sada haziendi kwa Mungu, na Mungu hali sadaka. Kila mtu anatoa na kupokea sadaka kila siku, na ukitoa zaidi utapokea zaidi, mfano kama wewe unatoa michango (sadaka) mingi ya harusi kwa watu wengi zaidi nawewe utapokea michango mingi zaidi kutoka kwa watu kama ukiwa na jambo lako, kama wewe unahudhuria misiba ya watu na wewe utapata watu wengi kwenye misiba utakayoipata. Maana sadaka ni msaada, pale zamani kulikuwa hakuna pesa hivyo sadaka ilikuwa ni chakula, wanyama, na mazao, baadae ikaongezeka nguo na fedha.Ni kweli Mkuu
Kweli KABISA!
Sadaka KWA nyumba za ibada ni wizi uliohalalishwa KABISA na Taasisi!!
Hata zaka walizotoa Wana wa Israel zili liwa na hao watoaji na kubakiza kidogo KWA walawi AMBAO Ndio walipewa jukumu Sasa leo KILA mtu ni kuhani nani wa kumpa mwenzake sadaka!??
Tuwape WAZAZI tu Basi!
Acha kubwia ugoro hiyo kitu huharibu kabisa akili πUnataka kusema yule aliyegundua kibatari alete reference alitoa wapi wazo la kutengeneza kibatari, aliyegundua gari ane alete reference, aliyegundua kuvaa chupi nae aeleze katoa wapi, wewe kaka amka. Hebu elezea namna sadaka yako ya sh. 10,000 iliyompa mtu wa Mungu itakavyomfikia Mungu huko mbinguni. Tueleze kama Mungu ana shida ya hela au nyama. Tueleze hizo sadaka Mungu anaziweka wapi kwa kazi gani.
Hawezi kuapiaApia
Waheshimu baba yako na mama yako.....Umenukuu andiko gani mkuu kujenga hiyo hoja yako?
Na mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."Waheshimu baba yako na mama yako.....
Uunawaacha inamaanisha unaanza maisha mapya na mkeo haimaanishi uwadharau.... Anamalizia uishi miaka mingi na upate heri katika nchi upewayo na BWANA Mungu wakoNa mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."
Guess will happen
Siwezi kuwadharau wazazi wangu ila nitaenda kuanzisha familia pasipo kuwategemea wao (kiuchumi)Uunawaacha inamaanisha unaanza maisha mapya na mkeo haimaanishi uwadharau.... Anamalizia uishi miaka mingi na upate heri katika nchi upewayo na BWANA Mungu wako
inatakiwa uwasaidie, ndiyo maana imeandikwa uwaheshimuSiwezi kuwadharau wazazi wangu ila nitaenda kuanzisha familia pasipo kuwategemea wao (kiuchumi)
Waheshimu baba yako na mama yako ili siku zako za kuishi ziwe nyingi.inatakiwa uwasaidie, ndiyo maana imeandikwa uwaheshimu
Mie nitakuwa katibuNataka kujenga kanisa,mchungaji mwenyewe
na heri duniani, anawasema wanaomjali pastor kuliko wazaziWaheshimu baba yako na mama yako ili siku zako za kuishi ziwe nyingi.
Hakuna upinzani ktk hilo
Ila mtoa mada hajui alisemalo ktk huu uzi wake.
ππππ jamanMie nitakuwa katibu
Tulia nipe ukatibuππππ jaman
Baba na mama yako ndio mungu wapiliNa mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."
Guess will happen
Hivi unaamini tunapotoa sadaka tunataka akazile Mungu?Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako. Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha. Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.
Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.
Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.
kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.
Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.
Kwa hiyo watoto yatima wapeleke hoja zoa kwa nani?Mungu anapokea dhamira na nia sio vitu na matendo yako. Unaonekana unaswali kumbe ni mchawi tu. Usikubali kumpa mtu sadaka, ni chukizo mbele ya Mungu, hahitaji chochote kutoka kwetu zaidi ya kumsifu, kumtangaza na Kumshukuru yeye baasi. Na Mungu hajibu maombi ya mtu mmoja mmoja na wewe huna hadhi ya kuongea na Mungu wala kuoona uso wa Mungu, huna uwezo na dhamani hiyo, wewe utaishia kumuomba mzazi wako tu na yeye atayapeleka maombi yako kwa baba yake na baba yake atayapeleka kwa baba yake ambae siku ya siku yatamfikia Adam na hawa ambao wao ndio wenye hadhi na sifa ya kuyawasilisha kwa Mungu, yaani protocol lazima izingatiwe. Ndiyo maana kama wewe huna mahusiano mazuri na wazazi wako unaowafahamu kwa sura usijihangaike kabisa na maswala ya Mungu ambae hujawahi kumuona.
Sadaka yenye nguvu ni ile inayoliwa na wazazi wako pamoja na familia yako.
Nyingine ni ile inayoliwa na watu mbalimbali wasiojiweza...
Nyie wachungaji uchwara mmesikia au niongeze s
Nataka kujenga kanisa,mchungaji mwenyewe