Usipojipanga Utapangwa!

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
USIPOJIPANGA UTAPANGWA

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?

Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)

*Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu...!

1. wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)

2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa)

3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia)
Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?

Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.

4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..

Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..?
Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)

Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..

-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zake...!

JE WEWE UPO KUNDI GANI?

WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..
 
Ujumbe mzuri sana, wenye akiri na tuusikie na kuufanyia kazi
 
Yote ni kweli ila pamoja tu mkuu, matajiri pia wanakuwaga busy mno mjomba! Hao unaowataja kina Mengi ukiambiwa ratiba yao ya siku hutaamini
 
Wapo wenye pesa kiasi na mda kiasi wa "kusocialize" na watu, hawa ukiwapa kadi ya mchango watakuchangia pesa nzuri na kwenye sherehe watakuja.
 
USIPOJIPANGA UTAPANGWA

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?

Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)

*Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu...!

1. wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)

2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa)

3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia)
Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?

Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.

4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..

Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..?
Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)

Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..

-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zake...!

JE WEWE UPO KUNDI GANI?

WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..
basi wewe utakua namba 1 maana umekua na muda mkubwa wa kuwaza haya mambo ya maisha
 
Maixha ni yaleyale hata matajir wana shida suala siyo pesa Bali ni kuwa na amani moyoni mwako kwasababu sote tunakufa
Usilolijua ni usiku Wa Giza .hao unaowaona kuwa wameshakua matajiri labda wamerelax ndio shughuli mtindo mmoja yaani mikopo yao ni mikubwa wapo busy na mawazo ya kutosha .

MF.kuna Jamaa mmoja yuko na hoteli mbili gorofa ila analalama marejesho unamkuta amekondeana unafikiri fedha ya masharti ya mganga kumbe mwenzio ni mikopo ya mabenki .

Mara mabrocker Wanataka kuuza Mara hivi Mara vile yaani kwa kifupi maisha yetu hayana tofauti Kubwa uwe una uwezo kidogo au kiwango Fulani pia inachangiwa na hulka yetu ya kutoridhika.
 
Ata hao unaosema wana pesa na muda,tambua hizo pesa hazikuja kirahisi...kna mda walikuwa hawana muda kabisa ila mambo yalivokaa sawa ndo unawaona hvyo,cha msingi kujinga katika umri wako mapema tangu ukiwa kijana nguvu unazo
 
Back
Top Bottom