Usitegemee kujaliwa kama wewe Hujijali

Usitegemee kujaliwa kama wewe Hujijali

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini waungwana mabestito wangu wa ukweeeeee!!!


Hali ya kutokujijali au kujipenda hujitokeza pale ambapo
mtu amekata tamaa sana au pale ambapo unajiachia pasipo
kuona kuwa wewe u wa thamani sana. Pengine rafiki unajiona
kuwa hufai mbele za watu; hii tabia mara nyingi huanza taratibu
sana mpaka baadaye inakuwa imekomaa na hupelekea kutojithamini
pengine labda uliona watu hawakujali wewe ukawa unajithaminisha
kwao bila kujua kuwa ini lazima ujijali mwenyewe ndipo ujaliwe na wengine

Rafiki tafakari na jihoji je unajijali wewe mwenyewe; je unajiweka katika
thamani gani ? je unajiona kuwa umekamilika au la? ukishajiona ukoje ndipo
anza kuona mapungufu yako wapi na uchukue hatua ya ziada ya kujijali wewe

Hutakuta watu wengine hata katika mavazi yao wao wanajiachia tu ilimradi tu
kavaa hajali yeye yukoje kimaumbile ilimradi eti yuko kwenye fashion sasa best
rafiki yangu kwanini ujijali mwengine utakuta kavaa ilmradi yu kwenye nguo
wewe uliona wapi kandambuga na pekosi ukivivaa vikawa vinaingiliana, kama sio
ushamba shosti!!! na kwa WANAUME nao utaona jitu zima limejitwika vesti na
suruali kaunda suti mchana kweupe utadhani anakwenda kuhani sherehe
Bestito ukijipenda na kujijali wewe utajaliwa na wengine hivyo kuwa mtu wa
kujijali wewe usitegemee ashuke mtu toka mlimani au mbinguni akujali best
Kuwa mtu wa kujijali wewe usijiachie achie bestito jipende, jithamini wewe.


Warning: Mamods msimuvuzishe hii kitu hapa please nawasihi


Nawatakia alasiri njema

Wasalaam


Ladyf
 
Back
Top Bottom