Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Usitupe mtoto chooni, usikinyonge kichanga chako, usitoe mimba, na siku zote mlee mwanao vizuri kwa uangalizi na umakini wa hali ya juu. Huwezi kujua huyo ni nani. Muda ni shujaa wa kweli pale matokeo yanapodhirika.
Mwite mwanao jina zuri na umjenge katika misingi iliyo bora. Usiwe mbinafsi, mpe anachohitaji kama kipo ndani ya uwezo wako. Mwoneshe upendo mpaka yeye mwenyewe akiri kwamba anapendwa. Watoto ni wakoseaji mara nyingi, siyo yeye ni utoto. Muonye na umsahihishe kwa upendo. Mkaripie na umuadhibu kwa upendo.
Ukiachana na Bikira Maria (Mariam) aliyepata mimba maalum iliyomleta duniani Yesu (Nabii Isa), hakuna mwanamke mwingine mwenye ufunuo wa zawadi iliyo tumboni mwake. Pengine ni Rais, Waziri Mkuu, daktari, mwanamuziki mkubwa, kiongozi wa kidini, mwanasayansi wa kuogopwa na kadhalika.
Ukipata mimba, usiseme imekuja kinyume na matarajio. Pengine ndiye zawadi ya ukombozi. Kwa namna ilivyo, wapo watoto wengi walikatishwa uhai wao ama kwa mimba zao kutolewa au kuuawa baada ya kuzaliwa, lakini wangepata fursa ya kuishi pengine walimaanishwa na Mungu kuja kuwa watu wakubwa duniani.
Ipo siku, ile inayoitwa ya mwisho, mara itakapowadia, wapo marais, wanasiasa wakubwa, wanasayansi waliomaanishwa kuja kuikomboa dunia, viongozi wa kidini na kadhalika, watasimamishwa kwenye uwanja wa hukumu, kisha kutangazwa kuwa ni mashujaa walionyimwa fursa ya kuishi na wazazi wao. Labda, hata aliyemaanishwa kuwa mgunduzi wa tiba ya Ukimwi, mimba yake ilitolewa au alinyongwa akiwa kichanga!
MTOTO NI UTAJIRI
Hakuna asiyejua hili maana ndani ya familia nyingi, watoto wamekuwa ndiyo chachu ya mabadiliko ya kimaisha, kutoka duni hadi afadhali na hata bora. Ni vema kufurahi kila hatua ya upatikanaji wa mtoto na kumpa sapoti ya kufikia ndoto na malengo yake.
Pattie Mallette ni mama raia wa Canada, aliye na mchanganyiko wenye asili ya Canada na Ufaransa. Historia ya maisha yake ya nyuma inampambanua kama mwanamke aliyepitia mateso makubwa ya kudhalilishwa kwa kunajisiwa na kubakwa akiwa na umri wa miaka mitatu.
Pattie ni ufupisho wa Patricia, alizaliwa Aprili 2, 1976, Stratford, Ontario, Canada. Baba yake anaitwa Michael Mallette na mama yake ni Diana Henry Mallette. Akiwa na umri wa miaka miwili tu, baba yao aliitekeleza familia.
Pattie amekuwa na ndugu mmoja tu, Chris ambaye ni kaka yake. Dada yao mkubwa aligongwa na gari alipokuwa anakatiza mtaani kwenda kwa yaya wao na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka mitano.
Mwanaume wa kwanza kumfanyia tendo la ubakaji ni yaya wa kiume, akafuatia babu wa rafiki yake ambaye alikuwa anamlea. Maisha ya utotoni yalikuwa magumu kutokana na kukosa wazazi, hivyo kukua kwa msaada wa wasamaria wema ambao wengi wao walitumia vibaya usamaria wao.
Pattie alibakwa pia na watoto wa jirani ambao walikuwa wakubwa kuliko yeye. Anasema kwamba kubakwa na kudhalilishwa kingono, ilikuwa sehemu ya maisha yake kuanzia alipokuwa na umri wa miaka mitatu hadi alipofikisha 14.
