Usituzingue!!! Wewe ni hawara tu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Unakutana na mwanaume, alishafunga ndoa kabla, hawajapeana talaka na mke wake, eti kwakua tu wametengana, kwakua tu hawaongei wewe unajiingiza moja kwa moja. Unaanza kuishi na huyo mwanaume kama mume wako, hakuna cha ndoa wala nini unaishi naye. Kama uko katika hali hii basi nataka ujue mambo haya matatu.

(1) Wewe ni hawara tu, kisheria mkitengana hawara hagawani mali. Mali zote mtakazochuma zikiwa na jina lake ni zake na si zenu, hata kama wewe ndiyo umechangia kiasi kikubwa. Lakini mke wake wa ndoa ambaye hata hawaishi naye yeye ana haki kisheria kusema ni mali zake na akitaka talaka wakagawana hizo mali.

(2) Wewe ni Hawara; Kisheria huyo mwanaume akiamua kufa basi jua kuwa vitu vyote mlivyochuma ambavyo vina majina yake, kama hakuandika wosia basi huenda kwa mke wake wa ndoa na watoto wake halali (labda kama wako aliwatambua) wanao ni watoto wa hawara hivyo kisheria hawarithi.

(3) Dhana ya ndoa (Kuishi miaka miwili mfululizo) haifanyi kazi hapa, kwamba ile watu wanasema kuwa ukiishi na mwanaume muda mrefu (kisheria miaka miwili mfululizo) anakua kama mume wako hapa haifanyi kazi kwakua tayari ana ndoa halali amabyo inatambulika. Kutembea na mume wa mtu mud amrefu haimfanyi kuwa mume wako, ni sawa na kuishi katika nyumba ya kupanga muda mrefu haikufanyi kuwa yakwako.

(4) Hata kama imeshindikana yeye kumuacha, hakikisha kuwa, kitu unachochangia katika kuchuma kiwe na jina lako wewe mwenyewe, lakini kile amabcho anawekeza yeye basi kiwe na majina ya watoto wenu kama hawezi kuandika yako, hapa utakua umejilinda kisheria lakini tofauti na hapo wewe unakua sawa na mchepuko hata kama huyo mke wake hawawasiliani.

(5) Sina uhakika sana kama kuna namna ambavyo mtu kama wewe anaweza kupata mali za huyo mwanaume, hata kama mmechuma wote lakini zina majina yake, labda uwe sijui na wakili mzuri namna gani ambaye anaweza kuihalalisha ndoa yenu (mahakamani kila kitu kinawezekana) ila kuwa makini, nimeandika kwakua kuna wadada wengi wanahangaika kuchuma na waume za watu kwakua tu wake zao wameondoka, aisee kuna siku mambo yatageuka usijesema sijakuambia.

Najua mpo wengi ila kama alishakua na ndoa kabla ila kuweni makini ndoa haivunjiki kwa kumfumania mtu au kumchukia, ndoa huvunjika kwa makaratasi kama sauti haitoshi nyie semeni🚶🏾‍♂️🚶🏾‍♂️
 
None of you seem to understand. I'm not locked in here with you.
YOU'RE LOCKED IN HERE WITH ME
 
Back
Top Bottom