Usiseme nchi haina pesa, sema wewe sio kipaumbele

Usiseme nchi haina pesa, sema wewe sio kipaumbele

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,901
Reaction score
1,511
ONGEZEKO LA WATU (9) TISA KWENYE UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ,

kutoka kwa Mchambuzi Malisa GJ anasema katika moja ya andiko lake kuhusu alichobaini kwenye uteuzi wa baraza jipya la Mwaziri wa JPM

Malisa anasisitiza katika uchambuzi wake kipengere cha saba cha andiko lake juu ya uteuzi wa baraza anasema hivi.

" Kubana matumizi ni kwa wananchi na sio wanasiasa. Idadi ya mawaziri na manaibu imeongezeka kutoka 32 baraza la awali hadi kufikia 41 baraza lililotangazwa leo. Ongezeko la watu 9 kwenye baraza. Haya ni mashangingi 9 mapya, ofisi 9 mpya zenye wasaidizi, mishahara 9 mipya, na nyumba 9 mpya kwa ajili ya makazi yao. Vyote hivi vinategemea kodi ya mlalahoi. Na haya yanafanyika ktk kipindi ambacho taifa linabana matumizi." Mwisho wa kunukuu

SASA HII INA MAANA GANI ?

Yaani hii inamaa kuwa kama watu wapya tisa waliongezeka yaani naibu waziri/Waziri

Mshahara wa waziri na naibu waziri hauna tofauti na mshahara wa Mkuu wa mkoa ambao ni Milion 5 kwa mwezi hii bila Marupurupu yaani ni basic salary sio gross salary. yaani hapo hamna house allowances, communication allowance, miscellenous allowances

MSHAHARA WAO TU.

Mshahara wa waziri/naibu ni Mil 5,000,000×9= 45,000,000×12=540,000,0

Sasa Mil 54 × 5 =Mil 270 kwa miaka mitano mshara wa watu tisa tu.

MAGARI V8 KWA WATU TISA
Kwa Mujibu wa Outo Traders Cars V8 jipya ni kati ya milion 230 hadi milioni 300
Mil 230 × 9 =Bil 2.7
Hii ni kwa magari ya watu tisa tu

MAFUTA YA MAGARI YA V8 TISA
Kwa tafsiri nyepesi kila V8 moja lita moja ya mafuta ni sawa kilometre 5 ,Mafuta ya V8 yenye cylinder 8 Kama ikienda zaidi ni faida kwake. Hata sisi kwenye mashirika gari za ofisi huwa tuna approximate 6Kms per litre
Kwahiyo lita moja ya mafuta ni 2,200 hii ni sawa Lita 40 kwa siku ×2200 =88,000 /=
Kwahiyo 88,000x9 V8 =792,000 kw mafuta ya V8,tisa kwa Siku moja sasa ×30
792,000 × 30 =23,760,000 ×12 kwa mwaka hapo × 5 miaka =Bil 1 mil 4000

NYUMBA KWA MWAKA WATU 9
Aliyewahi kua RC Mwanza Ndugu Mulongo aliwahi kupata kashfa ya kukataa nyumba ya serikali akaenda kupanga Capripoint. Habari iliyochapishwa na gazeti la mawio wakati ule ilionesha RC alikua akilipa kodi ya TZS 1.8M kwa mwezi kama kodi ya pango. Hii ni zaidi ya M20

Kwa tafsiri hii ni kwamba
Nyumba ya waziri /Naibu Mil 1 hadi Mil 2 kwa mwezi
Mil 1.5 ×9 watu mil 13.5 kwa mwezi =162Mil ×5Miezi = Mil 810

OFISI YA WIZARA MPYA

operational cost za ofisi ,Wizara pamoja na watumishi wake hardly inaweza kuoperate kwa labda M.10 kwa mwezi. Hizi ni operation cost tu za kawaida kama stationeries, umeme, maji, usafi, ulinzi, etc. Hujaweka gharama za Waziri/Naibu au Katibu akienda kufanya kazi za field, it takes some more.

