Usiri katika sekta ya madini wazidi kuimarishwa

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

Maofisa Usalama wawatimua waandishi




Katika hali isiyokuwa ya kawaida Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, jana amekutana na wawakilishi wa Kampuni ya Barrick na wazee wa mila lakita kikao ambacho maofisa Usalama wa Taifa walilazimika kuwatimua waandishi wa habari na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo bila sababu za msingi.

Hali hiyo ilijitokeza majira ya saa 4 asubuhi baada ya wazee wa mila na wakilishi wa kampuni hiyo inayomiliki mgodi wa dhahabu wa North Mara kuwasili katika ukumbi wa halmashauri tayari kwa ajili ya kujiorodhesha majina.

Katika hali ya kushangaza, ghafla Ofisa Usalama wa wilaya hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alimwagiza Ofisa Tawala, Baraka Nyamsenda, kuwatoa nje waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya habari pamoja na madiwani.

Aidha, Diwani wa Kata ya Sabasaba, Christopher Chomete, alikaidi amri hiyo ambapo ilibidi polisi kuingilia na ilidaiwa kuwa waandishi hao akiwamo wa gazeti hili hawakuwa na mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

Ilidaiwa kuwa waziri huyo alikuwa alikuwa ameambatana na mwandishi wake kwa ajili ya kuandika habari hizo.

Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Waziri kivuli wa mambo ya Ndani, Godbless Lema, alilaani hatua hiyo na kusema kuwa wananchi wa wilaya hiyo wamenyimwa fursa ya kueleza kero zao sanjari na kukandamiza uhuru wa habari.

Rais Jakaya Kikwete aliwahi kutoa maagizo kwa watendaji wakuu serikalini kutoa taarifa sahihi kwa wananchi juu ya utendaji wa wizara na taasisi zake……..

Chanzo: T. Daima
 
Hakuna siri tena siku hizi, kama wakifunga mlango wa mbele basi itatokea mlango wa nyuma, maana tunao watu wetu humohumo maofisini.
 
Hii Nchi ufisadi utaisha lini? Hivi kweli tutapata maendeleo chini ya ccm ikiwa inakandamiza wananchi?
 
Back
Top Bottom