziara yetu ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi wasioe iko pale pale
 
Aiseeee wadau wanadai vipi kuhusu kichwa Cha habari kinahusianaje na mada yenyewe
 
Hata Kama umeachwa sikushauri puchu ikuendeshe maisha yako hutakuwa huru ukiwa peke yako jigunze kuvumilia hali kikubwa uhai tu
 
Back
Top Bottom