So tufanye 10M kwa mwezi kwa mmoja × 9 upate 90M kwa mwezi then × 12 miezi = Bil 1.8 × 5miaka = Bil 5.4


JUMLA
Mshahara............ Mil 270
V8 tisa mpya ........Bil 2.7
Mafuta ya V8 miaka 5 =.................Bil 1 mil 400 .
Ofisi na Operation Cost= ..........Bil 5.4
Nyumba .............Mil 810
Posho na Matumizi Mil ..........................300




Total hii ni zaidi ya Bilioni 13 na Milioni 200 kwa miaka 5 huduma ya Watu 9 tu walioteuliwa ,


JE BILIONI 13.2 ZINGEWEZA KUFANYA NINI KWA VIJANA WA TANZANIA


Nchi ya Tanzania ina miko zaidi 28 na katika kila mkoa kuna Vijana zaidi ya asilimia 45%ambao ni sawa na wastani wa Vijana mil 2.5 kila mkoa

Katika kila mkoa pia kuna wastani wa vikundi 200 hadi 300 vya vijana vya Ujasiriamali hivi ni sawa vikundi zaid ya 4000 vilivyo hai

Kwahiyo Bil 13.2 ukigawa kwa vikundi 4000 vilivyo hai mikoa ya tanzania ni sawa
Milioni 3 laki 2 na Elfu hamsini kwa kila kikundi nchi nzima ,

Ambapo hivi vikundi 4000 kila kikundi kina vijana 15 hadi 20
Vijana 20× 4000 = 80,000 kwahiyo nchi hii ingeliwezesha kutengeneza ajira binafsi nje ya serikali Ajira elfu themanini kila baada ya miaka mitano,

Katika vikundi hivyo 4000 assume ambavyo vingesimama ni vikundi 3000 alafu vikundi 1000 vingekufa kutokana na usimamizi mbovu ,

Vikundi 3000 vingeliweza kuajiri Vijana wengine 10 katika kila kikundi
10× 3000 = 30000 ajira mpya kutoka kwenye vikundi

FAIDA ZA VIKUNDI 3OOO

Assume kila kikundi miongoni mwa 3000 kingepata faida ya Mil 2 kwa mwaka
Mil 2000000×3000 = Bil 6 kwa mwaka
Kwahiyo Bil 6 ×5miaka =Bil 30

Kwaiyo kumbe awa vijana ndani ya mwaka mmoja

Wangerudisha bil 13.2 ya serikali
Wangetoa ajira zaid ya Elfu 30 ndani ya miaka 5
Wangelipa kodi ya Tanzania
Wasingetegemea ajira serikalini,
Tungekuwa na vijana wengi matajiri.
Tungepunguza idadi ya wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya,
Tungepunguza wanywa viroba nk.

Kuwazesha vijana kumbe Inawezekana Malisa aiseh ,
Tusilalamike Nchi haina ela issue ni je wewe Ndio kipaumbele?



Kaza kijana
 
mbona huja hujadadavua hao mawaziri watatuletea faida kiasi gani hlf tukompee na hayo matumizi
 
kutoka kwa Mchambuzi Malisa GJ anasema katika moja ya andiko lake kuhusu alichobaini kwenye uteuzi wa baraza jipya la Mwaziri wa JPM

Malisa anasisitiza katika uchambuzi wake kipengere cha saba cha andiko lake juu ya uteuzi wa baraza anasema hivi.
Typical.
 
hapo kwenye mahesabu ya mshahara naona umefeli pamoja umekosea kuzidisha kwa miaka 5 7bu mpk utawala huu ufikie ukingoni imebaki takrbani miaka mitatu
mshahara ml 5 × mawaziri 9 = ml 45 kwa mwenzi
zidisha kwa miezi 12 ni mln 540 ambapo kwa miaka mitatu ni bln 1.62 hivyo mln 270 ni ndogo
 
hapo kwenye mahesabu ya mshahara naona umefeli pamoja umekosea kuzidisha kwa miaka 5 7bu mpk utawala huu ufikie ukingoni imebaki takrbani miaka mitatu
mshahara ml 5 × mawaziri 9 = ml 45 kwa mwenzi
zidisha kwa miezi 12 ni mln 540 ambapo kwa miaka mitatu ni bln 1.62 hivyo mln 270 ni ndogo[/QUOTE

umesahau mswada wa NKAMIA mkuu?? tunaenda hadi 2022
 
Wallet nzuri ni ile yakwako, account salama ni ile uliyo na password yake,saka hela kijana mwachie bwana serikali atumie hela zake zimzowee,ukimfatilia sana utadanja bila sanda ! Shauri lako.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
hapo kwenye mahesabu ya mshahara naona umefeli pamoja umekosea kuzidisha kwa miaka 5 7bu mpk utawala huu ufikie ukingoni imebaki takrbani miaka mitatu
mshahara ml 5 × mawaziri 9 = ml 45 kwa mwenzi
zidisha kwa miezi 12 ni mln 540 ambapo kwa miaka mitatu ni bln 1.62 hivyo mln 270 ni ndogo
Mkamia aliomba iongezwe miwili so mpk 2022
 
Nimesoma hii thread huku naimagine mimi ni kati ya hao tisa....nimetabasamu tu....
Btw serikali ni kampuni.. Wanachofanya hapo ni kama kampuni...maslahi ya kampuni
 
Back
Top Bottom