Mateso hayakuishia hapo, Pattie anakumbuka tukio lililomuumiza sana alipobakwa akiwa na umri wa miaka 15 na mwanaume ambaye baadaye alitokea kuwa mpenzi wake.
Pattie anasema: "Nilifanyiwa vurugu nyingi za kimwili na wanaume mpaka nikazoea. Nilibakwa mara nyingi mno na kadiri miaka ilivyokuwa inasogea nilianza kuona kawiada."
YOTE HAYO NI HISTORIA
Pattie ndiye mama wa staa wa muziki wa Pop duniani, Justin Bieber mwenye umri wa miaka 21 hivi sasa. Hakuandikiana na Mungu kwamba mwanaye huyo ndiye atakuja kuyabadilisha maisha yake ya mateso kuwa burudani na utajiri, ila imekuwa kutokana na kujitoa kumlea kwa mapenzi makubwa pamoja na ugumu wote aliokutana nao.
Mwanaume aliyembaka Pattie, anaitwa Jeremy Bieber ambaye ni baba wa kibaiolojia wa Justin. Baada ya kumbaka baadaye waliamua kuwa wapenzi na kuishi kama wanandoa. Pattie anafafanua: "Ilikuwa ndoa ya kipekee, nilijua kabisa siyo sawa lakini tukakubaliana na ikatokea kuishi pamoja."
Pattie 39, anakiri kuwa maisha yake na Jeremy hayakuwa na maelewano na kuna kipindi waliachana kabla ya kurudiana tena akiwa na umri wa miaka 16. Baada ya penzi lao kurejea haikuchukua muda alinasa ujauzito na Machi Mosi, 1994, alimzaa Justin. Kipindi hicho alikuwa na miaka 17 na miezi 11.
Justin alipozaliwa, waliishi pamoja kama familia kwa miezi 10 tu kabla ya kutengana na kuanzia hapo, Pattie alianza kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku wa yeye na mwanaye kama mzazi pekee (single parent).
USHUJAA WA PATTIE
Kutokana na kupitia shuluba nyingi, Pattie aliona furaha pekee ni kuwekeza kwa mtoto wake. Alimlea kwa upendo mkubwa. Akawa anabangaiza kwa kufanya kazi ndogondogo ili apate fedha za kujihudumia yeye binafsi lakini zaidi kumpa malezi bora mwanaye.
Pattie alikumbuka jinsi yeye alivyokimbiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka miwili tu, na kwa kumbukumbu ya mateso aliyopitia, alitia nia kisha akajifunga kibwebwe kuhakikisha Justin hafikii mateso aliyoyapata katika ukuaji wake.
Kila kilichokuwa ndani ya uwezo wake alimpa mwanaye. Na akajitahidi kufuatilia kujua kipaji cha Justin. Alipobaini kuwa ni mtoto anayekua katika mapenzi ya muziki, alifanya kudunduliza fedha na kumnunulia vifaa mbalimbali, ikiwemo piano, ili kukuza kipaji chake.
Hakuishia hapo, alimtia moyo kuwa anaweza, akamhimiza kufanya mazoezi ya kuimba na kutumia vifaa vya muziki. Kwa kipato chake kidogo cha kufanya vibarua vya kusafisha ofisi za watu na nyinginezo, alihakikisha anapata fedha na kufanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kumtengenezea njia ya mafanikio mtoto mwanaye.
Pattie alikuwa na kipaji kikubwa katika muziki na kuigiza lakini hakufanikiwa kutokana na giza totoro lililoyazunguka maisha yake wakati anakua. Hiyo ndiyo sababu aliona baada ya kukosa yeye, basi awekeze kwa mwanaye, akiamini Mungu atatengeneza njia.
Alimpeleka kwenye shindano la mtaani la kusaka vipaji, lililoitwa Stratford Star. Katika shindano hilo Justin aliimba wimbo So Sick wa mwanamuziki Ne-Yo na akafanikiwa kushika nafasi ya pili.
