Usimpe mtu pesa bure

Nyamwage

Member
Oct 16, 2020
93
150
Habari. kumekua na wimbi kubwa la marafiki au watu wakaribu mnaofahamiana nao au hata msio fahamiana wamekua na kawaida ya kupiga vizinga yaani kuomba vipesa vidogovidogo hili swala kwa sasa haliniumizi tena kichwa ni baada ya kuombwa kihela kidogo kama 10k na jamaa mmoja hivi akanunue kileo tunafahamiana mimi nilimchukua nikampeleka kwenye kijumba changu kinachoendelea na ujenzi kutoka hapo saiti na ninako nunua tofali sio mbali na ninapo jenga ni pua na mdomo nilikua nimelipia tofali kadhaa bado tu kuzihamishia kwenye eneo langu ili zijengwe nilimwambia huyo jamaa kuwa siwezi kukupa pesa bure utalemaa bro tupatane uzisogeze hizo tofali hapa saiti kwangu ili nikulipe tukabaliana kiasi cha pesa akazihamisha jioni nikamlipa pesa tuliyo kubaliana tangu nimeanza kuwa na hii desturi nikiombwa pesa na mtu nampa mtu kikazi anakifanya ndio nampa pesa kwa sasa wimbi la kuombwa vipesa tofauti na kukopwa naona linapungua taratibu kadri siku zinavyo zidi kwenda na ninamshukuru Mungu kwa hili.
 
Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
10,184
2,000

Inategemea mtu kakuomba pesa kwa shida gani, sio kila ombi la pesa ni lazima umtumikishe mtu.
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
13,440
2,000
Acha ubahili
Kutoa Ni Bora kwa nafsi yako kuliko kupokea
IMG-20210805-WA0006.jpg
 
Trendz

Senior Member
Jun 27, 2021
102
250
Roho ya kimasikini hiyo
Jifunze kusema SINA inasaidia pia hata kama unayo
Mama mtu mzima kakuomba hela basi umtumikishe?
Ukiombwa sio lazima utoe hata kama unacho sema SINA maisha yaendeleee
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,172

Hela mtu unayo.. lakini ina shughuli. WaTz wanapenda sana kuomba. Yani wakiona umebarikiwa ni shida. Ilibidi binafsi nijenge ukuta wa fensi wa eneo la ekari 3 sababu walikuwa wananivizia wakiniona tu wanalia shida. Ukuta ulisaidia sana. Utasema huna kwa wangapi? Inakuwa ni kero watu kuomba omba tu tena mara ya chai mara ya soda wala sio shida za maana. Nasaidia, lakini naamua ni nani. Mfano wiki hii tu kuna mama alikuwa anapigwa na mumewe asifanye ujasiriamali. Siku akaamua kukimbia ila hana nauli. Akaja kwangu. Nikampa na cruza ya kumpeleka hadi stendi na hela juu.
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,172
2,000
Hii ninaitumia pia ila siyo kila mahali. Shangazi akiniomba hela nimpe ndoo akabebe maji anijazie ndani nimlipe? Suala lako linategemea na mtu na hali.
Binafsi familia nzima ndio na uwezo mkubwa zaidi. Mashangazi, mabinamu, wajomba, nilikuwa nawasaidia sana. Ada, hela ya shule, kula nk. Nilijifunza somo siku mzigo mkubwa umeingia bandarini, nikapungukiwa 5 million hivi. Wiki hio hio nilisaidia shangazi wawili ada za watoto nikijua hela itakayobaki itatosheleza kabisa. Nikamsikia shangazi anaongea kwa simu .. amegawa gawa hela hadi kashindwa kutoa makontena. Nilikuwa mbogo, na tokea hapo nikakata mawasiliano. Nasaidia mazishi tu au ugonjwa. Shida nyingine wapambane na hali zao. Tena hata wakati napambana kwenda USA kulikonitoa ndg wote walinidharau na kunifanyia visa. Niliwasamehe, bado wakaleta ujinga. Tokea niache kutoa misaada ya ovyo mingi ndio mibaraka kwangu inazidi. Hata Mungu anataka tuwe stewards wazuri wa mibaraka. Kila mtu ana nguvu na wasiwe omba omba.
 
mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
761
1,000

Aisee, ngoja tuendelee kuishi mkuu, usiwe serious sana na maisha mkuu wangu
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,172
2,000
Aisee, ngoja tuendelee kuishi mkuu, usiwe serious sana na maisha mkuu wangu
Siko serious ndg yangu. Nasema tu uhalisia. Kila mtu anapenda hela.. ila kwa mtu uliyefanikiwa sana unafahamu mwenyewe vile umepambana kufanikiwa. Hao wengine wanataka wale tu jasho lako kiulaini. Haiko ivyo.
 
gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
7,780
2,000
Kuna jamaa yangu yeye anasema hawezi mpa hela mtu mwenye miaka chini ya 60 ni bora akaonge malaya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom