Habari wanajamvi wenzangu hapa MMU
Napenda kuwapongeza wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa nami
kila ninapotoa thread humu mjengoni, napenda kuwashukuru marafiki zangu wote ambao
wamekuwa mstari wa mbele kutoa comments zao na kuleta umakini wa hali ya juu ili ujumbe
ufike unapostahili yaani kwa walengwa watarajiwa.
Ni mara nyingine tena leo nimekuja kivingine kabisa. Leo siendi kwa gia bali naenda kwa wino
Marafiki zangu nimetafakari na kujiuliza maswali mengi sana ambao yamenifanya leo niweze
kununua kalamu na kuanza kuandika haya yaliyonipata kutoka kwa mawazo yangu.
Nimejiuliza hivi ni kwanini watu wengi hususani wanawake wajiona kuwa wao nidhaifu sana na
hawana upeo wa kuona ama kufikiri jambo gani la kufanya mpaka wawashirikishe wanaume, ndipo wagundue kuwa wana uwezo wa kulifanya hilo? Wengi wao wamegubikwa na wingu la kutokujua ama kutoweza kufanya, hususan wanao uwezo wa kutekeleza kile ambacho wamekiona kigumu kwao.
Na hata imepelekea kubadilishwa kwa maamuzi na misimamo yao kuyumba kutokana na dhana ya ufinyu wa mawazo yao yasiyoweza kupembua na kuchuja nini cha kufanya. Kwa mfano halisi mtu unataka kufanya kitu ambacho una utaalamu nacho, lakini inatokea katika fikra zako ukaogopa kufanya ilihali unao uwezo na ujuzi wa kulifanya jambo hilo. Ni kitu gani kinafanya usifanye? Kwanini unataka watu wakutendee badala ya wewe kutenda hilo jambo? Kwanini unaruhusu watu wakubadilishie msimamo wako wakati wewe mwenyewe hungeweza kufanya?
Wengine wamediliki hata kuona kuwa hawana jinsi yoyote ya kujikwamua katika maisha mpaka wauze miili yao ndipo wapate chakula cha siku hiyo, ndugu yangu hapo unajidanganya, kwanini unakosa kuuthamini mwili wako? na hata wako wengine wamekuwa wavivu wa kufikiri ni jinsi gani wanaweza kujikwamua hapo walipo? wanataka Watu ama jumuiya fulani iwasadie kutatua matatizo yao, na wakati uwezo wa kufanya wanao, ujuzi wanao, hekima na maarifa wanayo. Sasa nini tena kimebaki ufanyiwe? Kwanini unapenda watu wakubadilishie misimamo yako jamani?
Hebu kuwa mtu mwenye kusimamia yale uliyojiwekea au uliyojipangia usipende watu wakubadilishie msimamo wako rafiki yangu. Fanya kana kwamba utafanya tena jambo ulilojiwekea kulifanya kwa wakati ulionao kwani hakuna muda udumuo hapa duniani. Kama una nguvu sasa za kufanya au kutenda tenda yale uliyojikusudia kutenda. ACHA TABIA YA KUPENDA WATU WAKUBADILISHIE MAAMUZI/ MISIMAMO ULIYOJIWEKEA RAFIKI YANGU.
Siku njema