Pattie akiwajibika kama meneja wa Justin, aliweka kwenye mtandao wa YouTube video inayomuonesha mwanaye akiimba katika shindano la Stratford Star. Ni video hiyo ambayo ilifungua njia ya kila kitu.
Meneja wa sasa wa Justin, Scooter Braun, aliiona video hiyo kisha akapitia maelezo aliyoweka Pattie, waliweza kuwasiliana. Braun ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya RBMG (Raymond Braun Music Group) akichangia hisa na mwanamuziki maarufu duniani, Usher Raymond.
Baada Braun kumpata Pattie, aliweka mazingira sawa kisha alimkutanisha Justin na Usher kabla ya kukubaliana kumsainisha kwenye kampuni yao na kuanza kufanya kazi chini ya watayarishaji wakubwa wa muziki.
ANAOGELEA UTAJIRI
Justin ni mwanamuziki anayependwa sana duniani na kazi zake zinanunuliwa mno. Mitandao ya Celebrity Net Worth, The Richest na Forbes, inaandika kuwa Justin ana utajiri unaozidi dola milioni 200, sawa na shilingi bilioni 425.
Kwa utajiri huo peke yake, Pattie amekuwa ni mwenye kuishi kwa raha sana. Shida zote za nyuma ni historia ya kusimulia tu. Anaishi kwenye jumba la kifahari lenye kila aina ya starehe. Justin amekuwa akijitahidi kumfanya mama yake atabasamu kila siku.
Mbali na fedha za mwanaye, Pattie mwenyewe aliona fursa kupitia umaarufu wa Justin, akaandika kitabu kinachoitwa Nowhere but Up (The story of Justin Bieber's mom), chenye simulizi ya maisha yake ya dhiki, alivyonyanysika tangu akiwa mdogo, alivyomzaa Justin na kumlea kwa tabu mpaka kufika naye alipo.
Katika wiki ya kwanza, kitabu hicho kilishika nafasi ya 17 katika chati za mauzo za New York Times Best Seller. Na mauzo ya jumla, yamemuwezesha Pattie kumiliki utajiri wa dola milioni 20 (shilingi bilioni 42.5). Hakika maisha yamebadilika kwa sana.
Pattie anaishi anavyotaka, anakula na kuvaa vile anavyojisikia. Anaingia kwenye maduka ya mavazi ambayo yanatumiwa na watu mashuhuri duniani. Anabadili magari kadiri anavyotamani, na maisha yake hayana shaka hata kidogo.
Hayo ni matunda ya kuwekeza kwa mtoto. Angetoa mimba ya Justin au kumkimbia kwa kuona ugumu wa kumlea kwa sababu hakuwa na kazi, raha zote hizo angezipata wapi? Hakika Pattie ni mwanamke shujaa! Ni Mama Shujaa kwa sababu amemzaa shujaa na yeye mwenyewe anabaki kuwa shujaa kwa uimara wake na ubunifu wa kuhakikisha mtoto wake anafanikiwa.
ALIPOTOKA
Pattie alishakuwa mtoto wa mitaani, akatumikishwa kuuza madawa ya kulevya kwa rejareja, baadaye akawa mtumiaji (teja). Vilevile alibadilika akawa mwizi, akipora ili kupata fedha za kujisadia katika maisha yake. Ongezea na stori ya kubakwa tangu akiwa na umri wa miaka mitatu mpaka 14.
Leo hakuna mwanaume anamdharau tena, anaheshimika kwa sababu ana pesa, vilevile ni mama wa mwanamuziki maarufu na mwenye utajiri mkubwa. Ukipata mimba itunze, hata kama imeingia bila mipango usiitoe, hujui aliyepo tumboni atakuwa nani. Mwanao mkumbatie! Siku zote tazama mbele kwa matumaini.
Luqman Maloto